Mtizamo wako umeingia kwenye ukabila, Mimi nilijikita kwenye kupata urahisi wa kusafiri hasa Kwa Wale wasiyo miliki gari binafsi.
Naendelea kukurekebisha!
Mimi sijaongelea ukabila, wewe ndiye ulileta hoja yenye mlengo wa ukabila!
Ulisema kwamba watu wanakosea katika kufanya maamuzi wapi ni mahali sahihi pa kujenga makazi yao. Ukasema eti ilifaa tangu mwanzo watu WAJENGE MAENEO YALIYO RAHISI NA BARABARA ZA KWENDA KWAO. Huu ni ushauri wa kipuuzi kabisa una lengo la kuleta ukabila hapa nchini. Hivi kila watu kwa makabila yao wakiamua kujenga mahali rahisi na njia ya kwenda kwao huko so kuleta matabaka ya kujigawa kikabila hapa nchini?!
Maana yake ulitaka watu wa kaskazini wajenge maeneo ya kaskazini mwa DSM , watu wa nyanda za juu kusini wajenge maeneo ya magharibi mwa DSM , na watu wakusini wajenge maeneo ya kusini mwa DSM, so ndio njia rahisi za kwenda kwao?! Huu ni ushauri au upuuzi mtupu?! Unataka kutengeneza taifa la aina gani?! Lenye watu walinaoishi kwa kujigawa maeneo kwa kuzingatia ukabila wao au kanda zao?! Sasa hapa nani kaleta ukabila kama sio wewe kwakushauri upuuzi mtupu! Tanzania ni taifa lenye umoja na mshikamano mtu anaishi popote bila kujali ni wapi, ni jukumu la serikali kuhakikisha usafiri unapatikana bila kujali eneo husika.
Lakini pia umejikita mbagala hujaniajia kampuni mojawapo iliyokuwa inapakia abiria kutoka kigamboni, hujaongelea uwanja wa ndege pia, nimesema majiji yote makubwa duniani ya centers ambazo ni main hub ya usafiri umma, nilianza Kwa kueleza mwanzo stendi ilikuwa Kisutu siyo? Baadae ikaamia ubungo, abiria woote kutoka Dar ukiacha Wale WA mbezi, kiluvya, kibamba na kibaha wakawa wanaenda ubungo, baadae kidogo kidogo mabasi yakaanza Ku opt njia ya Bagamoyo Wale WA maeneo niliyotaja hapo juu wakalizimika kuyafuata, Leo serikali imefanya uwekazaji wa mabilioni mbezi hawawezi kuruhusu kila basi au kampuni ikawa na kijiwe chake. Naendeleo ni gharama
Maeneo Yote hayo uliyoyataja walikuwa wanapandia kwenye vituo vyao vya karibu kwamaana kupandia kwenye vituo au ofisi za mabasi kulikuwa hakuja zuiliwa kama sasa. Kwamfano kigamboni kulikuwa na mabasi ya Kilimanjaro na tashriff . bunju- tegeta mabasi mengi yanayopita bagamoyo road yalikuwa yanapakia kule.
hujaongelea uwanja wa ndege pia, nimesema majiji yote makubwa duniani ya centers ambazo ni main hub ya usafiri umma,
Ngoja nikuelimishe kidogo, sijui kama umebahatika hata kukaa huko nje unakojaribu kupaongelea,
Wenzetu nje wenye main hub, wanausafiri wa uhakika usifananishe kwa wenzetu na hapa kwetu ambapo Siku mwenye daladala lake akijisikia halitoki kufanyakazi, kwao kuna mabasi ya umma ya uhakika, kuna train na tram za uhakika, sio kama huku ampako raia anatakiwa kupanda daladala tatu mpaka afike bus terminal.
Pia wenzetu wana mipango miji mizuri vituo vikubwa vya mabasi vipi center ya mji sio pembezoni kama huko mbezi Luis, tena kufika main hub zao huamki usiku wa manane kugombania daladala kisha ukae kituoni kusubiri daladala lijae hapo bado ujapanda daladala mbili au tatu ufike terminal. Usafiri wao ni wauhakika.
nilianza Kwa kueleza mwanzo stendi ilikuwa Kisutu siyo? Baadae ikaamia ubungo, abiria woote kutoka Dar ukiacha Wale WA mbezi, kiluvya, kibamba na kibaha wakawa wanaenda ubungo, baadae kidogo kidogo mabasi yakaanza Ku opt njia ya Bagamoyo Wale WA maeneo niliyotaja hapo juu wakalizimika kuyafuata,
Sijui umekuja lini Dar???!
