Matajiri wakubwa duniani, wanatengenezwa na nchi zao au wanajitengeneza wenyewe?

It's like this, royal family wanamiliki nchi wanaweza wakatumia hela wanavyotaka ila hawazimiliki hizo hela, Kesho Salman akifa mwanae harithi Mali zake, bado zinaendelea vile vile kuwa Mali ya royal famili. Na Baadhi ya Nchi za Gulf unakuta Royal family ni karibia nchi nzima. Mfano Qatar Royal family Ina watu kama 30,000 na Nchi nzima wapo kama 300,000, so unakuta ngumu kukuta mtu sio royal family ama ndugu yake, mke wake, mke wa mjomba etc hatoki huko, it's like nchi nzima wanajuana.

Hata hizo familia nyengine ambazo sio royal family zinakua na vyeo vikubwa (Shura) ambapo viongozi wote wa familia wanaaamua mambo ya nchi ijiendeleze vipi.

Mwisho wa siku wote wana maisha mazuri, ukijifungua unalipwa mshahara, ukiwa huna kazi unalipwa mshahara, mwanafunzi analipwa mshahara, ukiumwa Bure kutibiwa na hospitali ya nchi ikishindwa kukutibu Serikali inakupeleka nje, wana benefits kibao compare na hizo nchi zenye Mabilionea wengi.
Ni muhimu pia kuelewa mabilionea wengi inategemea zaidi pia na ukubwa wa uchumi na jinsi ulivyotawanyika. Mfano Qatar uchumi wake ni mafuta na gesi tu na unamilikiwa na Ufalme wakati uchumi wa nchi kama US na China ni wa kila kitu kuanzia nishati, kilimo, silaha, madini, teknolojia, Sanaa, kamari, pombe n.k
 
NIkiangalia Marekani, Ulaya, naona matajiri ni wengi sana ukiringanisha na sehemu zingine za dunia.

Na kama wanatengenezwa na nchi zao, kwa sisi waafrika tujifunze nini?, Na kama wanajitengeneza wao wenyewe, ni nini kifanyike?

Nipo hapa nawaza nikawekeze kwenye uchimbaji wa mafuta Iran.​
1. Uchumi wa Tanzania wa dola bilioni 94 kwa watu milioni 70 ni mdogo sana, hauwezi kuzalisha mabilionea wengi.

2. Uwezo wa manunuzi wa Watanzania bado mdogo sana, sehemu kubwa sana ya uchumi bado inaendeshwa kwa pesa za serikali ambazo huwa zinaenda kwenye mifuko ya wachache tu kupitia tenda.

3.Mabilionea wengi kwenye nchi haina faida yoyote kama hawalipi kodi sahihi au hawapo kwenye sekta za maana za uzalishaji zenye kutoa ajira za staha. Mfano Mo na Bakheresa vibarua wanalipwa 5,000 kwa siku nzima kwa hiyo hata ubilionea wao hauna maana sana.
 
Ni muhimu pia kuelewa mabilionea wengi inategemea zaidi pia na ukubwa wa uchumi na jinsi ulivyotawanyika. Mfano Qatar uchumi wake ni mafuta na gesi tu na unamilikiwa na Ufalme wakati uchumi wa nchi kama US na China ni wa kila kitu kuanzia nishati, kilimo, silaha, madini, teknolojia, Sanaa, kamari, pombe n.k
Nimetoa mfano nchi za Nordic hapo, there was a time Finland walikua na kampuni kubwa zaidi ya Simu kwa maana Nokia, walitengeneza na software kubwa zaidi ambayo inatumika kote Duniani Linux, walikua na mambo kibao, Uchumi wao ni diversified ila hawakuwa na mabilionea wengi na income inequality ni ndogo, angalia nchi zote za ukanda huo Norway, Denmark etc utaona same thing.

So issue sio aina ya Uchumi Bali sera za Serikali.

Sasa hivi china kuna kampeni kubwa sana ya kutokomeza umasikini vijijini na mikoa ambayo sio ya Pwani, kampeni hii haiendi hivi hivi inaenda sambamba na kuwaongezea Kodi wenye nacho, 20% kwa Mali ambazo zipo nje ya china na wamerudisha Kodi ya Dividends za hisa

Soon tutaanza kusikia China wanalipa wananchi wake na China inakua kama mataifa mengine yenye welfare kubwa.

Edit: kutoa mfano mwengine angalia Angola, wana mafuta kuliko taifa lolote Africa wakichuana na Nigeria na wana mafuta mengi kushinda Baadhi ya Nchi za Kiarabu, nani katajirika zaidi? Raisi wao aliopita, mwanae na watu wachache, wananchi wa kawaida wapo Lindi la umasikini. So ni sera zinasababisha hayo na si aina ya Uchumi.

Nchi kama India wana Caste system kabisa, naamini unazijua, kama nchi nzima inaamini mtu Fulani kazaliwa azoe mavi maisha yake yote, mwengine awe dobi maisha yake yote, mwengine awe tajiri maisha yake yote unategemea taifa zima kuinuka na kutokomeza umasikini?
 
Finland ina mabilionea 7, hao sio wachache kwa nchi yenye watu milioni 5 tu.
 
Finland ina mabilionea 7, hai sio wachache kwa nchi yenye watu milioni 5 tu.
Bilionea wa 4B usd ndio tajiri mkubwa zaidi mabilionea wote 7 net worth Yao ni around $17B wakiwa na GDP 336B, so roughly mabilionea wote ni kama 5% ya GDP.

