Matajiri Wahindi na Waarabu watufundishe weusi kuhusu mirathi na mali kugawana bila ugomvi. Yasijirudie ya Mengi na Mama Lwakatare mbeleni

Matajiri Wahindi na Waarabu watufundishe weusi kuhusu mirathi na mali kugawana bila ugomvi. Yasijirudie ya Mengi na Mama Lwakatare mbeleni

FRESHMAN

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
9,137
Reaction score
34,793
Habari wadau.

Hivi wahindi na waarabu wanatumia mbinu gani ya kumaliza mirathi zao bila ugomvi na huku watoto wanazaa wengi na waarab wanaoa wake wengi.

Vifo vya mabilionea wa kitanzania wenye asili ya kihindi na kiarab ni vingi ila hatusikii wakigombea mali zao

Ila sisi weusi kila tajiri akifa tu lazima seke seke tuzisikie za kugombea mali.
Mfano mengi, mama getrude lwakatare, bilionea msuya, viki kamata na mumewe, etc etc

Ni ujanja gani wanatuzidi waarab kama ni elimu mbona shule za ukweli na vyuo vya majuu ambavyo watoto wa matajiri wahindi na waarab wanasoma hizo hizo pia watoto wa matajiri weusi ila bado wanagombea mirathi kila leo
 
Daah hao majamaa wameuteka uchumi wetu kabisa.
 
malezi yao kwa watoto wao yana changia pakubwa

huwapa watoto wao elimu ya kumjua M. Mungu na kumuogopa na kuwafundisha wagoto sheria zake sini tokea wadogo

watu wengi huwa wanakosea hapo

kwa hivyo watoto wakubwa tayari elmu ya dunia unayo na ya akhera pia wanayo

kwa hivyo likitokea tukio lakufa mzazi wake

basi tayari anajua kinacho endelea na wala hapanic kwa mali kwani huwa anajua mgao unakwenda vipi

pia wana kuwa na khofu ya kudhulumu kwani wana jua dhulma hamuachi mtu salama

kwa hivyo muhimu malezi y watoto wetu muwafunze kuwa na khofu kwa mwenyezi mungu hakuna siri nyengine
 
Siri kubwa ya wenzetu ni kuwa wawazi katika mali zao na wazazi kukubali kuachia usimamizi wa mali kwa watoto pale umri unapokwenda.

Ukichunguza wenzetu hushirikisha watoto wao kwenye biashara zao angali wadogo. Mtoto anakuwa akijua siri zote za mali zao na jinsi ya kuziendeleza. Hii inarahisisha kuhamisha usimamizi pale mzazi anapojiweka pembeni ama kufariki.

Kimbebe kipo kwetu sasa, baba ana michepuko kila kona. Mali zote anasimamia yeye tu. Mtoto hana tofauti na mfanyakazi. Hii inatengeza uchu na hamu ya kila alie kwenye familia kuja kushika madaraka pale msimamizi mkuu anapokufa.

Mali nyingi za watu weusi hupotea sababu ya usiri. Mzee anakufa hata mkewe hajui account zake za benki.
 
Sisi ubinafsi ni tatizo kubwa sana na sijui hili tumerithi kutokea kwa nani.

Binafsi katika makuzi yangu wazee wangu Baba mzazi,Baba mkubwa na Baba mdogo walunifundisha upendo na namna ya kusimamia miradi na ofisi zao.

Yaani ni kama walijua mie nitakujakuwa kiongozi wa familia maana wakubwa walikuwepo ila ndio hivyo hamuwezi kulingana mitazamo.

kifupi kwa sasa niliamua kujitenga na mambo ya kifamilia kwa sababu walinihisi najipendelea au nawabia, lakini baada ya kuona uhalisia wa mambo ni jinsi miradi ilivyoyumba na mingine kuiuza wanajuta kwa sasa na wala sina mpango wakusema tuungane tena maana majungu yatajirudia vile vile tuu,
hivyo kila mmoja apambane na hali yake.

hili ndio linatuumiza ngozi nyeusi kwa kiwango kikubwa sana.
 
