Matatizo ya nchi hii chanzo ni ndugu Nyerere

Matatizo ya nchi hii chanzo ni ndugu Nyerere

Nyinyi mnamsifi sisi tunasema yeye ndiye chanzo Cha matatizo.
Ukiharibu msingi basi jengo lote huanguka.
Hatusifii tu. Nyerere alikuwa na makosa mengi tu. Kama yeye ndiyo chanzo, muda aliondooka ungetosha kujenga msingi mpya. Wewe huoni kuwa kama ukichiwa msingi mbovu halafu badala ya kurekebisha ukaendelea kujenga utakuwa wewe ndiye mwenye tatizo? Nchi nyingine za Afrika zenye matatizo chanzo ni Nyerere? Hesabu nchi ambazo zinaweza kuwa mfano wa kuonyesha kuwa Nyerere alifanya vibaya.
 
Nyerere alikufa aliacha Chuo Cha TANESCO Morogoro Mali ya serikali.
Sasa mali ya waislam, kinaitwa chuo kikuu Cha Waislam.
Kweli Nyerere alikuwa mdini..
Sema mkuu. Maana hawa viumbe kwa lawama, hawana jema hata ungewabeba mgongoni. Mfano, Wasabato walikuwa na shule zaidi ya 200 kabla ya kutaifishwa na serikali, wakatoliki na WA Anglican na Lutheran nao maelfu ya shule. Zote Nyerere akazitaifisha kwa nguvu. Babu wa hawa walalamishi wakasoma bure, leo wanamlaumu. Tuseme ukweli ndani ya nafsi,, Samia angeweza kuwanyang'anya waislam wenzake shule ili makafiri wasome tena bure ????? Acheni chuki na lawama kama watoto.
 
Jibu maswali kwanza. Wapi mlipopeleka viwanda.

Miaka 40 ya peke yenu bila Nyerere hata sasa mnakwama wapi.

Hayo ya mabaya na mazuri hayasaidii.

Wewe una mazuri gani na mabaya gani,, tueleze.
Usihangaike sana. Watanzani ndivyo tulivyo. Hii ni kawaida ya watu wavivu. Hutafuta kila sababu ili tu kuhalalisha kushindwa kwao. Hebu watoe mfano wa nchi za kiafrika ambazo zilikuwa na viongozi wazuri kuliko Nyerere na aliwaachia misingi mizuri ambayo imewasaidia na sasa wako vizuri kuliko Tanzania.
 
Jibu maswali kwanza. Wapi mlipopeleka viwanda.

Miaka 40 ya peke yenu bila Nyerere hata sasa mnakwama wapi.

Hayo ya mabaya na mazuri hayasaidii.

Wewe una mazuri gani na mabaya gani,, tueleze.
Yaliharibiwa na wale waliotengenezwa na yeye.

Misingi mibovu aliyouweka yanamfanya asiwe na sifa ya baba wa taifa.
 
Kusema kuwa hakujenga misingi mizuri ya viwanda na maliasili ni kutojua historia ya Tanzania. Mambo mengi yaliharibika baada ya yeye kuondoka. Hivi ukiachiwa urithi wa nyumba na baba yako halafu ukauza ile nyumba utasema kosa ni la baba?
Kuhusu eti hatuambiwi mabaya ya Nyerere nako ni uongo. Nyerere ana mabaya na wengi wamekuwa wanayasema. Kwa mfano ''kutikisa'' mfumo wa elimu yetu umefanya watanzania wengi kuwa vilaza na hali imekuwa mabaya zaidi sasa hivi.
Baba asipokulea vizuri hata akikuachia ghorofa ukaliuza basi yeye ndiye mwenye makosa maana alitakiwa kujenga hata kabla hajakuruthisha.

Msingi ni kitu cha muhimu mno!!!
 
Baba asipokulea vizuri hata akikuachia ghorofa ukaliuza basi yeye ndiye mwenye makosa maana alitakiwa kujenga hata kabla hajakuruthisha.

Msingi ni kitu cha muhimu mno!!!
Your current life is shaped by the things you consistently focus on.
Not your parents. Not your upbringing. If you’re still pointing fingers at them, perhaps you’re just dodging a hard look at yourself.
Kwa hisani ya Kipangaspecial
 
Hatusifii tu. Nyerere alikuwa na makosa mengi tu. Kama yeye ndiyo chanzo, muda aliondooka ungetosha kujenga msingi mpya. Wewe huoni kuwa kama ukichiwa msingi mbovu halafu badala ya kurekebisha ukaendelea kujenga utakuwa wewe ndiye mwenye tatizo? Nchi nyingine za Afrika zenye matatizo chanzo ni Nyerere? Hesabu nchi ambazo zinaweza kuwa mfano wa kuonyesha kuwa Nyerere alifanya vibaya.
Mkuu watanzania tunamkweza sana Nyerere lakini kiuhalisia jamaa alikuwa janja janja.
 
Your current life is shaped by the things you consistently focus on.
Not your parents. Not your upbringing. If you’re still pointing fingers at them, perhaps you’re just dodging a hard look at yourself.
Kwa hisani ya Kipangaspecial
Mkuu Kuna baadhi ya vitu vinaathiriwa na mfumo ulitengenezwa na watawala lakini Kuna machache mtu unaweza ukafanya mwenyewe, kwa mfano kutopata elimu bora kunatengenezwa na watawala na si mtu binafsi.
 
