Wengi mlioangalia Boxing match kati ya Youtuber Paul Logan na bondia nguli Mike Tyson, mnaweza kudhani Mike Tyson ameshindwa, ila kiuhalisia Mike Tyson alipangwa kuuza match hili amfanye Paul Logan kuwa maarufu zaidi, ni mbinu za kibiashara za kumkuza Paul Logan, na tayari media nyingi za Marekani zilikwisha sema kuwa Paul Logan lazima ashinde. Lengo la pili ilikuwa ni kumuwezesha Mike Tyson kiuchumi.
Kwenye kufanya Promotion wazungu wako mbele ya muda. Achana na hawa wabongo wanatukanana insta kutafuta kiki, issues ya Tyson na Logan inaanza utotoni ambapo kuna picha ilipigwa ikionesha Tyson akin'gata shati la Logan alilovaa kipindi akiwa mtoto, katika onesho moja la Mike Tyson miaka ya 90, baadae Logan abaada ya kukua ndio akaja na promotion ya pambano na Tyson kwa ajili ya kukuza biashara huku akitumia hiyo picha ya Utotoni kama silaha kwamba anataka kulipa kisasi
Mwisho wa pambano hilo Logan baada ya kushinda kaonesha kutoa shukurani za dhati kwa mike na akimuita "Nguli wa muda wote wa Boxing", na kusema kuwa amekuwa akimtazama tangu utotoni. Mwisho logan aliinamisha kichwa kama ishara ya kutoa shukurani kwa Mike baada ya pambano.