Mateso ya Mdude Nyagali ndani ya kuta za Gereza la Ruanda

Na John Pambalu

Mara milango ya gereza ikafunguliwa. Askari akasisitiza acheni simu zenu na Muingie watu 4 tu. Tukaambatana na viongozi wawili wa chama wilaya ya Mbeya mjini, mimi pamoja na Kamanda Mwaipaya tukaingia ndani ya lango la Gereza.

Mwenyekiti umekuja?. Ilikuwa sauti ya Mdude aliyekuwa akichechemea na urefu wake huku akiinamia mkono wake wa kushoto. Mwenyekiti umekuja?, aliuliza kwa mara ya pili, sikumjibu kitu nikiwa mwenye moyo wenye huzuni nikimuona kamanda akichechemea kuzikabili nyavu zinazotenganisha mahabusu/wafungwa na watu wanaokwenda kuwaona.

Wamesema ninafanya biashara ya madawa ya kulevya, ninayasafirisha kutoka Pakistan. Sijui nilikuwa nasafirishaje Tanzania na Pakistan ilihali hata passport ya kusafiria sina kamanda, alisema Mdude.

Oh! Mwaipaya ni wewe kamanda, umehitimu mafunzo ya gereza. Hongera sana kamanda, naamini kuna kitu umejifunza. Moja kati ya faida kuu ya jela ni kukufanya uwe na ujasiri wa kukipigania kile unachokiamini. Najua sasa wewe ni jasiri. Alimueleza Mdude.

Makamanda wamenipiga, wananiuliza kwa nini ninaisumbua serikali? Walikuwa wamevalia mizura wamenipiga kamanda. Walinipiga nikiwa naumwa, walinitoa kwenye Zahanati ya jela nikiwa mgonjwa wakaja kunisulubu nje huku wafungwa wenzangu wakishuhudia. Wamenipiga alirudia tena akizungumza huku akiwa mwenye ujasiri na akizungumza kwa sauti ya ushupavu.

Ninachokiamini mimi, sikumkosoa Magufuli kwa kuwa nilikuwa namchukia, hapana. Wala sikumkosoa kwa sababu ya sura yake, bali kwa sababu ya uovu wa mfumo wa Serikali yake. Najua Mungu ni mkubwa ipo siku nitatoka.

Nikasogelea zaidi nyavu zinazotutenganisha. Nikamwambia Mhe. Freeman anakusalimia, akaniambia msalimie Mwamba mwambie naisubiria kwa hamu hotuba yake. Nikamwambia Mhe. Mnyika anakusalimia, akaniambia najua amewaandikia barua wenye mamlaka kuhusu madai yangu ya kuteswa gerezani, nimeambiwa. Wamekuja kuniomba radhi nikawaambia tutayamaliza nilikoyasemea.

Wakazungumza na Mwaipaya na kupeana vifungu vya biblia, nikamrudia nikamwambia kuna vitu kadhaa tumekuletea, wana wamekuchangia fedha kidogo. Akasema wapeni wanaonipikia chakula wanajua nini cha kufanya. Wamefanya kazi nzuri sana sijawahi teseka. Waambie watanzania ninawapenda

Aluta continue akatueleza akirejea ndani ya gereza akivuta mguu wake.

Tukaachana naye kulikabili Gereza la Songwe lililopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mjini mbeya wanakoshikiliwa wapiganaji wenzetu wapatao 60, kati yao wanaume 53 na wanawake 7 Gereza la Songwe. Wengi wao wakituhumiwa wa kesi za mauaji na uhujumu uchumi.

Leo tutahitimisha ziara yetu katika mahakama huku mkoani Njombe kusikiliza kesi ya mauaji inayowakabili viongozi wetu, akiwemo Mhe. George Sanga Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Njombe.

Unaweza kuchangia chochote kwa ajili ya mahitaji kwa wafungwa wenzetu kwa 0746 777 845 Voda Jina Twaha Mwaipaya

Wasalaam
John Pambalu
jpambalu@gmail.com
0676250710
Binafsi nimeumia sana kuona jinsi watu wasio staili kuteswa na kuburuzwa mahakama, wakiishi maisha ya kimateka , ilihali mtesi wao alihimiza tumtangulize Mungu mbele.
Note: MUNGU HADHIHAKIWI. rest with unpeace where you disserve.
 
