Tembea Kenya sista, acha majungu ya kiccm na propaganda zao. Aliyekuambia Kenya yote kuna njaa ni nani? Sehemu ambazo huwa zinakumbwa na njaa ni zile kame, ambapo kunaishi wafugaji wa kuhamahama. Eneo lenyewe kame linaanzia kule Ethiopia, S.Sudan, Somalia hadi Kenya kaskazini. Media na mashirika mengine ya Kenya huwa yanawajibika ipasavyo, kwa uzalendo, wanapoyaangazia maeneo hayo. Ili usaidizi uwafikie wananchi wenzao, wakati wa kiangazi. Hatuna utamaduni kama wenu wa kufukia vichwa mchangani.
Kenya ni nchi ya pili DUNIANI kwenye uzalishaji wa chai, ya kwanza Afrika kwenye uzalishaji wa maparachichi, top 3 kwenye uzalishaji wa maziwa na kwenye makadamia pia. Hayo yote ni mazao yenye 'high returns'(faida kubwa) na ambayo yanakuzwa kwenye sehemu zenye mvua ya kutosha. Tafakari hayo.
Ikifika kwenye kilimo BIASHARA, cha umwagiliaji, hamfikii hata 10% ya mazao ya 'horticulture' kutoka Kenya ambayo huwa yanapaa kwenye ndege kila siku hadi Uropa. 'Legumes' kama french beans, mboga, matunda n.k, n.k na maua pia. Ukitaka takwimu za kudhibitisha ninayo yazungumzia nitakupa.