Matatizo ya Mzio (Allergies) Mbalimbali: Visababishi, Madhara, Kinga na Tiba

Matatizo ya Mzio (Allergies) Mbalimbali: Visababishi, Madhara, Kinga na Tiba

Mzuqa!

Hii ishu ya allergy sijui kwa kiswahili siyo ya kuchukulia mchezo mchezo for granted hasa kwenye chakula. Waswahili wengi hatujali hasa mtu akikuambia ana allergy ya chakula flan tunadhani ana ringa ama anajifanya.

Kuna watu wana allergy ya bidhaa zote za maziwa dairy products yani akila tu anaweza kufa. Mwengine ana allergy na nyama na kadhalika. Bongo mtu akikuambia ana allergy na dagaa atasemwa sana eti anaringa.

Jana mmama flan kazini karibu afe baada ya kula cheese kwa bahati mbaya. Kila siku asubuhi kabla aanze kazi upitia jikoni na kuuliza chakula gani na atengewe. Kwake ni marufuku bidhaa yoyote au chakula chochote cha maziwa. Kwa bahati mbaya alikula cheese alianguka na kutetemeka karibu afe.

Mtu yeyote akikuambia ana allergy ya kitu flan usimdharau awe mtoto wako ndugu mwanafamilia n.k hii makitu very serious mtu anaweza kupoteza maisha hivihivi kizembe.

Pia kunawengine wana allergy na pets paka na mbwa etc.

Zamani kidogo nakumbuka dogo flan Arusha ana allergy na nyama tukawa tunamtaniaga sana jamaa hana bahati.


Asante kwa andiko hili. Watu wengi huwa wanachukulia kirahisi mambo haya wakati yanaweza kugharimu uhai wa mtu

kwa kuongezea tu, Allergy ni MZIO kwa Kiswahili fasaha.

Asante
 
Wengine wana allergy na flat screen kama Behaviourist[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
62644503_144187929991050_2495070317563609088_n.jpg
 
Kuja jamaa alikauja home alisema ana aleji na dagaa nili maindi kwa sababu home ndo ilikuwa mboga pendwa .napenda dagaa kinoma
Mimi mwenyewe nnapenda sana hio kitoweo ila nikila tu siku hiohio naanza kupata vidonda mdomoni,
hua nnajitahidi kwelikweli kujizuia nisile ila nikiiona tu mate yanajaa mdomoni lazima nipige walau tonge mbili halafu balaa linaanzia hapohapo, siku hizi home wameacha kabisa kupika hio kitu.
 
Me na allergy na Mayai yaan nikiyala tu lazima nitapike na kuugua kabisa hivi humu akuna mwny dawa anisaidiee
 
Kiboko yangu ni papai. Hili tunda Mimi nikionja hata kipande kidogo kama punje ya karanga hiyo siku nitalazwa, nana allergy na hii kitu na staki hata kuigusa, nishakubali matokeo, hata nikihisi harufu ya papai tu nakuwa zaidi ya teja.
 
Nilikuwa na mzio wa nyama nyekundu kwa miaka 6 ilikuwa nikila tu nawashwa usisimuliwe, rafiki yangu mmoja akanambia ili upone hiyo kitu inakubid ukubali yatakayokutokea nikakubali. Akanambia kula nyama wala usiwaze kuwashwa, siku ya kwanza mbona niliifurahia show, nikaipiga na siku ya pili ngoma ikawa noma vile vile.

Nikaipiga mara ya tatu, bado nikawashwa vile vile, ya nne ikawa sio kivile akawa ananisisitiza kunywa maji mengi sana na nijitahidi ile kitu nisiiweke akilini kwamba ninayo. Mara zingine zilizofuata nikawa nagonga fresh tu mpaka leo.

Nilichokuja kujifunza, mara nyingi Mzio huwa unatengenezwa na akili, ukiiruhusu akili jambo fulani ndivyo litakavyokuwa na usipojizuia linazua matatizo
 
Na mimi nasumbuliwa na hii kitu bado dawa ya uhakika sijapata dawa nilizowahi tumia ni Allegex, Cetrizine, na nasal spray inatwa Avamy, nikitumia hiz dawa napata nafuu kwamiezi kama miwili hivi halafu tatizo linarudi tena.
 
Mi nilipona kwa kunywa maji mengi kila wakati hasa nikiamka tu,kupiga push up Asubuhi napoamka za kutosha,Nikivaa nguo hasa mashati mara moja tu kwa siku nabadili,Nikilala nahakikisha nafunga mdomo napumulia pua,Nakuwa na henkachief safi wakati wote.

Nimepona.
 
Dawa kubwa ya allergy ni kuepuka vichocheo vyake lasivo itabidi tu uendelee kutumia ant histamine drugs kutuliza hali hiyo.
 
Hata mimi nina tatizo kama hilo tofauti ni kua ukiacha mafua pia nakua kama nina kikohozi kikavu kilichokwama kooni ambacho kabla sjaongea huhitaji kwnz kujitayarsha kwa kukohoa kidogo.. Na muda mwng pua moja linakaa limeziba wakati siumwi mafua, nmshaenda hosptl zaid ya tano kubwakubwa lakn hamna mafanikio. Wenye kujua tiba tusaidieni jaman.
Jaribu kuchunguza kinywani tatizo hilo linasababishwa na kuota kinyama juu ya ulimi kinaotea kwenye ulimi juu.

Ukikiona hicho nitafute nitakuelekeza dawa kitapona utumie huenda ikasaidia.
 
Back
Top Bottom