Matatizo ya nchi hii chanzo ni ndugu Nyerere

Matatizo ya nchi hii chanzo ni ndugu Nyerere

Alitumia akili ya kuhakikisha tunaongea lugha moja ya kiswahili, jiulize taifa hili lingekuwa wapi hivi sasa kama angetanguliza ubinafsi wa kukosa busara ya kuunganisha tuwe kitu kimoja.

Nenda Nigeria na Cameroon uone jamii zao zinavyoukosa utaifa kwa watu kutanguliza mbele makabila yao.

Nenda Ivory Coast uone walivyopigana kwa miaka mingi mpaka Drogba na wachezaji wenzake wakapiga magoti mbele ya kamera za TV kuwasihi wanasiasa waachane na tabia za kidhalimu na kibinafsi.

Nyerere kafa miaka 26 iliyopita, haiwezekani milele yote tukaendelea kumnyooshea yeye vidole, vipi kama asingewahi kuwa rais wetu?.
Hii ni amani feki mkuu. Hebu tazama kinachojiri sasa hivi hapa nchini kisha uniambie.
 
Umaskini dawa yake ni kupambana nao. Japan walipigwa na atomic bomb mwaka 1945 hawakukaa kujisikitikia wakaingia kazini leo hii Japan ni nchi tajiri ya dunia ya kwanza.

Kina Thailand, Singapore miaka ya 60 tulikuwa nao sawa leo hii ni matajiri sana.

Singapore na Dubai wanatajirika kwa kutegemea utalii pekee, sisi tumejaliwa ardhi nzuri na kila aina ya maliasili bado vijana wadogo wanamlalamikia Nyerere!, vipi tungekuwa hatuna chochote hali ingekuwaje.
Sasa kwa nini unanieleza leo haya, mkuu wangu 'steven'; kwani haya ni mapya kweli; mbona siku zote humu tumekuwa tukihangaishana juu ya haya haya, mkuu wangu!

Tanzania nchi tajiri sana hii; lakini tunakuwa watu wa kulialia tuuu, hivi hivi; hadi lini?

Tungekuwa tumetulizana vizuri, sasa hivi mshale wa maendeleo ya nchi yetu ungekuwa unapanda juu kabisa kwa kasi kubwa, na umaskini ungekuwa unaporomoka haraka sana; lakini angalia tunavyozungukazunguka tu, kama kuku waliokatwa vichwa!
Sasa tunasubiri tukatwe vichwa, ili kiongozi na timu yao waendeleze wanayoyataka wao, tutake wala tusitake! Atakuja mwingine baada ya hapo, na yeye atafanya kivyake,.... Tutapata maendeleo yapi kwa njia za aina hii!
 
Kwa wkati huo watangnyika walikuwa ni wajinga (high ignorance ) wenye uelewa walikuwa ni wachache sana.
Na ndio maana tunahitaji kurekebisha katiba huwezi kumlaumu samia ama mwalimu sisi sote ni watanganyika tushirikiane kurekebisha panapo wezekana.
 
Watu wanaweza mlaumu nyerere na viongozi wengine ila kwa nchi za ukanda wa kusini mwa bara la africa yaani SADC Tanzania ni nchi ilio kimkakati likija swala la jiografia, umaskini na kushushwa thamani kwa shilingi yetu si kwa sababu ya viongozi wa mwanzo hapana.

Ila nchi kama Tanzania ikiwa na uchumi mkubwa na mfumo wake wa maisha ukawa rahisi itapelekea kuendelea kwa nchi za kusini mwa Afrika kama Malawi, Zambia, Mozambique angola na nyingine hata mpaka botswana.

Sasa ni kwa namna gani wataweza kuwafanya hawa watu wa kusini mwa afrika wawe tegemezi kwa nchi nnje ya Afrika cha kwanza ni kuzorotesha uchumi na mfumo wa kiungozi kwenye nchi zilizokuwa mbele kwenye harakati za ukombozi wa bara la Afrika

Tanzania ingeachwa na kupewa nafasi ya shilingi yake kuwa juu kama nchi ya kenya, zambia na mataifa mengine ingekuwa kichocheo cha maendeleo kusini mwa bara letu

