Maswali na ushauri kwa Malinzi

Maswali na ushauri kwa Malinzi

The Boss hakuna makato yanapelekwa kwenye vyama vya makocha wala waamuzi.TFF ndiye msimamizi wa mpira nchini na ndiyo inaamua kipi kiende wapi kwa faida ya mpira wetu.

labda utuwekee hapa hayo makato tuyajadili
sababu hiko kitu kina discourage watu kuanzisha team

ikipatikana milioni 100 klabu inaambulia chini ya milioni 40
hebu tuwekee hapa jedwali la makato
 
ikizu kamwe siwezi kuagiza jambo kama hilo.

Mheshimiwa Jamal Malinzi tungependa kujua kuhusu ule mchakato wa jezi mpya za Taifa Stars. Vipi, mmefikia wapi hadi sasa?

maana mlitangaza ya kuwa mtawajulisha watanzania mapema tu.
 
Last edited by a moderator:
RAIS asikia tarehe 31/01/2015 unakutana na wenye viti wa mikoa DODOMA kulikoni?
mbona wenye viti wa vyama shiliki umewaacha kwenye kikao hicho?
 
inaweza kutokea ligi ikaisha bila kubadili badili ratiba ya ligi kuu au ligi daraja lakwanza?
,mnaviumiza vilabu vidogo wanaviendesha kwa shida sana fedha zenyewe wanachangishana halafu nyie mnakaa Dar na kubadili ratiba ovyo ovyo .
 
labda utuwekee hapa hayo makato tuyajadili
sababu hiko kitu kina discourage watu kuanzisha team

ikipatikana milioni 100 klabu inaambulia chini ya milioni 40
hebu tuwekee hapa jedwali la makato

The Boss kwa hesabu za haraka haraka tuseme mbeya city vs prisons zimepatika sh mia moja:
Itakatwa VAT 18%,itakatwa uwanja 15%,zitakatwa gharama za mchezo kama ulinzi,tkt nk 8%,kisha zitakazobaki vitagawana vilabu,TFF na bodi ya ligi.
 
Last edited by a moderator:
Mheshimiwa Jamal Malinzi tungependa kujua kuhusu ule mchakato wa jezi mpya za Taifa Stars. Vipi, mmefikia wapi hadi sasa?

maana mlitangaza ya kuwa mtawajulisha watanzania mapema tu.

Jezi imepatikana washindi watakabidhiwa zawadi zao muda si mrefu na tukijaliwa tutazindua jezi mpya muda si mrefu.
 
The Boss kwa hesabu za haraka haraka tuseme mbeya city vs prisons zimepatika sh mia moja:
Itakatwa VAT 18%,itakatwa uwanja 15%,zitakatwa gharama za mchezo kama ulinzi,tkt nk 8%,kisha zitakazobaki vitagawana vilabu,TFF na bodi ya ligi.
Ile 5%...kutoka ktk tiketi kwa ajiri ya soka la vijana...vipi?
 
Last edited by a moderator:
The Boss kwa hesabu za haraka haraka tuseme mbeya city vs prisons zimepatika sh mia moja:
Itakatwa VAT 18%,itakatwa uwanja 15%,zitakatwa gharama za mchezo kama ulinzi,tkt nk 8%,kisha zitakazobaki vitagawana vilabu,TFF na bodi ya ligi.

Mkuu samahani naomba hapa useme kwa mfano huo
TFF itapata ngapi na bodi ya ligi itapata ngapi
na sheria ni zipi zinazoongoza hayo?
kuna sheria ya FIFA inayo agiza hivyo?

na timu kama Azam kwenye uwanja wake inakuaje makato?

halafu alisemea uwanja upewe asilimia 15 na sio fixed amount mfano milioni 2 ni nani?
uwanja wa taifa unapata fixed au asilimia?
 
rais Jamali Malinzi nakuuliza: kama sikosei tff mliagiza timi za jeshi kwenye ligi iwe moja kwa kila idara kwa mfano polisi wametangaza polisi morogoro sasa huko daraja la kwanza kunafuja ya kupanda daraja.

sasa hatujui hilo agizo ni kweli au vipi
 
hili la timu za majeshi linafanyiwa kazi lakini ukumbuke vilabu vya jeshi vinamilikiwa na vikosi vyao na si mkuu wa majeshi
 
Bwana Malinzi ahsante kwa kuchukua muda wako kujibu maswali yetu.
Nina swali au maswali kuhusiana na uwanja wa nyamagana mwanza
1. Uwanja kwa sasa unawekwa nyasi bandia, niliona sehemu kwamba utajengwa majukwaa na kuwekewa taa, je hii ni kweli kwamba utajengwa majukwaa na kufungwa taa?
2. Yakijengwa majukwaa utakuwa na capacity ya kuchukua watu wangapi?
3. Hela zilizotolewa na fifa pamoja na jiji la mwanza zinatosha kufanya kazi yote hii?
4. Vipi kuhusu parking maana pale ni katikati ya mji na hakuna parking wala eneo la kutosha kujenga parking, mmejiandaaje kwa hilo?
5.kazi yote hiyo ikifanyika utaisha kujengwa lini ?

