Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kama inavyojulikana kuwa mateka wa nchi za nje huwa wanaachiwa tu kwa kushtukiz kwani Hamas hawakuwaingiza kwenye mashari yao ya kusitishwa vita,
Siku mbili za mwanzo wameachiwa waisrael wengi wao wakiwa ni akinamama na watoto.Pamoja nao walitolewa mateka kikundi kutoka Thailand.Katika orodha ya siku ya tatu yupo mateka wa Urusi ambaye Hamas wanasema wamemuachia baada ya raisi Putin kuwa na ukaribu nao.
Tanzania tunaweza tukawa tumejiuliza mbona mateka wetu,Mollel hajatolewa ?
Kwa namna ambavyo Hamas wamekuwa wakiwatoa mateka kwa kuzingatia maslahi ya pande zote lazima wizara ya mambo ya nje ya Palestina ilipata taarifa jinsi ambavyo Tanzania imeonekana kupuuza maslahi yao na kushindwa kulaani wazi wazi ukatili wa Israel kiasi kwamba jeshi la polisi la Tanzania lilipiga marufuku maandamano ya kuilaani Israel.
Naamini hatimae mateka huyo waliyebaki naye baada ya mwenzake kuuliwa na mabomu ya Israel atatolewa salama lakini kumuweka wa mwisho ni salamu kwa Tanzania kutokana na kubadili siasa zake katika miaka michache iliyopita.