Siyo Siri, kwa upande wa Serikali yetu ya Tz kuna uzembe fulani ulifanyika ktk kuwanusuru mateka raia wa Tz. Tangu enzi za utawala wa awamu ya Kwanza za Mwl. Nyerere, msimamo wa Tanzania unajulikana wazi kabisa kuhusu mgogoro huu wa Israel na Palestina kwamba Tz inaunga mkono uhuru wa Wapalestina, naamini hata Wapalestina wenyewe na Hamas wanatambua msimamo huu wa Serikali yetu. Kwa kutumia msimamo huu na kwa kutumia urafiki mkubwa uliopo kati ya Serikali ya Tz na Serikali marafiki na Wapalestina/Kundi la Hamas, Serikali yetu ingeweza kuishawishi au kuwaomba Hamas kuweza kuwaachia huru au kuwatendea wema mateka raia wa Tz. Serikali ingefanya ushawishi huu kwa kuwatumia/kupitia marafiki wa Hamas kama vile Serikali ya Misri, Yemen, Iran, UAE, Qatar, n.k., kwa vyovyote vile Hamas wasingeweza kukataa ombi la Serikali ya Tz ukizingatia kwamba Tz siyo nchi ambayo ni maadui wa Wapalestina au Hamas.