mama D
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 19,981
- 35,581
Haya maswali binafsi huwa nayachukia sana japo kweli nimeolewa na nina watoto. Ni maswali too personal kumuuliza mtu mzima mwenye akili zake maamuzi yake. Ila bahati mbaya ni maswali ambayo watu wengi huwa wanapenda kuuliza bila hata kuwaza hisia za wale wanaowauliza.
Tena heri haya maswali yatoke kwa mzazi au mtu wa karibu kuliko ilivyo kawaida kwa sasa.
Watu tujue kuwa single au kuwa kwenye mahusiano ni hali tuu kama ilivyo kuwa na kitu flani au kukosa kitu kingine kwenye maisha
Mtu anaweza kuwa single hajawa tayari kuingia kwenye jukumu la ndoa, sio sababu amekosa mtu wa kuoana nae kama wengi wanavyodhani
Kuna wakati mtu anakua single lakini anatamani sana kuwa ndani ya mahusiano ila anashindwa sababu hajampata mwenye sifa anazotaka
Wakati mwingine mtu yuko single sababu hana uwezo wa kuwa na mahusiano labda ana mapungu aliyozaliwa nayonayo
Na pia mtu anaweza kuwa single sababu alishapitia mahusiano yakamvuruga na kumpa maumivu makubwa sana, kwa hiyo kwake kuwa peke yake ndio amani
Ndoa na familia ni jambo la heri kwa wanadamu lakini pia sio amri useme lazima kila mtu aoe/aolewe; na Kuwa ndani ya ndoa au kuwa na watoto sio ujanja na kukosa iwe ujinga! Hata kwenye vitabu vitakatifu kuna watu ambao hawakuwahi kuoa/kuolewa, kuna watu walioolewa/walioowa wasipate watoto, na wapo watu walioowa/kuolewa katika umri mkubwa pia.
Yote juu ya yote, mipango ya Mungu ni sahihi na mawazo yake ni mawazo sahihi kwetu.
Hawa watarajiwa hapa wanatukumbusha kumshukuru Mungu kwa maisha tuliyo nayo, kumwomba Mungu afanye kwa wakati wake