inamankusweke
JF-Expert Member
- Apr 24, 2014
- 20,344
- 21,967
Habari za namna hiyo za Kenya huzijui,infact habari za ajabu Kama hizo Kenya zilianza kitambo tukajua yataishia hukohukoTanzania hii watu wanajinyonga kisa madeni. Mtu anaua watoto wake kisa ugumu wa maisha. Inaweza kuwa kweli
Na wamewaorodhesha wote au!?...maisha Bora hupimwa kwa upatikanaji wa mahitaji muhimu ya maisha,maji,afya,chakula,elimu,uchukuzi...unatembea kilomita ngapi kupata hivyo!? Vinapatkana kwa kiasi gani? Nkinamankusweke naomba ufahamu wanaposema maisha bora wanachukuwa wastani wa walala hoi na wastani wa wenye maisha bora na furaha wanajulisha na kutafuta wastani.
Usijifanye hulijui hili
Offcourse unaichukia sana Kenya. Ingekuwa huichukii usingekuwa unaiponda na kuitajataja Kenya tu, wakati orodha hiyo hapo ina majina ya mataifa mengine kumi ya kiafrika. Tuna deni lenu ambalo tumekataa kulipa au ndio kunaendaje? Sio kwa msururu wa povu ambalo unamwaga humu, kisa tu eti kwasababu Kenya imetajwa.Nimesema wapi naichukia Kenya!!?..kwenye uchumi wa kibepari tarakimu za ukuaji uchumi haziakisi Hali halisi ya maisha ya mmoja mmoja,Kenya Kuna maisha magumu mzee,usione wake ya Wanamnyenyekea boss kazini,halijaja Bure hilo
Hoja zipi? Labda kama unamaanisha hojaless zako. Eti watu wanatembea miguu peku jijini Nairobi? Utanivunja mbavu! 😄 Tangia lini kigezo cha ubora wa maisha ya mtu ikawa ni weusi au weupe wake. Sisi ni waafrika kamili jombaa, 'black and proud!Wewe jibu hoja zote nilizosema!
Nairobi nimefika zaidi ya mara 20 I talk from walking on the streets, nimelala sana River Road mtaa wenye ofisi za Dar Express bus, nyuma Kuna mtaa una ofisi za Akamba bus. nimeona Kila kitu kwa macho yangu! Pale Latema Kuna Banda la kuvutia sigara Nairobi wanajifanya wazungu hakuna kuvuta fegi mitaani!
Huwa nikitumia Uwanja wa Jomo Kenyatta tunabook KLM kwenda ulaya wanatupandisha Kenya Airways wahudumu wa kenya wabaya wa sura! Weusiii!
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]Kama kawaida kichwa cha mwendawazimu kinaburuza mkia .
Rudi kwenye hoja zangu zote ukabila ukame Mungiki nk.Hoja zipi? Labda kama unamaanisha hojaless zako. Eti watu wanatembea miguu peku jijini Nairobi? Utanivunja mbavu! 😄 Tangia lini kigezo cha ubora wa maisha ya mtu ikawa ni weusi au weupe wake. Sisi ni waafrika kamili jombaa, 'black and proud!
Yaani huwa unalala River Road, Downtown Nairobi kwenye logde za bei chee? Alafu eti unategemea wachuuza ngono wasikuandame, kwenye viwanja vyao?
Hujui kwamba kuzuia uvutaji sigara hadharani huwa kuna manufaa chungu nzima kwa afya ya jamii? Hiyo sheria imekuwepo Nairobi kwa miongo karibia miwili sasa. Kama unadhani huo ni uzungu basi sina budi kusema, ashakum si matusi, kwamba wewe ni mshamba kupindukia. Tena ukikamatwa faini ni shilingi 230,000 kwa hela za madafu, tzshs.
Aah wapi, mimi huwa sifati mkumbo ndugu yangu. Sina huo muda wa kujibu kila hoja hadi zile za kipuuzi ambazo hazina mashiko. 'Time is money'. Nani atanilipa kwa muda huo ambao nitapoteza bure? Rudi kwenye mada ya uzi huu, tafuta tafsiri, vyanzo na link zingine za habari hizo. Chambua ndio uelewe kinachozungumziwa, alafu urudu ukiwa umejipanga upya.Rudi kwenye hoja zangu zote ukabila ukame Mungiki nk.
Jibu hoja za msingi acha kuonesha ujinga wako. JF Huwa tunajibu hoja kwa hoja hatutafuti hoja dhaifu tunajibu zote za baridi na za moto!
Hawa kenya si ndio Daimond platinam wa Tandale na Samatta wa Mbagala wa kwao?Kenya wenzetu wanapaa sana katika nyanja nyingi.
kama kenya na ghana nao wamo na Tanzania haipo, basi waliofanya hii ranking wanatakiwa kupimwa akili au mkojo. kuna uwezekano walivuta bange kwanza kabla ya kuweka rankings hizo.Kiwango cha furaha ambacho watu wanahisi ni motisha ya kutosha kwao kufanya kazi kuelekea kulinda na hata kuinua ustawi uliosemwa, wakati huo huo kufichua kwamba kanuni na kazi zao za kiuchumi hazina ufanisi.
