Mateso ya Mdude Nyagali ndani ya kuta za Gereza la Ruanda

Mateso ya Mdude Nyagali ndani ya kuta za Gereza la Ruanda

Lkn pia bro tutumie lugha za busara hata tunapowakosoa watu tusiokubaliana nao,lugha ngumu na zenye ukakasi kuleta mgogoro,hata km ni ktk familia,mdude alivuka kiwango,
Unasema? Eti samahani mkuu mguu wangu umekaa chini ya mguu wako, we mwambie tu umenikanyaga
 
Pambaneni tu sisi hatuna nguvu ya kuingilia mchakato wa kimahakama.
 
Hii thread imenifanya nizidi kumchukia mwendazake kama kweli Mungu yupo basi Mwensazake ana hali mbaya sana katika moto wa jehanamu kwani hakupatana na aliowatesa
Inaumiza lkn sasa ndiyo hivyo mdogo siku zoote amekuwa ndiye wa kumalizia hasira.
 
Chadema kutoka wabunge mia hadi mbunge mmoja,bado mnajipa matumaini kuwa chama kiko imara [emoji1][emoji1][emoji1]Chadema ilikufa alipoondoka slaa.sasahivi Chadema imebaki fb na jamii foram
Corona inatesa sana.
 
Kweli Maisha yanakupa unachokitaka...mwenyekiti juzi katua kutoka Dubai mwanaharakati wake yuko nyuma ya kuta za ngome.

Bora mwenyekiti wetu Magu alikataa kwenda ulaya na marekani huko kuzulula akahaidi kukaa nasi hapa ndani mpaka kifo kinamchukua.
Bora aliye nyuma ya nondo za gereza kuliko yule aliye kwenye kuta za zege na kiza kinene
 
Kuna vitu vingine mimi sioni kama vina faida kwa mtu mmoja mmoja pia ni kutesa familia zetu tu hivi kulikuwa na haja gani ya kutukana matusi yale aliyokuwa anatukana ?

Sidhani kama kuna mtu yeyote Duniani ambae hatakubali siasa alizokuwa anaendesha huyu Mdude hata siku moja hayupo

Samia naomba afute kesi zote za kisiasa japo kuna wengine wamefanya makosa kweli, ila tuache tu tuanze upya. Sidhani kama huyu (Musa) wa sasa anaweza kubali matusi aliyokuwa anatukana huyu jamaa atukanwe yeye tena huyu mmemzoesha kumsifu na kumuabudu siku mkianza kumtukana ndo mtajua na yeye nani.

Kipimo cha uvumilivu kinapimwa kwenye maumivu na shida si raha na burudani sasa mnapa burudani jaribuni kumpa shida na tabu ndo mtaona kweli ni mvumilivu au lah .
mkuu waswahili husema mchuma janga hula na wa kwao huyu jamaa sasa hivi anasema eti alikuwa mkosoaji wa serikali hivi serikali inakosolewagwa kwa matusi mazito aliyokuwaga anatukana huyu mdude?anatukana serikali anamtukana rais kama anatukana mtotowake yaani leo anatikea kichaa mwingine kama pambalu lissu na maboya wengine wanaudanganya umma eti alikuwa mkosoaji wa serikali ? ujinga wa hali ya juu huo sasa anapata alichokuwa anakitaka yaani anastahili mateso anayoyapata huku kina pambalu wanajifanya kumtetea anaumia pekeyake huyo siasa hajui matusi siyo siasa NA BADO ANATAKIWA AKITOKA HUMO KILA MTU AMUAMKIE NA WAUWE KABISA NGUVU ZA KIUME ILI IWE KUMBUKUMBU YAKE
 
Wapumbavu woote wamejaa ngeo vichwani na usoni.lkn wenye hakika woote wana sura zao halisi.mdude nyangali anapata stahiki yake,tuache ushabiki,mdude alikuwa anautumia vibaya ndomo wake,na mdomo uliponza kichwa,wachina wana msemo mmoja,mdomo ni siraha kubwa sn ukiutumia vzr unaweza kujiokoa katkati ya jeshi kubwa la wanajeshi 1000,lkn pia mdomo ukiutumia vibaya unaweza kupoteza kichwa chako,
Huwa nakuangalia sana kila ukichangia, lakini leo hii ngoja nikushauri tu. Unaweza kujihisi wewe ni mzalendo mwenye uchungu sana na nchi kumbe umekosa maarifa, hekima, busara na uungwana. Nadhani pia huwa unaandika hivi kwasababu bado hujaiona dunia, lakini siku ukipata fursa ya kwenda sehemu zenye vita walau hata mashariki mwa Congo DRC nadhani utabadilika na kuachana na hizi tabia za kishenzi (Barbaric) ambazo sisi watanzania kwetu ni vitu vigeni sana.