Usipijiheshimu watoto hawatakuheshimu
sasa kosa la mdude utakuwa unalijua sana matusi aliyokuwa anatukana anastahili anachokipata tena ni kidogo waongeze zaidi ili akitoka asije akarudia tena
 
Binafsi nimeumia sana kuona jinsi watu wasio staili kuteswa na kuburuzwa mahakama, wakiishi maisha ya kimateka , ilihali mtesi wao alihimiza tumtangulize Mungu mbele.
Note: MUNGU HADHIHAKIWI. rest with unpeace where you disserve.
hata mdude anastahili hapo alipo kwa matusi yale kwanza hakufaa kuwa na uwezo hata wa kuongea sasa hivi
 
Maneno ya MALCOM LUMUMBA siyo msaafu, hivyo unaweza kuyapuuza kama unaona yana umbilikimo wa kifikra. Pia nashangaa sana kusema unaifahamu vizuri Congo DRC na Sudani Kusini ilhali bado fikra zako zimekaa kuabudu dola (Fanatical Worship of State Power). Lakini uko sawa, una haki zote kikatiba kufikiri unavyotaka kufikiri, wazungu husema Entitlement to Ones Opinions.

Lakini jambo moja tu ambalo mimi na wewe lazima tukubaliane kulifanya hata kama hatupendi, ni kuheshimu utawala wa sheria ambao umewekwa. Sheria ya Tanzania inasema mtu hata akimkashifu Raisi utaratibu ni kwamba apelekwe mahakamani ashitakiwe kwa hilo kosa: Kutesa, Kuua, Kuteka na kubambikizia mtu kesi ni mambo ya kishenzi (Barbaric) ambayo yanavunja utawala wa sheria na hayakubaliki.

Sasa ambacho kinanishangaza kuhusu wewe ni kutaka kutoa ushauri kwa vijana kuchunga ndimi zao ili wasiingie kwenye matatizo ilhali umefumbia macho kwamba yanayomkuta Mdude ni mambo yaliyo kinyume na Katiba. Kinachonishangaza zaidi ni wewe kushindwa kufahamu kwamba kama mamlaka zinaweza kumbambikia mtu yeyote yule kesi, nina kitazizuia hizo mamlaka kutubambikia mimi na wewe kesi ??? AU labda unahisi kwa mfumo huu wa sheria unawaonea wanaharakati tu ???

FIKIRI....
mdude kayataka mwenyewe msipoteze nguvu zenu kutetea ujingawake
 
sasa kosa la mdude utakuwa unalijua sana matusi aliyokuwa anatukana anastahili anachokipata tena ni kidogo waongeze zaidi ili akitoka asije akarudia tena
Nitakuwekea Video za Magufuli akitukana na kudharau Wanawake na kauli nyingine za fedheha
 
siyo kweli mdude hafai kutetewa ni mhuni tu acha apate alichikuwa anataka mnamhurumia wa nini acheni ajifunze
 
Mdude alikuwa anajibu mapigo ya Dikteta Uchwara na Mungu yuko upande wake ndio maana Dikteta kawa Mzoga ila Mdude bado anaongea
 
Na John Pambalu

Mara milango ya gereza ikafunguliwa. Askari akasisitiza acheni simu zenu na Muingie watu 4 tu. Tukaambatana na viongozi wawili wa chama wilaya ya Mbeya mjini, mimi pamoja na Kamanda Mwaipaya tukaingia ndani ya lango la Gereza.

Mwenyekiti umekuja?. Ilikuwa sauti ya Mdude aliyekuwa akichechemea na urefu wake huku akiinamia mkono wake wa kushoto. Mwenyekiti umekuja?, aliuliza kwa mara ya pili, sikumjibu kitu nikiwa mwenye moyo wenye huzuni nikimuona kamanda akichechemea kuzikabili nyavu zinazotenganisha mahabusu/wafungwa na watu wanaokwenda kuwaona.

Wamesema ninafanya biashara ya madawa ya kulevya, ninayasafirisha kutoka Pakistan. Sijui nilikuwa nasafirishaje Tanzania na Pakistan ilihali hata passport ya kusafiria sina kamanda, alisema Mdude.

Oh! Mwaipaya ni wewe kamanda, umehitimu mafunzo ya gereza. Hongera sana kamanda, naamini kuna kitu umejifunza. Moja kati ya faida kuu ya jela ni kukufanya uwe na ujasiri wa kukipigania kile unachokiamini. Najua sasa wewe ni jasiri. Alimueleza Mdude.