For comparison mabilionea wa Usa utajiri ni zaidi ya Trilioni 9 usd na GDP kama Trilioni 30 so watu wachache wanamiliki almost Asilimia 30.

Same kwa India mabilionea wote wana zaidi ya 1 Trilioni kwenye Uchumi wa 4 Trilion.

So hao mabilionea wa Finland wangeweza kuwa na net worth kubwa, ila mifumo ya nchi kuwatoza hela kubwa imesaidia wao kutokua na ukwasi mkubwa na wananchi wa kawaida kuwa na hela nyingi,
 
Edit: kutoa mfano mwengine angalia Angola, wana mafuta kuliko taifa lolote Africa wakichuana na Nigeria na wana mafuta mengi kushinda Baadhi ya Nchi za Kiarabu, nani katajirika zaidi? Raisi wao aliopita, mwanae na watu wachache, wananchi wa kawaida wapo Lindi la umasikini. So ni sera zinasababisha hayo na si aina ya Uchumi.

Nchi kama India wana Caste system kabisa, naamini unazijua, kama nchi nzima inaamini mtu Fulani kazaliwa azoe mavi maisha yake yote, mwengine awe dobi maisha yake yote, mwengine awe tajiri maisha yake yote unategemea taifa zima kuinuka na kutokomeza umasikini?
Aina ya uchumi wa nchi inatokana na sera za uchumi, historia na mambo mengine.

Angola imepigana vita mpaka 1975 na zote Angola na Nigeria ni nchi zisizo na viwanda, zinauza zaidi malighafi na kupeleka pesa zake za kigeni nje kununua bidhaa kama ilivyo Tanzania pia.

Caste System ya India inafanana kiasi kikubwa na mfumo wa Ufalme mkuu (Absolute Monarch) wa nchi za kiarabu. India wana matatizo mengi yaliyosababisha raia wake wengi kuendelea kuwa masikini ila caste System sio factor mojawapo kubwa kihivyo.
 
Bilionea wa 4B usd ndio tajiri mkubwa zaidi mabilionea wote 7 net worth Yao ni around $17B wakiwa na GDP 336B, so roughly mabilionea wote ni kama 5% ya GDP.

For comparison mabilionea wa Usa utajiri ni zaidi ya Trilioni 9 usd na GDP kama Trilioni 30 so watu wachache wanamiliki almost Asilimia 30.

Same kwa India mabilionea wote wana zaidi ya 1 Trilioni kwenye Uchumi wa 4 Trilion.

So hao mabilionea wa Finland wangeweza kuwa na net worth kubwa, ila mifumo ya nchi kuwatoza hela kubwa imesaidia wao kutokua na ukwasi mkubwa na wananchi wa kawaida kuwa na hela nyingi,
Tatizo la income inequality (pengo la kipato) Marekani kati ya matajiri na masikini kwa siku za hivi karibuni ni kubwa sana na kwa kiasi kikubwa inachangiwa na watu kutegemea na kutumia zaidi stock market kama vile wacheza betting badala ya kutengeneza value halisi kupitia uzalishaji.

China bado mabilionea hawajamiliki sehemu kubwa ya uchumi, kwa sasa mabilionea wao wanamiliki 11% ya GDP.
 
Aina ya uchumi wa nchi inatokana na sera za uchumi, historia na mambo mengine.

Angola imepigana vita mpaka 1975 na zote Angola na Nigeria ni nchi zisizo na viwanda, zinauza zaidi malighafi na kupeleka pesa zake za kigeni nje kununua bidhaa kama ilivyo Tanzania pia.
Achana na mambo ya 1975 naongelea sasa hivi Mafuta yanaingiza hela nyingi sana Angola, wanaingiza roughly $30B toka mafuta tu, hio hela inazidi mapato yetu ya Serikali Tanzania yote combined, na wao wapo wachache, ni level za Hela wanazopata Nchi kama Oman, na ni zaidi ya Nchi za Kiarabu za Africa kama Algeria.

Sasa niambie mkuu nchi inayopiga hela nyingi kushinda hata Algeria ni ya kuwa hohe hahe kweli? Angola kama sisi tu haireflect kama oil rich countries, hio hela ya mwaka mmoja tu inatosha kuweka nchi nzima lami na ikabaki, walitakiwa na wao sasa hivi wawe level za shule na Afya Bure.
Caste System ya India inafanana kiasi kikubwa na mfumo wa Ufalme mkuu (Absolute Monarch) wa nchi za kiarabu. India wana matatizo mengi yaliyosababisha raia wake wengi kuendelea kuwa masikini ila caste System sio factor mojawapo kubwa kihivyo.
Boss una chuki zako tu na waarabu, serious ufananishe mifumo wa kifalme wa Ghuba na caste system?

Kwenye caste za India ya Chini kabisa wanaitwa Dalits, aka Untouchable, wapo zaidi ya Milioni 200 huko India, hii ni kama Apartheid ya south Africa hao watu wametengwa kabisa, shule, Afya, na huduma za kijamii hawapewi, kama akifanya kazi basi akazoe mavi nyumba za watu, jamii inawatreat kama watu waliolaaniwa, masikini, life expectancy ni miaka 40 na kitu, hebu kuwa serious kabisa niambie mfumo huu unafanana na Nchi gani ya Ghuba.
 
Back
Top Bottom