Miaka ya 1990-1994 Wahutu (Interahamwe) walikuwa wanatoa kauli kama hizi kwenye vyombo vya habari na magazeti, wakiamini kabisa wanafanya usahihi kuilinda Rwanda dhidi ya mamluki wa Kitutsi ambao ni vibaraka wa mabeberu. Ikafikia hadi kipindi wakaamini kabisa kwamba kuua Watutsi ni suala la kizalendo kwasababu wale ni maadui wa nchi. Unafahamu nini kiliikuta Rwanda hasahasa Wahutu baada ya yale mauaji ya halaiki ya 1994 ???

RPF ilifanya mauaji makubwa mara mbili (mamilioni ya watu) ya Wahutu kule Congo DRC, kuliko idadi ambayo Wahutu waliuwa Watutsi kule Rwanda. Ukienda Rwanda leo hii ni nchi ambayo inaendelea kwa kasi, lakini itachukua miaka mingi na vizazi vingi sana mpaka makovu yapotee. Unafahamu tatizo la Rwanda lilikuwa ni nini haswa ??? Raia wenye tabia kama zako, The Jean Kambanda's and Jean Akayesu's type.

Mwanafalsafa Plato alishawahi kusema maneno haya "At his best, human being is noblest of all animals, separated from law and justice, he is the worst of all". Mdude katukana na kukashifu basi apelekwe mahakamani na utaraibu ufuatwe. Asibambikiziwe kesi na wala asiteswe bali aadhibiwe kama sheria inavyosema. Tulitunga sheria ili ziweze kututofautisha sisi binadamu wenye utashi dhidi ya wanyama....

Tanzania ilipofikia hapa, tusipojiangalia sana tutakuja kukaa siku na kuangalia nyuma kwa majuto na kusema laiti tungelifahamu. Hii nchi ikiingia kwenye balaa hataumia Mdude peke yake hata wewe na familia yako mnaweza kuwa wahanga........

Be vigilant my friend......
 
mkuu waswahili husema mchuma janga hula na wa kwao huyu jamaa sasa hivi anasema eti alikuwa mkosoaji wa serikali hivi serikali inakosolewagwa kwa matusi mazito aliyokuwaga anatukana huyu mdude?anatukana serikali anamtukana rais kama anatukana mtotowake yaani leo anatikea kichaa mwingine kama pambalu lissu na maboya wengine wanaudanganya umma eti alikuwa mkosoaji wa serikali ? ujinga wa hali ya juu huo sasa anapata alichokuwa anakitaka yaani anastahili mateso anayoyapata huku kina pambalu wanajifanya kumtetea anaumia pekeyake huyo siasa hajui matusi siyo siasa NA BADO ANATAKIWA AKITOKA HUMO KILA MTU AMUAMKIE NA WAUWE KABISA NGUVU ZA KIUME ILI IWE KUMBUKUMBU YAKE
Kwani wewe uliyeharibiwa uwezo wako wa uzazi ulimtukana nani?
 
Huwa nakuangalia sana kila ukichangia, lakini leo hii ngoja nikushauri tu. Unaweza kujihisi wewe ni mzalendo mwenye uchungu sana na nchi kumbe umekosa maarifa, hekima, busara na uungwana. Nadhani pia huwa unaandika hivi kwasababu bado hujaiona dunia, lakini siku ukipata fursa ya kwenda sehemu zenye vita walau hata mashariki mwa Congo DRC nadhani utabadilika na kuachana na hizi tabia za kishenzi (Barbaric) ambazo sisi watanzania kwetu ni vitu vigeni sana.

Miaka ya 1990-1994 Wahutu (Interahamwe) walikuwa wanatoa kauli kama hizi kwenye vyombo vya habari na magazeti, wakiamini kabisa wanafanya usahihi kuilinda Rwanda dhidi ya mamluki wa Kitutsi ambao ni vibaraka wa mabeberu. Ikafikia hadi kipindi wakaamini kabisa kwamba kuua Watutsi ni suala la kizalendo kwasababu wale ni maadui wa nchi. Unafahamu nini kiliikuta Rwanda hasahasa Watutsi baada ya yala mauaji ya halaiki ya 1994 ???

RPF ilifanya mauaji makubwa mara mbili (mamilioni ya watu) ya Wahutu kule Congo DRC, kuliko idadi ambayo Wahutu waliuwa Watutsi kule Rwanda. Ukienda Rwanda leo hii ni nchi ambayo inaendelea lakini itachukua miaka mingi sana mpaka makovu yapotee. Unafahamu tatizo la Rwanda lilikuwa ni nini haswa ??? Raia wenye tabia kama zako, The Jean Kambanda's and Jean Akayesu's type.

Mwanafalsafa Plato alishawahi kusema maneno haya "At his best, human being is noblest of all animals, separated from law and justice, he is the worst of all". Mdude katukana na kukashifu basi apelekwe mahakamani na utaraibu ufuatwe. Asibambikiziwe kesi na wala asiteswe bali aadhibiwe kama sheria inavyosema. Tulitunga sheria ili ziweze kututofautisha sisi binadamu wenye utashi dhidi ya wanyama....