Na njia nyingine matatizo mengi yaliundwa na hawa tunao wakimbilia kwa sasa, hatukatai kwamba hawanw uwezo ila kwa ilipo fikia hatuna budi zaidi ya kuwaomba pale tunaposhindwa na si mara moja ni mara nyingi, na kuomba huko tunawekea sera na vikwazo vinavyo wapa wao upendeleo search au soma hii google (structural adjustment programs)

Sasa kwa mtindo huu tunao ona hapa nchini kwetu sio kwamba viongozi hawatamani kubadili ila wanashindwa kuja na kuwaeleza ukweli nini wanakumbana navyo wakijaribu kujing'amua kwenye hizi sera na mipango

Ndio maana matatizo ya nchi za Afrika yanafanana wanajamii forum na kote Afrika lawama zita dondokea kwa viongozi ila siku wakisema kama burkina faso hamto amini mtafikiri ni story za kusadikika

Kikubwa mshukuru tuna hiyo amani ila ikichukuliwa nayo tukawa destabilize kama majirani mmekwisha, Ombeni Mungu amani idumu na tuilinde mengine ni juu ya uwezo wetu kwa sasa

Naomba niishie hapa karibuni kwa maswali.
 
Umaskini dawa yake ni kupambana nao.
Na tulikuwa tunapambana nao; na kukumbana na vikwazo chungu nzima; lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kumalizia mapambano hayo hapo, yalitakiwa yaendelee kufuatana na mazingira ya wakati husika.
Sisi tulibwaga mnyanga moja kwa moja, na kujisalimisha!
 
Baba asipokulea vizuri hata akikuachia ghorofa ukaliuza basi yeye ndiye mwenye makosa maana alitakiwa kujenga hata kabla hajakuruthisha.

Msingi ni kitu cha muhimu mno!!!
Watoto wanaweza kulelewa na baba mmoja baadaye mmoja anakuwa wa ovyo na mwingine wa tabia njema na mwenye mafanikio.
Mmoja mvivu, mwingine mchapakazi.
Kuna wakati hutegemea na mtu husika siyo malezi.
 
Kweli
Nyerere ni shida, Tanzania ya hovyo leo imesababishwa na yeye.
Aliukumbatia na kuupenda umasikini.
Hakuwekeza kwenye elimu hadi leo wasojua kusoma na kuandika ni zao la utawala wake.
Sheria nyingo mbovu alizibeba hadi leo zinatumika.
Kachukua Dsm kashindwa ipanga vizuri
 
Na tulikuwa tunapambana nao; na kukumbana na vikwazo chungu nzima; lakini hiyo haiwezi kuwa sababu ya kumalizia mapambano hayo hapo, yalitakiwa yaendelee kufuatana na mazingira ya wakati husika.
Sisi tulibwaga mnyanga moja kwa moja, na kujisalimisha!
Tanzania haikuwekewa vikwazo, ilijiwekea kwa kupendana na wajamaa
 
Wakati jaribio la mapinduzi lilipotokea nahisi ulikuwa embryo ama wazazi wako hakuzaliwa kabisa. Hapa Tanzania hata usome Vipi huwezi ukafundishwa jinsi Nyerere alivyokuwa mtu mbaya, pia huwezi kusikia kama alikuwa hapendwi na baadhi ya watu hapa Tanzania.

Kua uyaone maisha 😎.

Kutopendwa na baadhi ya watu ni jambo la kawaida. Yesu na Muhammad wenyewe hawapendwi na kila mtu ndo itakua Nyerere.

Kuendelea kumlaumu Nyerere kwa umasikini wenu ni kumlaumu Babu yako kwa umasikini wako. Ni ufinyu wa akili na kukwepa uwajibikaji.
 
Tanzania haikuwekewa vikwazo, ilijiwekea kwa kupendana na wajamaa
Hizo ndizo stori mnazopenda kusikia msiokuwa na vikra huru. Kwani kupendana na wajamaa ilikuwa ni dhambi?
 