Ngoja nikueleweshe tena!
Kituo cha mabasi hapa Dar, wanzoni kabisa kilikuwa pale Kariakoo, Gerezani kikapewa jina la kampuni ya mabasi ya KAMATA, pale karibu na traffic lights,wanapaita kamata mpaka Leo.
Baadae wakadai watu wamekuwa wengi na mabasi mengi hivyo kukwepa msongamano wakakihamisha kile kituo kikapelekwa pale MNAZI MMOJA.
Vivyo hivyo kama ilivyokuwa kwa madai ya kwanza kituo kile cha mnazi mmoja nacho kikahamishwa kupelekwa pale KISUTU..(hapa ndipo ulipopajua kuwa kituo kilianzia hapo kisutu kumbe sivyo kilianzia KAMATA)
Pale Kisutu pia kituo kikahamishwa kwa madai yaleyale kuwa kumekuwa na msongamano na mabasi yamekuwa mengi, kikahamishiwa kule UBUNGO,
Ubungo nako kimekuja kuhamishwa na kupelekwa huko pembezoni kabisa mwa jiji MBEZI LOUIS.
Sijui na huko kitakuja kuhamishwa tena kwamadai ya msongamano na traffic jamm na kukipeleka KIBAHA au CHALINZE.
Hata hivyo unapotosha watu kusema eti wakati kituo kipo KISUTU watu walitoka sijui bunju , gongolamboto etc nakukifuata kule, ndio maana nina mashaka na uelewa wako au wewe ni mgeni hapa jijini. Wakati kituo kipo KAMATA, MNAZI MMOJA NA KISUTU, Jiji la Dsm lilikuwa dogo sana, halijatanuka kama Leo, maeneo ya mbagala yalikuwa pori tu mji uliishia hapo mtoni mtongani,temeke sudani nk. Kule tabata, ubungo na bunju kulikuwa pori tupu hata ukimuuzia mtu kiwanja hataki kununua. Kwahiyo kisutu haikuwa mbali na wakazi wa DSM.
Tatizo Hapa ni mipango miji, hatuna mipango ya muda mrefu kwamba baada ya muda Fulani let say miaka 50 au 100 Jiji la Dar litakuwa na wakazi kiasi gani? Je, watakidhi kutumia bus terminal itakayo jengwa Leo? Je, trafficking itaweza kuhimili mabasi yanayotoka kwenye terminal hiyo? Ukosefu wa plan hii ndio unapelekea kuhama hama kama Kobe!
Leo serikali imefanya uwekazaji wa mabilioni mbezi hawawezi kuruhusu kila basi au kampuni ikawa na kijiwe chake. Naendeleo ni gharama
Unatetea bila kufikiri, hakuna anayepinga uwekezaji wa serikali,
Lakini je, umezingatia kuwasaidia watanzania wanyonge? Una rahisisha usafiri wao au unawakandamiza zaidi?!
Hakuna mtu anayetetea kuwa na kijiwe cha mabasi, tunachotaka mabasi yaruhusiwe kupakia abiria walio mbali na terminal lakini wakishapakia waende terminal kukaguliwa na sio kuwapa mzingo abiria wa bunju akapandie basi mbezi Luis wakati basi ilohilo linapita njia ya bagamoyo kwenda kwao. Au abiria wa mtwara kutoka kisemvule akapandie mbezi Louis kwakupanda daladala mbili, wakati basi hilohilo litapita hapo kwenda kusini.
Kama hilo haliwezekani basi ni vyema serikali iboreshe usafiri wa daladala kuwe na route moja kutoka maeneo yote ya jiji kwenda mbezi Louis bus terminal tena uwe usafiri wa uhakika, sio kama sasa ambapo msafiri analazimika kuamka saa tisa usiku na watoto na mizigo tena aunganishe daladala mbili au tatu! Hapa bado hujawasaidia watanzania! Hivi hao mipango miji huwa wanalifikiria hili au sisi tunakurupuka kusifia tu majengo mazuri na uwekezaji wa mabilioni?!
Good for nothing!
*********