Mateka wa kiyahudi wasipopatikana je Israel itafanya nini?? Je bado wapo hai?


Mkuu kuna watu humu hawajui hata Gaza au West Bank ni nini haswa na maisha yakoje?

Wao wanadhani pale Gaza ni kama Bongo tunavyoishi
 
Sasa sioni faida ya hamas kudai wafungwa 2700 kwa kuteka wayahudi 253 na kupelekea vita iliyoua wapalestina 30000 na kubomoa 50% ya nyumba za Gaza

Mkuu unapambana kulingana na resources ulizonazo

Toka lini uliwahi kuona watu wanaopambana na walio wakalia wakawa na hesabu sawasaw

Unajua ni wa South Africa wangapi walikufa kabla haijapata uhuru? hawakuwa na bunduki wala vifaru nk
 
Sasa hivi duniani kote Hadi marekani wanapush Palestine wapate taifa lao...acha Israel wabomoe majumba Ila Palestine wakipata taifa lao watakua wameshinda,Sasa hv Israel wanalazimisha Hilo taifa la Palestine lisiwe na jeshi
Nakuhakikishia hizo kelele za Free Palestine zitaisha mara moja baada ya uchaguzi wa Marekani. Marekani kwa sasa inajiandaa na uchaguzi mwezi November, Rais Biden anazitaka na kura za Waislamu ndio maana anaipush Israel kuingia kwenye mazungumzo ya kusitisha mapigano. Baada ya uchaguzi wa Marekani, si Trump wala Biden atakayekuwa na nia ya kuipush Israel isitishe vita. Mark my words.
 
Umeamua utumie id nyingine badala ule ya mk 254
 
Sasa kama mnajua uwamuzi wa hamas kudai uhuru ni sahihi mbona mnatulilia lia wapalestina wanateseka
Katika hao wanaoliliwa waache dhulma na uonevu kwa Wapalestina nawewe umo!?
Lau kama akina mama wangelitishika kwa machungu na mateso wanayopitia wakati wanapobeba mimba hadi kujifungua wasingepata watoto kamwe!
"Kelele za Wapalestina hazimaanishi kuwa wanajutia."
 
Adui hana sababu!
 
Kudai ukitakacho kama ni haki yako ya kweli ni jambo jema.Lakini,mbinu zinatakiwa kuwa za akili nyingi bila kuumiza watu wako.Kudai chako siyo ufunguo wa kujiumiza au kuruhusu kuumizwa zaidi ya matarajio.
Huna unaloelewa wewe.mbinu gani gani unaweza kutumia kudai uhuru wako zaidi ya vita? Toa mfano hapaa
 
Inasikitisha sana,wanatangaza kufia katika kudai haki kwa kujitoa ufahamu kufa na wasiodaiwa hiyo hakiNa

Kudai ukitakacho kama ni haki yako ya kweli ni jambo jema.Lakini,mbinu zinatakiwa kuwa za akili nyingi bila kuumiza watu wako.Kudai chako siyo ufunguo wa kujiumiza au kuruhusu kuumizwa zaidi ya matarajio.
Hongera akili kubwa
 
Aiseeee washauwawa hao na najiuliza tu waliwatekaje
Nakama walikuwepo leo wamewamalizia maana leo Israel kapiga katikati ya kundi la wa Palestine waliokuwa wakikimbilia gari la misaada 128 kawalaza na 700 majeruhi!
 
Israel iendelee kupigana mpaka wapatikane, unaweza kuta walipelekwa Iran, inabidi watandikwe mpaka waseme walipo hata kama MAJINI ndiyo yamewahifadhi nayo yapigwe mpaka wapatikane, wanatoa somo zuri kwa magaidi wa miaka ijayo kwamba usichezee moto.
 
Hii vita inapelekea Taifa huru la Wapalestina kupatikana siku si nyingi zijazo !!!
Taifa Huru la wapalestina linapatikana kwa damu ya wapalestina !!
Hilo sahau ...Kwanza Kuna dalili Gaza nayo ikaenda na maji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…