Tanzania ilipofikia hapa, tusipojiangalia sana tutakuja kukaa siku na kuangalia nyuma kwa majuto na kusema laiti tungelifahamu. Hii nchi ikiingia kwenye balaa hataumia Mdude peke yake hata wewe na familia yako mnaweza kuwa wahanga........

Be vigilant my friend......
Aisee huu ujumbe unamgusa kila mtanzania ambaye ana tabia za kujiona kuwa yeye ndiye haki kuubwa na hii nchi.

Kwa ujumbe huu nadhani watu tutajirekebisha na kuvaa utanzania.
 
Jo
Na John Pambalu

Mara milango ya gereza ikafunguliwa. Askari akasisitiza acheni simu zenu na Muingie watu 4 tu. Tukaambatana na viongozi wawili wa chama wilaya ya Mbeya mjini, mimi pamoja na Kamanda Mwaipaya tukaingia ndani ya lango la Gereza.

Mwenyekiti umekuja?. Ilikuwa sauti ya Mdude aliyekuwa akichechemea na urefu wake huku akiinamia mkono wake wa kushoto. Mwenyekiti umekuja?, aliuliza kwa mara ya pili, sikumjibu kitu nikiwa mwenye moyo wenye huzuni nikimuona kamanda akichechemea kuzikabili nyavu zinazotenganisha mahabusu/wafungwa na watu wanaokwenda kuwaona.

Wamesema ninafanya biashara ya madawa ya kulevya, ninayasafirisha kutoka Pakistan. Sijui nilikuwa nasafirishaje Tanzania na Pakistan ilihali hata passport ya kusafiria sina kamanda, alisema Mdude.

Oh! Mwaipaya ni wewe kamanda, umehitimu mafunzo ya gereza. Hongera sana kamanda, naamini kuna kitu umejifunza. Moja kati ya faida kuu ya jela ni kukufanya uwe na ujasiri wa kukipigania kile unachokiamini. Najua sasa wewe ni jasiri. Alimueleza Mdude.

Makamanda wamenipiga, wananiuliza kwa nini ninaisumbua serikali? Walikuwa wamevalia mizura wamenipiga kamanda. Walinipiga nikiwa naumwa, walinitoa kwenye Zahanati ya jela nikiwa mgonjwa wakaja kunisulubu nje huku wafungwa wenzangu wakishuhudia. Wamenipiga alirudia tena akizungumza huku akiwa mwenye ujasiri na akizungumza kwa sauti ya ushupavu.

Ninachokiamini mimi, sikumkosoa Magufuli kwa kuwa nilikuwa namchukia, hapana. Wala sikumkosoa kwa sababu ya sura yake, bali kwa sababu ya uovu wa mfumo wa Serikali yake. Najua Mungu ni mkubwa ipo siku nitatoka.

Nikasogelea zaidi nyavu zinazotutenganisha. Nikamwambia Mhe. Freeman anakusalimia, akaniambia msalimie Mwamba mwambie naisubiria kwa hamu hotuba yake. Nikamwambia Mhe. Mnyika anakusalimia, akaniambia najua amewaandikia barua wenye mamlaka kuhusu madai yangu ya kuteswa gerezani, nimeambiwa. Wamekuja kuniomba radhi nikawaambia tutayamaliza nilikoyasemea.

Wakazungumza na Mwaipaya na kupeana vifungu vya biblia, nikamrudia nikamwambia kuna vitu kadhaa tumekuletea, wana wamekuchangia fedha kidogo. Akasema wapeni wanaonipikia chakula wanajua nini cha kufanya. Wamefanya kazi nzuri sana sijawahi teseka. Waambie watanzania ninawapenda

Aluta continue akatueleza akirejea ndani ya gereza akivuta mguu wake.

Tukaachana naye kulikabili Gereza la Songwe lililopo zaidi ya kilometa 100 kutoka mjini mbeya wanakoshikiliwa wapiganaji wenzetu wapatao 60, kati yao wanaume 53 na wanawake 7 Gereza la Songwe. Wengi wao wakituhumiwa wa kesi za mauaji na uhujumu uchumi.

Leo tutahitimisha ziara yetu katika mahakama huku mkoani Njombe kusikiliza kesi ya mauaji inayowakabili viongozi wetu, akiwemo Mhe. George Sanga Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Njombe.

Unaweza kuchangia chochote kwa ajili ya mahitaji kwa wafungwa wenzetu kwa 0746 777 845 Voda Jina Twaha Mwaipaya

Wasalaam
John Pambalu
jpambalu@gmail.com
0676250710
JOHN POMBE MAGUFULI ASANTE SANA KWA KAZI YAKO. MUNGU ATAKULIPA SAWA SAWA NA MATENDO YAKO. AMENI.
 
Nimesoma hii thread huku machozi yakinilengalenga.

Hii nchi tulishafika sehemu mbaya sana yaani mtu unakosa uhakika wa kesho yako.

Tumuombe Rais Mama Samia ahakikishe huu uonevu uliosimikwa nchini mwetu anauondosha kabisa .
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mdude anafundishwa na ulimwengu maana ***** hakumfunza adabu!

Haya mabavicha vipi?
 
Back
Top Bottom