Makamanda wamenipiga, wananiuliza kwa nini ninaisumbua serikali? Walikuwa wamevalia mizura wamenipiga kamanda. Walinipiga nikiwa naumwa, walinitoa kwenye Zahanati ya jela nikiwa mgonjwa wakaja kunisulubu nje huku wafungwa wenzangu wakishuhudia. Wamenipiga alirudia tena akizungumza huku akiwa mwenye ujasiri na akizungumza kwa sauti ya ushupavu.

Ninachokiamini mimi, sikumkosoa Magufuli kwa kuwa nilikuwa namchukia, hapana. Wala sikumkosoa kwa sababu ya sura yake, bali kwa sababu ya uovu wa mfumo wa Serikali yake. Najua Mungu ni mkubwa ipo siku nitatoka.

Nikasogelea zaidi nyavu zinazotutenganisha. Nikamwambia Mhe. Freeman anakusalimia, akaniambia msalimie Mwamba mwambie naisubiria kwa hamu hotuba yake. Nikamwambia Mhe. Mnyika anakusalimia, akaniambia najua amewaandikia barua wenye mamlaka kuhusu madai yangu ya kuteswa gerezani, nimeambiwa. Wamekuja kuniomba radhi nikawaambia tutayamaliza nilikoyasemea.

Wakazungumza na Mwaipaya na kupeana vifungu vya biblia, nikamrudia nikamwambia kuna vitu kadhaa tumekuletea, wana wamekuchangia fedha kidogo. Akasema wapeni wanaonipikia chakula wanajua nini cha kufanya. Wamefanya kazi nzuri sana sijawahi teseka. Waambie watanzania ninawapenda

Aluta continue akatueleza akirejea ndani ya gereza akivuta mguu wake.

Tukaachana naye kulikabili Gereza la Songwe lililopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mjini mbeya wanakoshikiliwa wapiganaji wenzetu wapatao 60, kati yao wanaume 53 na wanawake 7 Gereza la Songwe. Wengi wao wakituhumiwa wa kesi za mauaji na uhujumu uchumi.

Leo tutahitimisha ziara yetu katika mahakama huku mkoani Njombe kusikiliza kesi ya mauaji inayowakabili viongozi wetu, akiwemo Mhe. George Sanga Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Njombe.

Unaweza kuchangia chochote kwa ajili ya mahitaji kwa wafungwa wenzetu kwa 0746 777 845 Voda Jina Twaha Mwaipaya

Wasalaam
John Pambalu
jpambalu@gmail.com
0676250710
Tatizo la mdude ilikua sio kukosoa Bali Yale matusi take ndio yanauzi Hana kauli nzuri
 
mdude kayataka mwenyewe msipoteze nguvu zenu kutetea ujingawake
Mr Malcolm lumumba,huwezi kudai haki zako, bira kwanza wewe kutimiza wajibu wako juu ya haki za wengine,hata ktk kanuni za kimaumbile,hakina kitu kinapenda kuchokozwa au kuonewa,ukikichokoza kwa maksudi,ujiandae kwa majibu usiyoyatarajia,tizama hata miti na wadudu,kuna miti ina miiba,mingine ina utomvu wa hatari kwa watu wenye tabia km za mdude,wadudu wengine wana harufu kari na yenye kukera,lkn mpk umchokoze,wadudu wengine wana sumu kali,yoote hiyo ni kijikinga dhidi ya watu wenye tabia za kichokozi km mdude,Mr Malcolm,kila tendo tunalolitenda,linamatokeo yake,
Mr malcom,tabia za watu zinamchango mkubwa ktk maendeleo ya taifa lolote lile..ili tuendelee kama taifa ni lazima tujenge nidhamu na tabia za watu wetu.taifa lenye watu wasiokuwa na nidhamu haliwezi kuendelea.huu ni ukweli ambao tunapaswa kuufahamu.ili tuendelee ni lazima tujenge tabia za watu wetu,kwenye mkondo furani wa mawazo na matendo,na jambo hili linahitaji nidhamu,
Kitu cha kwanza, kama tunataka kuendelea kama taifa,ni lazima tujenge nidhamu na raia wanaotii sheria,kwa nini taifa letu linashindwa ktk mambo mengi,ni kwa sababu hatujawajenga watu wetu kuwa na nidhamu,nidhamu huleta dira ktk taifa,hakuna malengo yoyote ambayo yatafikia km taifa na tukafanikiwa,km taifa hili watu wake hawana nidhamu,na km hawatokuwa na malengo ya pamoja,
 
Kila mchuma janga hula na wa kwao, Mdude tamaa ya tumbo lake ndio imemfikisha hapo. Alionywa mapema hakutaka kusikia, sasa mwenyekiti anakula bata na familia yake huku Mdude ananyea debe kwa ujinga wake
Azory gwanda,alphonce mawazo na wengine malizia maana unawajua,je nao mliwaonya mapema?