Kwa maneno rahisi zaidi, nchi inapotumiwa kwa kiwango cha maisha kinachofaa, huwa wanafanya kazi kwa bidii ili kuiendeleza, na bidii hii inaakisi vyema uchumi. Hii ndiyo sababu mataifa mengi yaliyofanikiwa zaidi ulimwenguni kwa kawaida hujitahidi sana kulinda njia yao ya maisha.
Kwa bahati mbaya, Afrika imekuwa katika mchanganyiko huu. Katika historia changa ya bara hili, Waafrika wamelazimika kuvumilia baadhi ya hali mbaya zaidi za maisha duniani. Hata hivyo, katika siku za hivi majuzi bara hilo limekuwa na ufahamu wa njia bora ya maisha, na mataifa mengi katika bara hilo yamekuwa yakifanya kazi bila kuchoka ili kufikia wakati ujao unaotamanika.
View attachment 2480598Mataifa 10 ya Afrika yenye viwango vya juu vya ubora wa maisha
Business Insider Africa
Sio bange walivuta shisha!kama kenya na ghana nao wamo na Tanzania haipo, basi waliofanya hii ranking wanatakiwa kupimwa akili au mkojo. kuna uwezekano walivuta bange kwanza kabla ya kuweka rankings hizo.
Hizo nchi zingine sizijui,Kenya isiyojitosheleza hata kwa chakula naijua,ndiyo maana nimeshangaa,niichukie Kenya ili iweje!?Offcourse unaichukia sana Kenya. Ingekuwa huichukii usingekuwa unaiponda na kuitajataja Kenya tu, wakati orodha hiyo hapo ina majina ya mataifa mengine kumi ya kiafrika. Tuna deni lenu ambalo tumekataa kulipa au ndio kunaendaje? Sio kwa msururu wa povu ambalo unamwaga humu, kisa tu eti kwasababu Kenya imetajwa.
Kenya,Ghana na Tanzania hatuachani sana,hapo ndio utaona ubatili wa hii postkama kenya na ghana nao wamo na Tanzania haipo, basi waliofanya hii ranking wanatakiwa kupimwa akili au mkojo. kuna uwezekano walivuta bange kwanza kabla ya kuweka rankings hizo.
Hawa Wamisri wako wengi sana, ila hawasambai sana katika nchi za watu kama Tanzania walete mbegu zao huku kama ilivyo Raia wengine. Nasikia hawa jamaa wana uwezo mkubwa sana kiakili.Kiwango cha furaha ambacho watu wanahisi ni motisha ya kutosha kwao kufanya kazi kuelekea kulinda na hata kuinua ustawi uliosemwa, wakati huo huo kufichua kwamba kanuni na kazi zao za kiuchumi hazina ufanisi.
Kwa maneno rahisi zaidi, nchi inapotumiwa kwa kiwango cha maisha kinachofaa, huwa wanafanya kazi kwa bidii ili kuiendeleza, na bidii hii inaakisi vyema uchumi. Hii ndiyo sababu mataifa mengi yaliyofanikiwa zaidi ulimwenguni kwa kawaida hujitahidi sana kulinda njia yao ya maisha.
Kwa bahati mbaya, Afrika imekuwa katika mchanganyiko huu. Katika historia changa ya bara hili, Waafrika wamelazimika kuvumilia baadhi ya hali mbaya zaidi za maisha duniani. Hata hivyo, katika siku za hivi majuzi bara hilo limekuwa na ufahamu wa njia bora ya maisha, na mataifa mengi katika bara hilo yamekuwa yakifanya kazi bila kuchoka ili kufikia wakati ujao unaotamanika.
View attachment 2480598Mataifa 10 ya Afrika yenye viwango vya juu vya ubora wa maisha
Business Insider Africa
wamisri gani ndugu unaowaongelea? hawahawa kila Salaa? kuna chochote pale wameinnovate? ni wazungu tu wamejaa pale na viwanda, hawana technolojia, hawana chochote. washukuru Mungu wapo karibu sana na ulaya na nchi za mediterenean.Hawa Wamisri wako wengi sana, ila hawasambai sana katika nchi za watu kama Tanzania walete mbegu zao huku kama ilivyo Raia wengine. Nasikia hawa jamaa wana uwezo mkubwa sana kiakili.
Tembea Kenya sista, acha majungu ya kiccm na propaganda zao. Aliyekuambia Kenya yote kuna njaa ni nani? Sehemu ambazo huwa zinakumbwa na njaa ni zile kame, ambapo kunaishi wafugaji wa kuhamahama. Eneo lenyewe kame linaanzia kule Ethiopia, S.Sudan, Somalia hadi Kenya kaskazini. Media na mashirika mengine ya Kenya huwa yanawajibika ipasavyo, kwa uzalendo, wanapoyaangazia maeneo hayo. Ili usaidizi uwafikie wananchi wenzao, wakati wa kiangazi. Hatuna utamaduni kama wenu wa kufukia vichwa mchangani.Hizo nchi zingine sizijui,Kenya isiyojitosheleza hata kwa chakula naijua,ndiyo maana nimeshangaa,niichukie Kenya ili iweje!?
haipo, wakati ndio nchi yenye matajiri wengi zaidi africa, ndio nchi yenye wasomi zaidi africa, ndio nchi yenye watafutaji zaidi africa. hii report itakuwa imeandaliwa na wakenya. sio bure.