Ukifuata maadili na wengine dini zinavyofundisha kuhusu mirathi hasha hamuwezi kugombania mali

Mali ni ya aliyoichuma na hilo ndio tunajua
Sisi watoto tunafundishwa kutokuwa na tamaa wala kuwaza akifa baba nani achukue nini na nani apewe nini bali huwa tunafundishwa namna ya kuzitafuta zako

Kwa hiyo mzazi anapokufa hakuna anaeshobokea mirathi bali kama ni kuendeleza biashara inaendelezwa bila khiyana wala kugombana

Mirathi inagawanya kwa sheria za dini au mila
Ila wengine wanaona mirathi ni Dili kubwa mpaka inafikia mnauwana

Jamani mkigombania mali isiyokuwa yako na hujui alihangaika Vipi itaisha upesi kwa sababu hujui namna ya kuiongeza bali kuimaliza

Baba alipofariki mali zilibaki katika familia ila hatukuliongelea sana zaidi ya kuendeleza miradi aliyoiacha

Hivi unaanzaje kugombana na ndugu yako kwa ajili ya mali tena alizoziacha mzazi?
Hapo ndio mnafeli
Unamuuwa mzazi ili mgawane mali au anakufa unadai chako kama ulikitolea jasho

Bora mfe masikini tu kwa sababu ya tamaa zenu
 
Kwa waislamu kuna fomula maalumu ya kugawana mirathi.

Wazazi (mama na baba) ikiwa wako hai wanakuwa na percent yao.

Mke au wake wanakuwa na percent yao. Watoto wa kiume na wa kike wana mgao wao.

Kwa hivyo hapo zinapigwa calculations kwa kutumia LCM halafu kila mtu anaondoka na chake.
 
Kwa waislamu kuna fomula maalumu ya kugawana mirathi.

Je sisi wa wamatumbi wa Mlingotini Bagamoyo mbona tunagombana wakati ni waislamu kwa mavazi, imani na kuisoma dini .

Hapa nadhani kama wachangiaji wengine walivyosema makuzi, kushirikishwa toka utotoni, desturi na mila walizonazo ndiyo zinaleta muendelezo wa Mali ya familia kuendelea kuwepo vizazi na vizazi kwa watanzania wenye nasaba za waarabu, wahindi na waasia.


Wamatumbi huko vijijini watoto wanashirikishwa toka wakiwa wadogo kufahamu fani za familia zao iwe ni uvuvi, ufugaji, kilimo.


Tatizo mswahili akija mjini anaacha yale mababu na mabibi waliyokuwa wanafanya kuhakikisha vizazi vyao vinaendelea na fani walizokuwa nazo kwa kuelekezwa tangu wakiwa watoto.

Wamatumbi Mjini Tukiacha ujima wetu na kuingia ktk maisha ya kisasa ya mjini sisi wamatumbi tunazuzuka na majumba, mataa, magari, taa za umeme, vyakula vya mjini na pia kutupilia mbali jinsi mfumo wa makuzi ya kuhakikisha vizazi vipya vinashirikishwa ktk maisha haya mapya ya shughuli za kiuchumi za mijini.


Matokeo yake sisi waswahili / wamatumbi tunashangaa waTanzania wenzetu wa asili za Kiarabu / Shirazi / Burushi/ Kihindi / Baniani / Gujarati /Goa n.k wakiwa na migogoro michache ya Mali za familia.
 
Je sisi wa wamatumbi wa Mlingotini Bagamoyo mbona tunagombana wakati ni waislamu kwa mavazi, imani na kuisoma dini .
Ikiwa munajua masharti ya dini kwa nini hamutafuti msajili wa mirathi mukagawana kisheria? MEngine ni ya kujitakia
 
Huwa naliwaziaga lile jumba aliloliacha marehemu Tanil Somaiya pale Coco beach (karibu na ubalozi wa Iran). Natamani serikali ilinunue ilifanye jumba la kupokelea wageni mashuhuri wa serikali. Tanil alikuwa anajenga bonge la Estate, bahati mbaya alifariki kabla hajalimaliza...
 
Back
Top Bottom