Maswali magumu: Utetezi wa Jakaya Kikwete dhidi ya tuhuma za chuki binafsi dhidi ya Hayati Magufuli msibani

Maswali magumu: Utetezi wa Jakaya Kikwete dhidi ya tuhuma za chuki binafsi dhidi ya Hayati Magufuli msibani

Kwani mtu akiwa rafiki yako huwezi kumkwaza? Tena bora JPM alienda kumshitaki kwa broo wake maana angeenda kwa mtu tofauti ingekuwa ni kumfitini Rais kitu ambacho kingemfanya atupwe nje ya ulingo.

Hapo JPM alicheza kama CR 7 maana kwa broo wanajadili kiundugu but tofauti na hapo angepotezwa
Swadakta!
 
JK ni Mswahili kama Waswahili wengine tu wa Pwani. Kuna sehemu alisema JPM alikuwa akimshtaki kwa kaka yake (JK) mara zote alipo mkwaza!! Mara alimpenda sana!! [emoji56]
Kwani watu wakipendana hawakwazani?
 
Siasa za bongo Tanzania za kijinga sana,Chadema sasa wameamua kujiunga na team ya msoga...wameachama na chama chao kabsaa!!!Hivi na 2025 mkishindwa uchaguzi mtalalamika mmeibiwa kura?
 
”Duniani waganga njaa wengi, wengine wanapata ugali wao kwa kuongopa.”
Jakaya Kikwete, Chato
26/03/2021
Mleta maada kama huu msumari cyo wako hebu jifanye J.K na uwasilishe salaamu zako ukishindwa ujumbe huo wa mzee wa msoga ubebe unakuhusu
 
JK leo tumekusikia ukijitetea kuwa watu wameanza kuzusha mitandaoni eti wewe ulikuwa unamchukia JPM na pengine ukawa mmoja wa maadui zake wakati wa utawala wake. Majibu yako yalikuwa mepesi saana kama kawaida yako "Mswahili" nanukuu "eti kama kweli ningekuwa namchukia JPM nisingeweza kupitisha jina lake katika mchakato wa kuwania Urais 2015 kwani mimi (kama Rais na Mwenyekiti wa chama) ndiye niliyepeleka majina matano (5) Halmashauri" na ukaenda mbele zaidi ukasema katika kuchagua majina matano jina la kwanza lilikuwa la JPM alafu yakafuatia mengine manne. Umeenda mbele zaidi na kusema kuwa alikuwa jembe lako katika baraza lako la mawaziri huku ukijikanganya zaidi na kusema mlipokuwa mnatifuana JPM alikimbilia kupeleka mashtaka kwa kaka yako mkubwa ambaye ni marehemu sasa.

Maswali magumu:

(i) Je, kwani wewe ndiye uliyependekeza hayo majina matano au ni CC ya chama chako ndiyo iliketi na kukuletea wewe kwa ajili ya kuyawakilisha Halmashauri? Labda tusaidie kwani hayo majina ulitoka nayo nyumbani kwako kwa kushauriana na familia yako?

(ii) Je, si kweli JPM aliingizwa katika tano bora baada ya kuona "mamvi" hawezi kuaminika katika chama na wananchi wanataka mchapakazi asiyekuwa na doa ili kukikomboa chama kilichokuwa kinaelekea kuanguka na sio kwa mapenzi yako binafsi?

(iii) Hivi mashtaka aliyokuwa anapelekea JPM kwa kaka yako mara kwa mara yalihusu nini kama kweli alikuwa jembe lako katika baraza lako?

(iv) Mwisho japo sio kwa umuhimu. Unajuaje pengine watu wanasema chuki zako dhidi ya JPM zimeanza kuonekana zaidi baada ya yeye kuwa tayari ni "Mkuu" kwa maana ya kuwa hukuwa na jinsi tena ya kubatilisha maamuzi yako?
Kama unamajibu yako unauliza ili iweje yeye ndo ameshasema yake ilivyokuwa bila hata kuulizwa
 
JK mtamchukia na kumtukana kwa kila namna lakini ukweli utabaki kuwa kwa ujanja tu jamaa yuko mbali sana....bila kupenda mtaendelea kulitaja jina lake mpaka siku anaingia kaburini.