Hakuachia madaraka, bali alitema bungo, famasiala nini
Alimuangushia jumba bovu Mwinyi, alikuta nchi masikini sana
Watu tulikuwa tunavaa nguo za viraka, fundi cherehani kila kona, fundi cherehani alikuwa anaheshimika kipindi kile....
Sina hakika kama umesoma vizuri uzi, uzi unasema, "Chanzo cha matatizo yetu ya sasa ni Nyerere"
So kuvaa hizo nguo unazo sema zilikua za viraka kuna uhusiano gani na matatizo ya sasa hvi? Na kwa makusudi (sina hakika kama ulikuwepo enzi hizo au umesimuliwa ) umeamua kuacha mengi alioyafanya makusudi. Iko hivi, hospital ilikua bure, hulipi hata sh unless umeamua kwenda kwenye hospitals za Roman Catholic, those times tulikua tunaziita hospital za misheni; shuleni tulikua tunapewa daftari, kalamu, vitabu na pia bure, kuanzia level za sekondari (shule zote zilikua ni boarding schools ) tulikua tunalipiwa nauli na serikali and kama safari yako sio ya likizo, kwenye train (Tazara na reli ya kati ) tulikua tunasafiri kwa nusu nauli, sharti tu upite kwa mwl wa usafiri akupatie warrant. Chuo kikuu was free of charge na kwenda kusoma nje ya nchi, serikali ilikua inaingia yenyewe mfukoni. Well, hata hizo nguo unazo ziita za viraka, ukweli zimeanza miaka ya 80, before that hakukua na hi kitu, mambo yaliharibika sana baada ya vita vya Kagera and according to him, alitaka kuachia mwingine mwaka 1980 but madhara ya vita yalikua makubwa sana, akaona aendelee mwenyewe na aliyangaza kwamba, miezi 18 ya kufunga mkanda akiwa na maana ya kubana matumizi. Enzi hizo, mashuleni tulikua tunasoma na watoto wa viongozi wa nchi hata wa wakuu wa mikoa na wilaya, sasa hvi hata mtoto wa mtendaji wa kata, hasomi shule za serikali.

Umegusia suala la tume kudanganya matokeo, hapa pia nina mashaka sana kama ulikuwepo au umesimuliwa; maeneo mengi tume ilipopita, RTD ilikua live, chuo kikuu cha Mlimani kama mfano wangu, RTD ilikua live, tume haikufanya kazi gizani.
Shinikizo kubwa la IMF na world bank ndio hasa liliongeza ugumu wa maisha Tanzania, Nyerere hakupenda sana masharti na mikataba na hao big fishes, hadi anaondoka madarakani Dola 1 was equal to Tsh 40.
 
Bila CCM imara nchi yetu itayumba. Hii ilikuwa imani ya Mwalimu akiitumia kuhalalisha taratibu zinawekwa ili CCM iendelee kutawala hata kama tuna sarakasi za vyama vingi.
Hi statement kama sikosei aliitamka mwaka 1981, miaka 11 kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanza, enzi za vita baridi kati mashariki yakiongozwa na Urusi na magharibi yakiongozwa na Marekani. Tunaweza kua na tafsiri tofauti kuhusu hiyo statement, mimi nilimtafsiri hivi, "ccm ikiyumba, nchi pia itayumba, ccm ikiwa imara, taifa pia litapoteza mwelekeo"
Watu (hasa wana ccm ) wanaomtafsiri tofauti (kama ilivoiweka wewe hapa ) wanajisahaulisha kwamba, the same mwl alitamka kwamba, "ccm sio mama yangu, ikipoteza misingi hata mimi naweza kuachana nayo" statement hi again kaitamka miaka ya 90 baada ya kina Chadema, NCCR Mageuzi, kile chama cha mzee Abdul Fundikila, nakisahau jina lake
 
hahahaha kwahiyo kila anayempinga Nyerere ni muislamu? Come down basi we mzanaki wa Rwamkoma wewe, halafu mimi nipo huku butiama nawatumbua majipu wazanaki wenzio huku
Mjusi wewe, mada na commentz zako humu huwa zinajionesha tu ni mvaa kobazi.

Huna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kupiga makelele ya kijinga huku mitandaoni fala wewe.
 
Shida ni DINI ndugu yangu. Muislam yeyote msaidie hata kupata kazi, hawezi kukushukuru hata siku 1 kwasababu wewe sio Muislam mwenzie. Fikiria Nyerere asingechukua shule za hadi za kanisa lake, Waislamu haw wangesoma wapi? Au put this way, say shule kama Tosamaganga, ile ya Dodoma, Mkwawa, nk zingekua zinamilikiwa na Waislamu halafu Nyerere Mkristo akazichukua ziwe mali ya umma, si angesomewa albadiri na masheikh wote Tanzania? Kama sio Nyerere hata kuondoa udini bongo, unadhani kuna muislam angekuja kushika urais wa nchi hi kweli? Dini inafundisha chuki kwa wengine, sio ajabu kabisa kumlaumu Nyerere kwa makosa yanayofanywa na wengine
Binafsi mimi huwa sitaki kuwa mnafiki kabisa, kwa jinsi mnavyowaona hawa watu hawafai kabisa kishika uongozi wowote wa juu hasa uraisi, hawajui wala hawana hulka ya uongozi.