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Hao uliowataja hapo juu muulize mwenyekiti wenu. Mara nyingi anapotafuta kiki au huruma ya kisiasa, huwa anatuma kikosi chake cha wanywa viloba wakamdhuru mtu fulani ili baadae wahamishie unyama huo walioufanya kwa serikali. Ni nani mwenye akili timamu hayajui haya? Mwaka uliopita mwenyekiti alichezea kichapo bar baada ya kukutwa na dem wa mtu lkn baadae akaja na kelele zake kuwa serikali ilimtumia watu wasiojulikana kumdhuru. Mungu alikupa akili ili uitumie mwenyew, lkn cha kushangaza akili yako umemkabidhi mwenyekiti wako akuwekee!
 
Mie sina shida kama alitumia lugha ya kuudhi au matusi changamoto ni kesi ya madawa inaingiaje hapo?

Yaani mtu kakuibia mke unampachika murder case ni haki kweli? Kwanini asipewe kesi inayokaribiana na kosa lake mfano cybercrime ili hta mkimkaliza mahabusu nusu mwaka kama Lema it's better kuliko kesi ya madawa ambayo anakuja kuachiwa baada ya miaka 6!! Sio sawa kwa kweli tusiunge mkono hili
Haki ipo mbinguni ndugu yangu
 
Hao uliowataja hapo juu muulize mwenyekiti wenu. Mara nyingi anapotafuta kiki au huruma ya kisiasa, huwa anatuma kikosi chake cha wanywa viloba wakamdhuru mtu fulani ili baadae wahamishie unyama huo walioufanya kwa serikali. Ni nani mwenye akili timamu hayajui haya? Mwaka uliopita mwenyekiti alichezea kichapo bar baada ya kukutwa na dem wa mtu lkn baadae akaja na kelele zake kuwa serikali ilimtumia watu wasiojulikana kumdhuru. Mungu alikupa akili ili uitumie mwenyew, lkn cha kushangaza akili yako umemkabidhi mwenyekiti wako akuwekee!
mahaba walliyonayo kwa DJ mbowe hata hiyo ya kulewa akajiangusha wanakubali anavyosema aliytumiwa watu wamzuru lakini huyo jamaa mbowe ni mafia funga kazi muulizeni sumaye alichoambiwa anaonja sumu? ukitaka uenyekiti serious lazima akupoteze ndiyo hao uliowataja
 
Nimesoma hii thread huku machozi yakinilengalenga.

Hii nchi tulishafika sehemu mbaya sana yaani mtu unakosa uhakika wa kesho yako.

Tumuombe Rais Mama Samia ahakikishe huu uonevu uliosimikwa nchini mwetu anauondosha kabisa .
Tulitembelea hilo gereza kuwaona hao kina mdude na wafungwa wengine. Kimsingi, mdude ana afya njema kabisa wala hajawawahi kuteswa kama inavyoelezwa, hachechemei wala kuburuza miguu. malalamiko yake ni hayo ya kubambikiwa kesi. Kwahiyo, Huu ni uongo uliotukuka, ili kuwafanya mtoe michango. hayo machozi yanayokulenga bora ungewalilia na kuwakumbuka ndugu zako waliotangulia mbele za haki.
 
Wewe uliye mlilia jiwe inatosha
 
mahaba walliyonayo kwa DJ mbowe hata hiyo ya kulewa akajiangusha wanakubali anavyosema aliytumiwa watu wamzuru lakini huyo jamaa mbowe ni mafia funga kazi muulizeni sumaye alichoambiwa anaonja sumu? ukitaka uenyekiti serious lazima akupoteze ndiyo hao uliowataja
Jamaa ashapoteza wengi..sana sana wale waliojifanya wanamkosoa wazi wazi au kuutaka uenyekiti wake. Baadhi yao ni ben saa8, Chacha Wangwe, pia wapo waliowahi kukimbia kabla hawajamalizwa na genge lake nao ni Zito, Sumaye, Kubenea na wengine wengi tu
 
Back
Top Bottom