Mataifa ambayo ni vigumu kuyavamia kijeshi duniani

Yani wametoa sababu nyepesi sana aisee.
Mbaka nawashangaa.
Watu humu wanachukulia ubishani wa humu na uelewa wetu finyu kuwa hivyo ndivyo nchi zinapaswa kuongozwa hili ni tatizo.

Tanzania tuna mgogoro na Malawi ila hatupo tayari kuivamia Malawi si kwamba huo uwezo hatuna hapana tunao ila zile tu athari za kagera war sidhani kama kuna kiongozi atakuwa na ubavu wa kuipeleka nchi vitani kipuuzi.

Nchi zinaongozwa na washauri na wataalam wa masuala kadhaa hivyo hupima faida na hasara za maamuzi yao tena haya mataifa makubwa ambayo yapo katika vita za kushushana huwezi ipeleka nchi vitani kwa sababu za kipuuzi.

China wana mpango wa mwaka 2049 sio wa leo huu mpango, sasa fikiri taifa linawaza 2049 lifanikishe nini ndio uliingize vitani kwa sababu ya hisia na mihemko yako.

Xi yupo kwenye nafasi mbali mbali za uongozi wa China kwa zaidi ya miaka 40 sasa maana yake anaifahamu China, Taiwan na marekani kuliko sisi humu tunaotumia hisia zetu kutoa maamuzi
 
Hujaolewa maana ya 90%
Hiyo 90% haijafika.
Oktoba 7 2023 Hamas walirusha light rockets kusini mwa Israel takriban 5000,maroketi 2300 yalipenya na kuleta madhara,yaliyobaki ndio yalidunguliwa na iron dome.
Fanya hisabati 5000-2300 unapata ngapi.
Halafu tafuta percentage hapo je asilimia 90 imefikiwa!??
Turudi mfano wa Galilaya,mpaka kufikia mwezi June Hizbollah walifanya operation 689 za guided missiles kuelekea Kaskazini mwa Israel.
Katika mashambulizi yote hayo hakuna hata moja lililoweza kuzuiliwa.
Aya huo ufanisi uko wapi kaka!??
 
Hiyo Iran,Korea kaskazini alizozitolea mfano zote ziko hali ngumu kiuchumi.
Mwisho mwezi wa 8 Iran walitaka kulipiza kisasi kwa Israel kwa kumuua mgeni ndani ya nchi yao,rais wa Iran alikataa huo ulipizaji kisasi na akasema wazi IRAN UCHUMI WAKE HAUKO KATIKA AFYA YA KIVITA.
Leo hii mtu anaendekeza hisia.

Na hata ukitizama sababu za Russia kupigana na Ukraine huwezi ukafananisha sababu walizozitoa wao za China amlipue Nancy Pelosi.
Yani ni sababu mbili tofauti.
Ugomvi wa Ukraine na Russia ni wa toka kuporwa Crimea bado haujaisha,huwezi ukaifananisha na sababu yao ya kumtaka China amlipua Pelosi kisa kaenda Taiwan.
Ukizingatia Taiwan haijawa ndani ya China kama Hong Kong ilivyo ndani ya sovereign ya China.
 
Hapo Kursk hata Hitler na Mwenzie Napoleon walikomea hapo hivyo elewa hao walioingia Russia wataishia hapo woote na Sasa wamezungukwa kwa Nyuma yaani nawahurumia sana kwanza kichapo wanachopokea sio cha kawaida.
Mkuu kuna special thread na live hapa JF ya kinachoendelea huko Urusi na Ukraine, usitupange πŸ˜ƒ
 
Watu humu wanaandika matamanio zaidi.

Naamini ziara ya shoigu Iran haikuwa ya hivi hivi bila sababu za msingi hasa kipindi kile tension zilikuwa zime raise high kati ya Israel na Iran kuna kitu shoigu alishauri pia.

Yaani Russia yupo vitani huku anakuja Pelosi haya unataka kuingiza China vitani na huku Israel ana mchokoza Iran unataka Iran iingie vitani sasa hapa nani atamsupport mwenzake ? Vitu vingine tutumie akili tu ya kawaida
 
Upo sahihi
 
Unachosema kipo sahihi na wala sikupingi hata kidogo. Cha kwanza kinachoangaliwa ni athari za hatua unazotaka kuchukua kwqhiyo sikatai kwanini China alishindwa kuitungua ndege iliyombeba Pelosi (Civilian aircraft) that could be a triggering point. Ila kuhusu China kuwa na total sovereignty over Taiwan hilo sahau mkuu.
 
Mkuu hayo maswali hayana hata haja nikujibu.
Hata nikijibu paragraph itakuwa ndefu mno kwa usomaji, na nikutoe shaka hayo maswali yako hayahalalishi kwamba China anajikomba kwa west aendelee kutengeneza uchumi.

US anamchukulua China ni threat, hata hii vita ya Russia na Ukraine, China kashindwa kuwa na kauli thabiti yupo upande upi, hana maamuzi.

Hapo umeelewa, China wanakuwa treated vibaya na US na west lakini wamo tu, wana force mahusiano.

