Maswali mengi yaibuka baada ya kupotea kwa mkazi wa Kigamboni Vicent Masawe. Mkewe asimulia kilichotokea. Jeshi La Polisi latoa tamko!

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumezuka na tarifa kuwa Vicent Peter Masawe, anayejulikana pia kama Babuu au Bright, amepotea tangu Novemba 18, 2024. Kulingana na taarifa zilizopo, siku ya tukio, Vicent alidai kufuatiliwa na watu wasiojulikana kabla ya kupoteza mawasiliano.

Vicent, ambaye ni mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na hufanya shughuli zake za kila siku Magomeni, alionekana mara ya mwisho akiwa na gari lake lenye namba za usajili T 642 EGU, aina ya Ractis (Old Model).

Kwa mujibu wa maelezo ya mke wake, mara ya mwisho walizungumza kwa simu ambapo alieleza wasiwasi wake kuhusu kufuatiliwa. Baada ya mazungumzo hayo, juhudi za kumpigia simu tena hazikufanikiwa, na hadi sasa hajulikani alipo.

photo_2024-11-25_16-15-55.jpg

Tukio hili tayari limeripotiwa polisi na uchunguzi unaendelea. Hata hivyo, msaada wa raia wema unahitajika katika kufanikisha kupatikana kwake. Ikiwa una taarifa yoyote kuhusu alipo Vicent au gari lake, tafadhali wasiliana na familia kupitia mawasiliano yao au toa taarifa kwa kituo cha polisi kilicho karibu.

Tuendelee kushirikiana kwa nia njema ili kuhakikisha Vicent anapatikana salama.

Msaada wako kama raia mwema kufanikisha kumpata, mawasiliano ya ndugu kwa taarifa

0719 293 117
 
Kwanini wanaopotea wengi ni Wachagga

USSR
 
Wakipigwa mawe utasikia ooh walikua TRA, lakini wakifanikiwa kukuteka umetoweka. Mliro anasemaje kwenye hili
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii kumezuka na tarifa kuwa Vicent Peter Masawe, anayejulikana pia kama Babuu au Bright, amepotea tangu Novemba 18, 2024. Kulingana na taarifa zilizopo, siku ya tukio, Vicent alidai kufuatiliwa na watu wasiojulikana kabla ya kupoteza mawasiliano.

Vicent, ambaye ni mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam na hufanya shughuli zake za kila siku Magomeni, alionekana mara ya mwisho akiwa na gari lake lenye namba za usajili T 642 EGU, aina ya Ractis (Old Model).

Kwa mujibu wa maelezo ya mke wake, mara ya mwisho walizungumza kwa simu ambapo alieleza wasiwasi wake kuhusu kufuatiliwa. Baada ya mazungumzo hayo, juhudi za kumpigia simu tena hazikufanikiwa, na hadi sasa hajulikani alipo.

Tukio hili tayari limeripotiwa polisi na uchunguzi unaendelea. Hata hivyo, msaada wa raia wema unahitajika katika kufanikisha kupatikana kwake. Ikiwa una taarifa yoyote kuhusu alipo Vicent au gari lake, tafadhali wasiliana na familia kupitia mawasiliano yao au toa taarifa kwa kituo cha polisi kilicho karibu.

Tuendelee kushirikiana kwa nia njema ili kuhakikisha Vicent anapatikana salama.

Msaada wako kama raia mwema kufanikisha kumpata, mawasiliano ya ndugu kwa taarifa

0719 293 117
TR
 
Back
Top Bottom