kwani kukwazana ndo uhasama?!!!! wanakwazana wanandoa ndani itakuwa wanasiasa waliojuana siasani!!! uzuri mmoja jamaa akishasema anatulia tuliii anajilia zake mananasi msoga huko hana hata muda wa kushughulika nanyi hadi siku anayoamua. na akiamua kujibu siku hiyo (kama alivyofanya leo) anakuacheni na kazi tena ya kujadili kama hivi........mumwache tu hamumuwezi, kuna kitu amepewa lazima tukubali tu!
Aahahaaah hakika tumuache tu😂
 
Mi sioni sababu ya kuhoji aliyoyaeleza JK, yeye ndiyo kasema JPM alikuwa jembe na rafiki yake hadi akatafutiwa kiwanja Chato, sasa unapopinga na kuhoji unamaanisha nini? Yaani unabishana na mtu anaekuelezea yake ya moyoni mwake!Hii nayo ni habari nyingine sasa mkuu.
Mjinga wewe
 
Jitu lilishindwa kupendwa hata na mkewe seuzw na kuchukiwa na jk?yaani jiwe lilikua na gundu hakuna mpenda haki alompenda yule mnafiki
Ungeenda kusema hayo msibani au kwa wale walokuwa wakitandika kanga njiani ili zikanyagwe na gari lililobeba mwili wake uone kama ungetoka mwili ukiwa ukiwa na roho yako i see! Kuna watu wa ajabu sana...eti Magu alichukiwa😳!
 
Mimi sijawahi kumchukia JK! Maana katika miaka yake ya Urais, alitupatia stahiki zetu zote mihimu kama watumishi wa umma! Nilicho maanisha hapo ni kwamba, mzee ni mswahili na ana maneno na vijembe vingi.

Ni kawaida sana kwake kumpiga mtu kijembe kwa maneno na misemo tofauti, huku anacheka!
Hata marehemu kipindi cha uhai wake alikuwa ni mtu wa vijembe
 
JK ni Mswahili kama Waswahili wengine tu wa Pwani. Kuna sehemu alisema JPM alikuwa akimshtaki kwa kaka yake (JK) mara zote alipo mkwaza!! Mara alimpenda sana!! 😇
Huu wote ni uongo. Kama ni kweli, mbona alienedelea kuwa naye katika baraza la mawaziri. Hivi inakujia akilini mwako, kuwa wewe ndiyo mkuu na mwenye uwezo wa kuteua na kutengua eti mtu aakushitaki kwa raisi mstaafu wewe unaendelea kuvumilia kuwa nate. Kumbuka raisi anateua na kutengua uteuzi bila kuwashirikisha marais wastaafu.
 
Siasa za bongo Tanzania za kijinga sana,Chadema sasa wameamua kujiunga na team ya msoga...wameachama na chama chao kabsaa!!!Hivi na 2025 mkishindwa uchaguzi mtalalamika mmeibiwa kura?
Upinzani uliopo kwa ss ni upinzani wa ccm ya zamani vs ccm ya sasa.

Chadema hawana cha kupoteza tena maana chini ya ccm ya sasa walipoteza vyote.
 
Mi sioni sababu ya kuhoji aliyoyaeleza JK, yeye ndiyo kasema JPM alikuwa jembe na rafiki yake hadi akatafutiwa kiwanja Chato, sasa unapopinga na kuhoji unamaanisha nini? Yaani unabishana na mtu anaekuelezea yake ya moyoni mwake!Hii nayo ni habari nyingine sasa mkuu.
Labda yeye atuambe JK angesemaje basi kama hayo aliyoyasema yeye hakubaliani nayo.
 
Hii inanikumbusha miaka niko form four. Nilimsaidia sana kijana mmoja kuwa Raisi wa serikali ya wanafunzi shuleni. Baadaye akanigeuka. Kwa kawaida wanafunzi huvaa mashati ya mikono mifupi isipokuwa viongozi na wastaafu. For one reason or another na mimi nilikuwa navaa shati la mikono mirefu. Sasa huyu president niliyemuweka madarakani akawa amepanga kulikata mikono shati langu mbele ya halaiki. Na mimi nilishtukia mchezo kwa kuondoka assemble na kwenda kubadili bwenini. Alinitafuta sana pale assemble ili atimize nia yake ovu ila hakunipata. Kijana huyu nilikuja kumpokea tena akiwa form five na mimi nikiwa form six pale Mzumbe sec na nilimsaidia kwa hali na mali mpaka alipokuwa mwenyeji.
 
Ulikuwa na upendo wa dhati mkuu!!!!,kwa jinsi ninavyo jijua mm pangechimbika.
 
Back
Top Bottom