Ni wabaguzi sana, kwao yeyote asiyemuumini wa dini ya kiislamu hana thamani.. sasa watu kama hawa ndio tunawapa nchi kama hii ambayo majority ya raia wake sio waislamu? Si ndio maana kila kitu ni ovyo tu.

Hawa kama ni uongozi basi waishie kwenye nafasi ya ukuu wa mkoa tu basi na tena kwenye mikoa ambayo majority ya wakazi wake ni waislamu.
 
Nyerere alikufa karibu robo karne iliyopita bado tu mnamlaumu? Na kama mmegundua ni yeye tatizo mnahitaji miaka mingapi kuyarekebisha mapungufu yake?? Mnataka miaka 100? 20+ haijawatosha kumfuta?

Kuwa mbongo shughuli kuliko shughuli yenyewe dah! Yani marais watatu wamepita bado mnamlaumu mzee wa uhuru? Kweli??
 
Magufuli angepewa miaka kama aliyoongoza Nyerere angefanya vyema zaidi labda na mkapa Hawa wengine ni utopolo.
Nyerere alifanya kazi ngumu ya kujenga misingi, anayemlalamikia leo hii kasahau ugumu wa kazi iliyomlazimu kuifanya mpaka Tanzania ikafika hapa ilipo.

Ni ukosefu wa heshima na adabu kudai hakufanya lolote kisa mtu anapitia matatizo leo hii, anasahau kuna jana na juzi ambazo zilikuwa bora kuliko leo hii.
 
EPA na ESCROW zilikuwepo miaka ya Kikwete, Nyerere hahusiki.

Jamaa waliotupiga kwenye sekta ya umeme mapesa kibao ni kuanzia miaka ya Kikwete, Nyerere alishaondoka ikulu.

Bulyanhulu Gold Mine walipewa wazungu zile dhahabu ni miaka ya Mkapa, mpaka wakamzawadia jiwe zito la dhahabu. Nyerere alishaondoka ikulu.

Kuanzia awamu ya Kikwete mpaka leo hii kila report ya mwaka inayotolewa na CAG inajaa hati chafu, hilo nalo ni kosa la Nyerere?.

Matatizo mengi ya nchi hii yamekuwepo katika awamu za kuanzia ya pili mpaka hii ya sita. Kumlaumu Nyerere ni kutokufahamu mengi ya nchi hii.
 
We mzan
Mjusi wewe, mada na commentz zako humu huwa zinajionesha tu ni mvaa kobazi.

Huna uwezo wa kufanya lolote zaidi ya kupiga makelele ya kijinga huku mitandaoni fala wewe.
aki mke wa vicent Nyerere kuwa staha na vikao vya wanaume humu
 
Binafsi mimi huwa sitaki kuwa mnafiki kabisa, kwa jinsi mnavyowaona hawa watu hawafai kabisa kishika uongozi wowote wa juu hasa uraisi, hawajui wala hawana hulka ya uongozi.

Ni wabaguzi sana, kwao yeyote asiyemuumini wa dini ya kiislamu hana thamani.. sasa watu kama hawa ndio tunawapa nchi kama hii ambayo majority ya raia wake sio waislamu? Si ndio maana kila kitu ni ovyo tu.

Hawa kama ni uongozi basi waishie kwenye nafasi ya ukuu wa mkoa tu basi na tena kwenye mikoa ambayo majority ya wakazi wake ni waislamu.
We ndiyo umejibu ujinga gani? Magufuli ndiyo mwanzilishi wa uchawa,ukabila,ujinga, upumbavu, sifa na kujipendekeza? Magufuli alikuwa mkristo na unajua awamu ya Magufuli amepoteza waislamu na mashekhe wangapi nchi hii? We umewahi kusikia padre au kiongozi wowote wa kikristo amepotezwa awamu yake? Acha upumbavu na huyo Christian supreme yako eres tonto
 
Back
Top Bottom