Source: MwananchiBodaboda umezitaja. Zinaua sana watu hizi.
Sasa huku kuzifanya usafiri wa kulipia ndiyo kabisaa.
Kuna vijana wengi sana wanamalizika. Hii leo nimepewa taarifa kuna mwana wa miaka kibao Upanga amefariki kwa ajali ya Bodaboda. Miezi kadhaa nyuma mwaka huu kuna cousin alifariki kwa ajali ya Bodaboda.
Waafrika tunategeana sana.watu kama nyie ndio tunawahtaji sana katika bara hili. Lakini nyie ndo kwanza hamjali,mmekimbia na kuendelea kulidharau bara hili. Rudini tuanze ukombozi sasa.
Sikuhizi I heard PF3 wameiondoa inakuja afterBodaboda umezitaja. Zinaua sana watu hizi.
Sasa huku kuzifanya usafiri wa kulipia ndiyo kabisaa.
Kuna vijana wengi sana wanamalizika. Hii leo nimepewa taarifa kuna mwana wa miaka kibao Upanga amefariki kwa ajali ya Bodaboda. Miezi kadhaa nyuma mwaka huu kuna cousin alifariki kwa ajali ya Bodaboda.
Kuna jamaa alikuwa anasema Bongo sio tu unaweza kukosa matibabu kwa kukosa pesa za kulipa upfront, bali pia hata ukifariki ndugu zako wanaweza kushindwa kuchukua maiti yako mpaka walipie kwanza.Sikuhizi I heard PF3 wameiondoa inakuja after
Hili la pili sasa hivi ni sera kabisa ya kuombea kura kwa serikali ya CCM. Mtu anasimama jukwaani kabisa anasema akichaguliwa watu hawatazuiliwa kuchukua maiti kwa kushindiwa kulipia.Kuna jamaa alikuwa anasema Bongo sio tu unaweza kukosa matibabu kwa kukosa pesa za kulipa upfront, bali pia hata ukifariki ndugu zako wanaweza kushindwa kuchukua maiti yako mpaka walipie kwanza.
Hilo la kwanza sina uhakika sana lakini nimesikia malalamiko mengi kwenye hilo la pili.
Mkuu kuna kipindi uwa unaisifia Kenya huwa nashangaa sana. Africa almost yote inafanana if you are not exposed utafikiri kuna wenzio ni bora kuliko kwako.
Acha kamba mkuu. Tiba ni ghali sana ila kwenye dharula ndani ya dakika 5 wameshafika na utapatiwa msaada wa kitaalamu haraka. Kama ni stroke au heart attack utakimbizwa hospitali huku ukihudumiwa na huko hospitali utakuta kila kitu kiko tayari ni kwenye operesheni moja kwa moja.
Ukishapona sasa ndiyo ishu ya malipo itaanza. Kama huna bima (ambayo mara nyingi kwa mtu wa kawaida unaipata kupitia kwa mwajiri wako) ndo utakiona cha mtema kuni. Usipolipa credit score yako itaharibika na hata itakubidi ujitangaze kuwa bankruptcy. Utakuwa hukopesheki na kila kitu kwako kitakuwa ghali sana. Total financial ruin; na ukizembea ndiyo mwanzo wa kuwa homeless maana hutaweza kupata mortgage. Hata kupata sehemu ya kupanga tu itakuwa kipengele sana!
Niko hapa mwaka wa nne huu. Ni mapambano hasa kama unafanya hizi kazi za kawaida mtu asikudanganye maana maisha yako juu mno. Ila mifumo yao dah mpaka mtu unajiuliza: Walianzaje? Waliwezaje? Iliwezekanaje?
Ambulance ikija ni lazima magari yote yapishe. Ukikaidi unalimwa tiketi. Dola 250 zitakutoka. Usipolipa wanafuta leseni yako. Na jela inakuita. Na ukiwa felon hutapata kazi ng'o!
Wakiona jam haipitiki na watu wameumia sana basi wanaleta mwewe (helikopita). Mwenye helikopita utamlipa baadaye lakini lengo kwanza ni kuokoa maisha ya watu.
Nyie mliowahi kwenda kuyajaribu maisha ya huko mna bahati, kwa jinsi serikali za magharibi zinavyobana uhamiaji sasa hivi, tuliopo huku tushafungiwa.Serikali ya Tanzania hata ukikutana na mfagizi wa choo hapo chooni lazima akuwekee mashauzi kujionesha yeye ana nguvu juu yako katika hicho choo. Na anaweza hata kukutoza rushwa kwa huduma ya bure.
Sasa watu wengine huwa tunayajua matatizo yatatokea wapi na tunayaepuka kabla hayajatufikia.
Mimi kuwapo Tanzania is a problem waiting to happen.
Nitakuwa frustrated, nitakipaka kwa namna ambayo mimi naona kawaida tu, halafu nitapewa kesi ya uchochezi.
Kuepuka yote, nimeona nisirudi.
Hata tukiwapa mbinu na mipango,issue ni utekelezaji,huenda kwenye hiyo hiyo mipango watu wakazipiga hela za utekelezaji wa hiyo mipango,Tulidhani diaspora mlioona ulimwengu bora unafanyaje kazi mngerudi kutusaidia kurekebisha hali ya mambo nyumbani, sasa na nyie mnatokomea huko tena!😁
Rudini wakuu mtupe mambinu na mipango mtukwamue kutoka kwenye minyonyoro ya tawala duni.
Hakuna matata, ain't no passing craze😁Mkuu fast paced life ya majuu haikufanyi ku miss life letu la kibongo la maisha ya taratibu, mwendo mdogomdogo, ku chill out muda mwingi, hakuna haraka? Nyakati nyingi tu mtu unaamka hujui hata siku, wiki au mwezi utaishije, hakuna mipango yoyote ya maana ila maisha yanaenda tu kama gari kwenye mteremko😁
Ukiangalia Ambulance Dar zinavyopambana na foleni wakati mwingine unatamani uwakamate watawala uwachape viboko.hapan
oneni hii kiaziHaurudi bongo sababu mifumo mgogoro ama sababu hauna hela?
Hapa bongo kuna watu wanatembea na escort na wanamiliki helkopta
Endelea kubeba box kaka ujipatie ridhiki yako
Juzi kwa mara ya kwanza nilivyoona kwenye mitandao wananchi wamembeba Anthony Joshua huku akigugumia maumivu nikajua ni AI, nimeamini kama alivyosema muandika uzi... hata uwe tajiri bongo ukipata matatizo nje ya nyumbani kwako( mitaani) utateseka kama watesekavyo masikini wengine.. Just imagine Anthony Joshua amebebwa mikononi utafikiri charii wa R.Sikuona ambulance wala gari lingine lolote la uokoaji!
AJ aliishia kupandishwa kwenye gari ya polisi tena siti ya mbele.
Halafu nimeona picha za wale waliopoteza maisha yao.
Mmoja alikuwa hana kichwa. Miili yao iliachwa wazi tu na hakuna hata mmoja kati ya waliokuwepo ambaye alijaribu walau kuifunika hiyo miili.
Sijui AJ ata recover kivipi kutoka kwenye trauma aliyoipata.