Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Simbajr kwa mfumo wa kimahakama tuliojiwekea si vyema adminstrators tukazungumzia maamuzi ya judicial commitees,nikuhakikishie haki ilitendeka.
Malinzi kiuhakila kabisa haki haikutendeka ktk suala la kumfungia Ndumbaro, naamini hata wewe unafahamu hilo, au wewe na kamati yako mkiambiwa Ndumbaro kosa lake ni nini? Naamini hamtakuwa na jibu la kisheria kwa sbb yeye aliteuliwa na vilabu kama MWANASHERIA na siyo mjumbe wa bodi ya ligi, kwa maana hiyo alikuwa pale kusimamia maslahi ya waliomteua( vilabu) na siyo bodi ya ligi.
Kamati yenu ilikuwa na uharaka gani wa kutosubiri Ndumbaro arudi safari yake ili aweze kujibu hoja zenu ili km ni adhabu basi itolewe baada ya kumsikiliza na pia alishatoa taarifa akiambatanisha na tiket ya safari husika, ndio maana familia ya wapenda soka tunaamini kuna njama za kuficha udhaifu wenu ktk uongozi na tuhuma zingine za ubadhirifu ktk shirikisho.
2.Pia kuna suala la Mwenyekiti wa matawi ya Simba Tmk kuzuiwa kuingia taifa kuangalia soka na Wilfred Kidau kwa maagizo yako na baadae kumpakazia kesi ya kumtusi kidau, kisa ni kuwa huyo Mkiti amesikika kny vituo vya radio akikupinga kutokana na tabia yako uliyoionesha ya kibabe, ebu tupe ufafanuzi wa haya masuala mawili. Kiukweli ule uwanja siyo wa TFF, pia mtu ambaye ana kitambilisho kinachotambuliwa na wadau wote ikiwemo TFF kwanini azuiwe kuingia taifa, hapo ndio mnapotuhumiwa kuwafunga watu midomo ili wasiseme mabaya yenu, ila kumbuka anaekusifu bila kukueleza na mabaya yako hakutakii mema na ndio mbaya kwako.
3. Msipojibu hoja zinazotolewa na familia ya wapenda soka basi tunaamini mtakuja kutoka kwa aibu hapo TFF HQ kwa kutofanya lolote ktk kuendeleza soka, kwani mpaka hivi sasa unashindwa kuendeleza yaliyofanywa na mtangulizi wako.
Hautakiw ufananishwe na mkiti wa zamani (FAT) sasa TFF Ndolanga.
FAMILIA YA SOKA TUNAAMINI NA TUNAHITAJI UFAFANUZI WA KINA KTK HOJA ZINAZOTOLEWA NA WADAU WA KANDANDA KUTOKA KWENU TFF, SIYO UBABE NA VIFUNGO VISIVYO NA HOJA.
NB: PIA MWAMBIE KIDAU SIKU AKIMZUIA MKITI WA MATAWI YA TMK ASIINGIE TAIFA HATATOKA SALAMA HUO NDIO UKWELI NA HATUITAJI KUBURUZWA.
AHSANTE!
marimba hoja za msingi wakati wote zinajibiwa,katu huwa siogopi kujibu hoja.Nilikwishasema judicial bodies zikishatoa ruling that's it huwa hatuwezi kuingilia.Right of admission mpirani ni WA match organizer
Kifungo cha miaka saba ni kidogo sana kwa mtu kama Ndumbaro anayeleta uchochezi na maasi katika mpira wa Tanzania. Ningefurahi kama angefungiwa 'maisha'.
Du....ulitaka apewe adhabu km ya bin hamman wa qatar..?
Malinzi ia a disgrace to our soccer.....Namuomba Mungu amrudishe Tenga
MWANGUKU amanyise ninakuomba ufuatilie kwa karibu programu zetu za vijana,kwa mfano fuatilia:TFF hii ya kwako mkuu hamna kitu kama FAT tu enzi hizo sioni haja ya wewe kukaimu shughuli karibu zote kwanini most of the time wewe ndo unakua msemaji stay as a president mambo ya mipasho tupa kulee
Hamna kitu hapo, kiini macho tu hicho
Jamal Malinzi nasikia mashindano ya VIJANA ya TIMU B za vilabu hayatakuwepo mwaka baada ya alikua akisaidia na si kudhamini kampuni ya SSB kupitia UHAI na kuitwa UHAI CUP kujitoa....hii unaizungumziaje ukizingatia ulikuwa ukitambulisha kama muumini wa SOKA la VIJANA inakuaje tunakosa UDHAMINI wa hayo MASHINDANO?...je tutaunda timu bora ya taifa kwa mtindo huu?...TFF mlipotangaza kuwa mnataka kuwa wenyeji wa mashindano ya VIJANA africa mlikua mnajua hao vijana pakuwapata...
Achana na Malinzi, yeye anajali maslahi yake tu si mpira as such, hata akitoa povu kuwa anataka kuendeleza mpira wa vijana. Ndiyo hao hao wakina James Rugemalila, utapeli tu
Jamal Malinzi nasikia mashindano ya VIJANA ya TIMU B za vilabu hayatakuwepo mwaka baada ya alikua akisaidia na si kudhamini kampuni ya SSB kupitia UHAI na kuitwa UHAI CUP kujitoa....hii unaizungumziaje ukizingatia ulikuwa ukitambulisha kama muumini wa SOKA la VIJANA inakuaje tunakosa UDHAMINI wa hayo MASHINDANO?...je tutaunda timu bora ya taifa kwa mtindo huu?...TFF mlipotangaza kuwa mnataka kuwa wenyeji wa mashindano ya VIJANA africa mlikua mnajua hao vijana pakuwapata...