Lakini namshukuru kwa hilo.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚Mkuu unaruka ruka kama bisi tu.
Kama ingekua China yuko ill treated na Westerners na USA halafu anakaa kimya basi kila trade war angekua anafeli,angewekewa vikwazo kwa kushirikiana na mataifa yaliyowekewa vikwazo pia angeshaamuliwa juu ya Hong Kong na South China.
China kuhusu Russia alisema hatoingilia vita kati ya Ukraine na Russia ila ataendelea kuwa mshirikia na msaidizi wa Russia kiuchumi.
Ndio maana unaona licha ya NATO na EU kumpa package ya vikwazo Russia vya kiuchumi usaidizi wa China ndio umeifanya Russia isimame kiuchumi pale ilipo.Kama isingekua China Russia ingekua inapata anguko la uchumi ikiwa vitani.

Kaisome China vizuri mkuu kesha ndio urejee,hiyo China ilipozuiliwa kutumia google nayo ikapiga ban madini ya kimkakati ya utengenezaji simu na kusababisha iphone kushuka uzalishaji wake.
Kama ingekua China wanajikomba wasingekua wanarudisha mashambulizi katika trade war.
 
Sisi binadamu hatujui ya kesho yetu kaka.
Hata pale South China kila mtu alisema aaah kwasababu USA chini ya uongozi wa Trump umepeleka aircraft carriers na battleships,basi China ata surrender na atarudisha visiwa Phillipines na kuiachia njia ya South China sea.πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mwishowe kajenga kisiwa bandia cha kijeshi na ku deploy silaha nzito zilizomfanya hata USA mwenyewe arudi alipotoka.
China ni mtu ambaye anakubana kiuchumi kwanza kabla ya kukuvamia,Taiwan ilishaanza kuhujumiwa kiuchumi,hatujui ya mbeleni tusimalize maneno.
 
Acha ubishi, China inajikakamua mno na wao wajikute wanapambana na US lakini nchi nyingi za EU wanamsikiliza US.

Tech ya 5G angalia ilivyopigwa figisu, China walishatest transmitter zao Australia, Japan, UK n.k US ikaweka majungu, 5G ya China ikadoda, nadhani Russia ndiye alikubali kutumia.

Qualcomm kuja kuachia 5G nchi zote hizo zikatumia.

Binafsi kwa maoni yangu, China inajipendekeza kiaina kwa west.

Bado haijawa na uwezo totally kuingia vita ya kiuchumi na US.
 
Diplomasia ni pana sana, yanayokubaliwa leo asubuhi jioni yanaweza yakavunjwa na wahusika kutangaziana ubaya kama vile asubuhi hawakukaa meza moja. Ila jua kuwa yanayowekwa wazi kwa jamii ya kimataifa si yale wanayokubaliana katika vikao vya siri kaka. It needs a very comprehensive knowledge to understand this mkuu
 
Wewe una ushabik maandazi tu, North Korea haikushinda vile vita na laiti kama wangeshinda basi wangekuwa na eneo kubwa la ardhi kijiografia kuliko Korea Kusini na haiko hivyo.

 
Tech ya 5G angalia ilivyopigwa figisu, China walishatest transmitter zao Australia, Japan, UK n.k US ikaweka majungu, 5G ya China ikadoda, nadhani Russia ndiye alikubali kutumia
But at what cost?

Wamelazimika ili kuiridhisha Marekani tu na bado huduma zinasuasua, leo hii ukienda UK internet huduma sio nzuri tangu waachane na Huawei

Hata Marekani mwenyewe bado anatumia Huawei 5G devices kwenye mataifa mengine ambayo ana kambi za kijeshi. Na wameona mi vigumu sana kuachana na huduma ya Huawei

Mchina hauwezi kumkimbia dunia ya sasa
 
Mkuu mbishi ni wewe sio mimi.
Hao USA na EU inajulikana wanafanya juu chini kumzuia China asiwapiku kiuchumi ndio maana kila leo wanaunda vikwazo.
Hiyo athari ya kuzuia 5G ya China unajua China ali respond vipi!?
Ndio maana nikakusisitiza nenda ukatizame kwanini kila TRADE WAR CHINA ANASHINDA DHIDI YA USA NA EU!??
Usiongee kama umelewa hansons choice bro.
Kama ubavu hana kwanini anaweza kushinda mbele yao!??

Mwaka huu China imetolewa ripoti anaongoza kwa uuzaji wa EV cars kushinda hata Tesla.
Na Ulaya takataka za China hususan BYD zimejaa kuliko za wazungu.
Walipiga kelele juu ya hili USA wakatoa wito waongeze higher tarrifs juu ya gari za umeme za China ziingiapo Ulaya.
URSULA VON DER LEYEN rais wa EU alitamka wazi kuwa hatuwezi kuwa tunakinzana na China kila muda,kuna kipindi viongozi wakae chini wafanye win to win situation negotiations juu ya masuala ya kibiashara.
Ndio uliona alianza Emmanuel Macron katembelea China,akafuatia kiongozi wa Italy,akafuatia chancellor wa Germany.
Jiulize hao viongozi wakubwa walifuata nini China??

Bro usiongee kama umelewa bana zungumza facts.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…