Founder wa haya yote yanayofanyika Leo hii ni Nyerere.
Uwoga wa watanzania umetengenezwa na Nyerere, uonevu unaotokea aliusuka Nyerere, umalaya unaotokea umeasisiwa na Nyerere, umasikini ambao umetamalaki umeasisiwa na bwana Nyerere.

Nyerere hafai kuigwa na jamii.
Nyerere aliongoza kipindi hiki 1961-1985 leo ni 2025 miaka hiyo 40 mingine tumefanya nini?. Kumlaumu marehemu ni ishara ya tatizo kubwa linalotusumbua kitaifa.
 
Watanzania tumesangangwa ana kumhusu huyu mtu.
Hafai hata kuitwa kaka wa taifa.
Ni Baba wa Taifa kwa waliokuwepo miaka hiyo ya uongozi wake wakaiona dunia halisi ipo vipi kwa kuilinganisha na Tanzania.

Watoto wadogo wa miaka ya juzi ndio wanaimba nyimbo za chuki dhidi ya Nyerere.
 
Nyerere aliongoza kipindi hiki 1961-1985 leo ni 2025 miaka hiyo 40 mingine tumefanya nini?. Kumlaumu marehemu ni ishara ya tatizo kubwa linalotusumbua kitaifa.
Nasema katengeneza misingi mibovu ambayo inawapa mianya hawa viongozi wenzake vichwa maji kutawala kwa maslahi yao.
 
Kwani inakushangaza mkuu 'steven', kwani haya ni mapya!

Kwanza nikuulize, ni nini madhumuni ya mada hii hapa kwa sasa, unajuwa?
Umaskini dawa yake ni kupambana nao. Japan walipigwa na atomic bomb mwaka 1945 hawakukaa kujisikitikia wakaingia kazini leo hii Japan ni nchi tajiri ya dunia ya kwanza.

Kina Thailand, Singapore miaka ya 60 tulikuwa nao sawa leo hii ni matajiri sana.

Singapore na Dubai wanatajirika kwa kutegemea utalii pekee, sisi tumejaliwa ardhi nzuri na kila aina ya maliasili bado vijana wadogo wanamlalamikia Nyerere!, vipi tungekuwa hatuna chochote hali ingekuwaje.
 
Nasema katengeneza misingi mibovu ambayo inawapa mianya hawa viongozi wenzake vichwa maji kutawala kwa maslahi yao.
Hakuna lolote zaidi ya kuendekeza hulka ya kimaskini ya kumtafuta mtu wa kumnyooshea kidole.

Nyerere kafa 1999 miaka 26 imepita, nini kimefanyika kuondokana na huu umaskini?.
 
Ni Baba wa Taifa kwa waliokuwepo miaka hiyo ya uongozi wake wakaiona dunia halisi ipo vipi kwa kuilinganisha na Tanzania.

Watoto wadogo wa miaka ya juzi ndio wanaimba nyimbo za chuki dhidi ya Nyerere.
Watoto wadogo wanaodanganywa mashuleni ndio wanaoimba mazuri ya Nyerere. Pia wale wazee wenye uelewa fupi kama mkia wa sungura nao wanamsifu sana lakini wale wote waliosoma enzi za utawala wake na wenye uelewa mkubwa walimwona Nyerere kama andazi.

Ukiweka Nyerere na ndazi watu wasio na uelewa wanachagua Nyerere lakini wanye uelewa watachagua andazi.
 
Amani inayobatana na hofu na umasikini ni umalaya umalaya tu.
Hata hivyo vyuo vilivyompa Nyerere shahada ya heshima vingi ni vya nje ya Afrika na walimpa Ili kutupumbaza kiakili na unafiki kama kuna vyuo vya ndani vilivyompa hiyo heshima basi walimpa kwa sababu nao ni wajinga kama wajinga wengine.

Kwa nini shuleni wanafundisha mazuri tu ya Nyerere kwa nini upande wa mabaya aliyoyatebda haufundushwi?

Nyerere ni tapeli mkubwa sana kupata kutokea hapa nchini.
Alitumia akili ya kuhakikisha tunaongea lugha moja ya kiswahili, jiulize taifa hili lingekuwa wapi hivi sasa kama angetanguliza ubinafsi wa kukosa busara ya kuunganisha tuwe kitu kimoja.

Nenda Nigeria na Cameroon uone jamii zao zinavyoukosa utaifa kwa watu kutanguliza mbele makabila yao.

Nenda Ivory Coast uone walivyopigana kwa miaka mingi mpaka Drogba na wachezaji wenzake wakapiga magoti mbele ya kamera za TV kuwasihi wanasiasa waachane na tabia za kidhalimu na kibinafsi.

Nyerere kafa miaka 26 iliyopita, haiwezekani milele yote tukaendelea kumnyooshea yeye vidole, vipi kama asingewahi kuwa rais wetu?.
 
Hakuna lolote zaidi ya kuendekeza hulka ya kimaskini ya kumtafuta mtu wa kumnyooshea kidole.

Nyerere kafa 1999 miaka 26 imepita, nini kimefanyika kuondokana na huu umaskini?.
Kitu hakijafanyika kwa sababu yeye hakuwaanda vizuri watu wa kufanya kile kinachopaswa kufanyika.
 
Ndugu nyerere ndo nani mbona hatumfahamu lbd ungesema mwl.Julius kambarage Nyerere apo ungekuwa fresh
 
Back
Top Bottom