Ni hayo tu, kama unaweza kupost picha ya namna uwanja utakavyokuwa ukiisha itakuwa nzuri zaidi. Ahsante
 
Mkuu Jamal Malinzi hapa unatupa picha gani sie Mashabiki wa Simba na Club nyingine..
1.Rais wa T.F.F - Yanga
2.Katibu mkuu - Yanga
3.Ofisa habari - Yanga
4.M/Kiti kamati ya Sheria - Yanga
4.M/Kiti kamati ya Nidhamu - Yanga
5.M/Kiti kamati ya Rufaa - Yanga
6.M/Kiti kamati ya. Maadili - Yanga

Saa sijajua Team nyingine hakuna viongozi au ni Siasa za zako za Uyanga!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa mpira hapa Nchini Tanzania.
nilikwambia kwenye ushauri wangu na maswali kwako hatimae yametimia.
KWANZA
Kuhusu suala la kubadilisha waamuzi wa mechi za TOTO ukakanusha sijui na la mechi ya jana ya TOTO na GEITA utalikanusha? aibu aibu sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kwako kama mkuu wa mpira jitafakari kwa hilo.

PILI
Kituko kingine ni hiki kilichotokea kwenye kamati yako ya utendaji ni juu ya uuandaji wa kamati ya kuwa inashugulika na adhabu hili umelitoa wapi mbona kwenye katiba halipoooooooo jamani huna washauri au husomi katiba ya tff ni aibu aibu na shidaaa hao watu watamuhukumu nani na kwa misingi ipi? na hizo kamati zako za kutoa haki zitafanya kazi gani ikumbukwe fifa masuala yaote yanayohusu adhabu kuna kamati huru zilizojaa wanataaluma wewe kumchagua kalia na yahaya wawe mahakimu hilo umelitoa wapi? kumbuka utakuwa RAIS bogasi kuliko wate waliowahi kuongoza soka la bongo.

TATU
INAUMA sana kusikia nawe unajihusisha na mpango mchafu wa kuhakikisha toto anaingia ligi kuu RAIS jitafakali wapi ulipoanguka na kama hujui nambie niendelee kukusaidia kwa ushauri, Timu ya TOTO mechi 7 zote ilizocheza zimetokea vurugu au mpira kutoisha umewapa point ni aibu
 
MALINZI RAIS WA TFF
ulipo ingia madarakani watu wa kawaida walikuwa na wewe ila sasa imani hiyo imeanza kutoweka pole sana
AIBUUUUUUUU.

.Rais wa T.F.F - Yanga
2.Katibu mkuu - Yanga
3.Ofisa habari - Yanga
4.M/Kiti kamati ya Sheria - Yanga
4.M/Kiti kamati ya Nidhamu - Yanga
5.M/Kiti kamati ya Rufaa - Yanga
6.M/Kiti kamati ya. Maadili - Yanga
 
NIMESAHAU NA WASHAURI WKO WOTE YANGA
MATANDIKA
AYUBU NYENZI
RUTHA
 
Bwana Malinzi ahsante kwa kuchukua muda wako kujibu maswali yetu.
Nina swali au maswali kuhusiana na uwanja wa nyamagana mwanza
1. Uwanja kwa sasa unawekwa nyasi bandia, niliona sehemu kwamba utajengwa majukwaa na kuwekewa taa, je hii ni kweli kwamba utajengwa majukwaa na kufungwa taa?
2. Yakijengwa majukwaa utakuwa na capacity ya kuchukua watu wangapi?
3. Hela zilizotolewa na fifa pamoja na jiji la mwanza zinatosha kufanya kazi yote hii?
4. Vipi kuhusu parking maana pale ni katikati ya mji na hakuna parking wala eneo la kutosha kujenga parking, mmejiandaaje kwa hilo?
5.kazi yote hiyo ikifanyika utaisha kujengwa lini ?

Ni hayo tu, kama unaweza kupost picha ya namna uwanja utakavyokuwa ukiisha itakuwa nzuri zaidi. Ahsante

Ngokongosha uwanja wa Nyamagana ni mali ya manispaa ya Mwanza.Wao ndio wenye hiari na mamlaka ya kuuendeleza.TFF na FIFA kwa kushirikiana na mamlaka ya ya jiji la Mwanza tunajenga artificial turf baada tya hapo developments nyingine (kama zitakuwepo) zitakuwa ni juu ya manispaa yenyewe kuamua na kutekeleza.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom