Mateso ya Mdude Nyagali ndani ya kuta za Gereza la Ruanda

Adhabu anayopewa ni kubwa ingawa pia alikuwa na matusi mazito kwa magufuli ,hata baba yako huwezi kumtukana vile unaonywa na unarudia ,kuna namna ya kupinga kwa hoja nzuri kama Mnyika anavyofanya lakini si kwa namna alivyokuwa akifanya ,watesi wake wamemtega na ameingia kwenye mtego wao
 
Kama alikuwa anatukana alitakiwa ahukumiwe kwa makosa hayo na kwa mujibu wa Sheria. Kubambikia watu kesi Ni unyama
 
Pole yake sana na si jambo zuri sana, ila pia huyu dogo alikosa washauri kwanamna nchi ilipokuwa na harakati zake, hakujitathmini na kugundua nyakati alizopo.

Wanasheria msaidieni kijana huyu
Kweli alikosa washauri
Na lugha alizokuwa anatumia hazikuwa na staha
Ona sasa
 
Umesahau kuwa katika dunia hii iitwayo uwanja wa fujo kila mtu ni mfungwa mtarajiwa.

Nakushauri sana ndugu yangu usikebehi mahabusu au mfungwa.
Muombe sana mungu asikupe kiburi cha kutenda hiyo dhambi.
muuza unga huyo mdude lazima apambane na sheria
 
Bwege wewe. Sasa ukitukana ndio ubambikiwe kesi ya ngada? Wangemshtaki kwa kosa hili unalomtuhumu na siyo kumbambikia. Mungu yupo. Magufuli hayupo.

 
Nimesoma hii thread huku machozi yakinilengalenga.

Hii nchi tulishafika sehemu mbaya sana yaani mtu unakosa uhakika wa kesho yako.

Tumuombe Rais Mama Samia ahakikishe huu uonevu uliosimikwa nchini mwetu anauondosha kabisa .
Mmawia

Nchi ndio inaendeshwa hivyo, lazima mkono mmoja uwe wa chuma na mwingine wa plastic! Ukitaka kuendesha nchi kwa mikono ya plastic pekee baadhi ya watu watakosa adabu na Taifa lao au na viongozi wao!
Mfano: ukosoaji wa mdude haukuwa Mbaya lkn alikuwa anachanganya na matusi kwa Kiongozi mkuu! Hata mm ningekuwa ndio Kiongozi mwenyewe lazima nikupoteze, maana unakosa adabu!
 
Ila mwendazake katesa sana watu, hivi JK alijigamba kutuletea huyu mtu. Mbona hajatuomba radhi kwa madhira tuliyoyapata sababu ya kutuletea "chuma" ???
 
Nikushukuru kwa andishi zuri na lefu,japo umeonyesha kukosa ustahimilivu,binafsi mie nimeishi Congo zaidi ya miezi 21,ninaijua Congo vzr,lkn pia kulingana na shughuri zangu nimekaa sana Nubi,sudani kusini kipindi wanapigana wao kwa wao,Mr Malcolm lumumba,ivue hiyo miwani uliyoivaa ili uweze kusoma nilichoandika na unielewe,hakuna mahari niliposhangilia ila nimeonya matumizi mabaya ya ulimi,labda huo ndio Ushenzi wangu,lkn hebu kasome hata maandiko ya vitabu vya mungu,quruani na biblia,vimeonya juu ya kutokuzitii mamlaka,lkn pia mchukue huyo mdude nyangali mpeleke rwanda akayafanye hayo anayoyafanya kama atabaki hai,tusiwatie watu ujinga kwa kuwahamasisha wafanye upumbavu,tuwape vijana wetu hekima,wajifunze kutumia ndimi zao kwa busara na hekima,kwa taarifa yako alichokuwa akikifanya huyu kijana wetu mdude ni hatari kuliko mie ninae shauri matumizi sahihi ya ulimi,hata wewe nakuona huna ustaarabu kama huyo lidude,kama ni kukosoana tukosoane kwa kutumia lugha nzuri za kuelimishana,nakuona km umestaarabika,lkn maandishi yako nayaona km yana umbirikimo wa fikra,hekima na uchaji,TUVUMILIANE TU,
 
jamani huyu kijana aliyataka mwenyewe mbona kina mbowe wanakosoa kistaarabu hao ndiyo wanafaa kuwa viongozi mdude? huyu ni kichaa kasoro hakupelekwa milembe tu acha apate alichokuwa anakitafuta na akitoka hatarudia tena maana wanaompamba wako nje anateseka pekeyake
 
mkuu nakuunga mkono asilimia miamoja 100% huyu anayekupa lawama naona hakuwahi kusoma matusi aliyokuwa anaandika mdude hamjui vizuri mdude nyagali mbona kina mbowe wana siasa za kistaarabu lakini mdude yaani alikuwa analazimisha yeye mwenyewe akamatwe yaani alikuwa anahamasisha kukamatwa kina mandela walikaa jela siyo kwa matusi kama ya mdude asifikiri kuwa mtu akityokea jela basi anakuwa rais never huyo anapata alichokuwa anatkitaka mwenyewe
 
Mdude ni kijana shupavu aliyekataa kunyamazishwa na Dikteta kipenzi cha Mazezeta.
 
Mdude ni kijana shupavu aliyekataa kunyamazishwa na Dikteta kipenzi cha Mazezeta.
wewe unamjua mdude vizuri mkuu naomba unijibu kwa staha maana wewe nakujua ni mbishi unamjua vizuri mdude na harakati zake?
 
Unataka kusema nini?
tuchukulie wewe ni mzazi una watoto kawaida siyo watoto wote wakishakuwa watapenda sera zako sasa je ndiyo wawe wanakushauri kwamatusi utawaelewaje na unamkanya bado anaendelea
 
Maneno ya MALCOM LUMUMBA siyo msaafu, hivyo unaweza kuyapuuza kama unaona yana umbilikimo wa kifikra. Pia nashangaa sana kusema unaifahamu vizuri Congo DRC na Sudani Kusini ilhali bado fikra zako zimekaa kuabudu dola (Fanatical Worship of State Power). Lakini uko sawa, una haki zote kikatiba kufikiri unavyotaka kufikiri, wazungu husema Entitlement to Ones Opinions.

Lakini jambo moja tu ambalo mimi na wewe lazima tukubaliane kulifanya hata kama hatupendi, ni kuheshimu utawala wa sheria ambao umewekwa. Sheria ya Tanzania inasema mtu hata akimkashifu Raisi utaratibu ni kwamba apelekwe mahakamani ashitakiwe kwa hilo kosa: Kutesa, Kuua, Kuteka na kubambikizia mtu kesi ni mambo ya kishenzi (Barbaric) ambayo yanavunja utawala wa sheria na hayakubaliki.

Sasa ambacho kinanishangaza kuhusu wewe ni kutaka kutoa ushauri kwa vijana kuchunga ndimi zao ili wasiingie kwenye matatizo ilhali umefumbia macho kwamba yanayomkuta Mdude ni mambo yaliyo kinyume na Katiba. Kinachonishangaza zaidi ni wewe kushindwa kufahamu kwamba kama mamlaka zinaweza kumbambikia mtu yeyote yule kesi, nina kitazizuia hizo mamlaka kutubambikia mimi na wewe kesi ??? AU labda unahisi kwa mfumo huu wa sheria unawaonea wanaharakati tu ???

FIKIRI....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…