Mathematics inaweza kutufunulia kuhusu siri za ulimwengu kweli...??

Mathematics inaweza kutufunulia kuhusu siri za ulimwengu kweli...??

Kuna utani wenzetu wazungu huwa wanaamini kuwa watu wanaojua sana hesabu ni viumbe (au wana elements) kutoka sayari zingine.

Hesabu ni logic zanazopaswa kueleweka tatizo wengi tunazikariri na ndio maana unakuta mtu ni profesa lakini bado anaendeshwa na njaa ya siku moja au kulala laktika nyumba nzuri japo hadi sasa hatujui mainjinia waliojenga mfano pyramids waliishi au walikula nini ila kazi za fikra zao zipo na zinaonekana.
Hata recent history iko wazi, huwezi kurusha ndege au kwenda mwezini kwa kuwasingizia wenzio ugaidi wenzio bali hesabu zichemshe kichwa 24/7.
 
mkuu Ile mathematics iliyotumika kukata mawe Kwa kuyashape na zile Kona za Pyramids hupati shaka ya kwamba Ile sio kawaida
Pia Mathematics iliyotumika kuzijenga Parallel kuanzia Mesopotamia,Misri na Mexico,konakry,mstari Mmoja
Ile sio kawaida mkuu!
Kwani binadamu anashindwa..?
Na Kama unaamini sio uweza wa binadamu kuunda hayo ma pyramids unafikiri Nini kilikosekana mpaka hao viumbe wasiwepo tena kati yetu..?
 
Kwani binadamu anashindwa..?
Na Kama unaamini sio uweza wa binadamu kuunda hayo ma pyramids unafikiri Nini kilikosekana mpaka hao viumbe wasiwepo tena kati yetu..?
Binadamu atawezaje kutengeneza kitu kilichomzidi maarifa?
Ile science zama za Leo Leo Bado imewashinda Labda waendelee kutafiti huku mbeleni mkuu,
Zile Pyramids Kwa Nje zipo simple sana ila ukiingia ndani ya bunkers Kule ndani muundo wake Bado una utata Kwa Engineer wa Leo yaani Kila wakipiga hesabu kuona formula wanakwama zinakataa kabisa maana zile angles sio za kawaida,
Kuhusu wajenzi wa zile washaondoka Miaka mingi sana huko nyuma na hawakuacha
Tunaona Kazi zao Bado zipo ila zile walijenga Binadamu wa kawaida zilishazikwa Ndio kwanza watafiti wanachimba ardhini Ndio kugundua miji ya kale ambayo ilijengwa zama ambazo Pyramids zilikua zimeexist Miaka maelfu kabla Yao
Kila kitu kinapita ila Yale madude yamesimama vile vile hayana hata dalili ya kupata ufa what a great Technology!
 
Kwahiyo alikuwa na maana yake..? Okay sijui kiundani zaidi lakini turudi kwenye namba Kama namba achana na Nikola je kwa fikra zako mathe inaweza kutufungulia siri za ulimwengu..?

Mimi ninavyojua ni natural sciences ndizo zinaweza kufungua siri za ulimwengu na maths ni nyenzo inayosaidia natural science, mfano wake ni kama gari na mafuta, gari ni natural science na mafuta ndio maths.
 
Binadamu atawezaje kutengeneza kitu kilichomzidi maarifa?
Ile science zama za Leo Leo Bado imewashinda Labda waendelee kutafiti huku mbeleni mkuu,
Zile Pyramids Kwa Nje zipo simple sana ila ukiingia ndani ya bunkers Kule ndani muundo wake Bado una utata Kwa Engineer wa Leo yaani Kila wakipiga hesabu kuona formula wanakwama zinakataa kabisa maana zile angles sio za kawaida,
Kuhusu wajenzi wa zile washaondoka Miaka mingi sana huko nyuma na hawakuacha
Tunaona Kazi zao Bado zipo ila zile walijenga Binadamu wa kawaida zilishazikwa Ndio kwanza watafiti wanachimba ardhini Ndio kugundua miji ya kale ambayo ilijengwa zama ambazo Pyramids zilikua zimeexist Miaka maelfu kabla Yao
Kila kitu kinapita ila Yale madude yamesimama vile vile hayana hata dalili ya kupata ufa what a great Technology!
Kazi ya hizo pyramids ilikuwa ni nini..?
 
Kuhusu swali lako ......nadhani angekuwepo mtaalamu PYTHAGORAS. kila kitu kilikuwa wazi ....coz huyu mtaalamu ndiye aliyetoa concept ya kuwa Siri za dunia zimefichwa kwenye hesabu

Mfano mchawi ....anaweza kutamka maneno flani hivi kwa kujirudia Mara 3 then kitu fulani kikatokea

Sema Pythagoras alikuwa mchoyo so alikufa na Siri nyingi
 
Kuna huu uhusiano wa namba inaitwa "Golden Ratio" na ulimwengu ambapo kupitia ratio hiyo karibia kila Kitu kinaangukia humo.

Kuanzia kwenye design zote ambazo zimefanywa na binadamu ukifatilia au kutumia golden ratio unapata majibu sambamba kabisa.

Si hivyo tu hata vitu asilia namna vinavyo-exist vyote vinaangukia kwenye "Golden Ratio".

Golden ratio ni namba ambayo inapatikana kwa mfano mstari umegawanywa sehemu mbili, kipande kimoja ni kirefu zaidi ya kingine.

Tuzipe herufi Mistari hiyo yenye vimo tofauti, mstari mrefu (X) na mstari mfupi (Y).
Kupata golden ratio ni kuchukua kipande cha mstari mrefu zaidi (X) gawanya na kimo cha mstari mfupi(Y) jibu utakalo lipata litakuwa sawa na uchukue jumla ya vimo (X) na (Y) ugawanye na kimo cha mstari mrefu na majibu siku zote yatakuletea 1.618.

Golden ratio tunaweza kusema siku zote kama ni hii namba 1.618.

Sasa namba hii inauhusiano na kila kitu katika huu ulimwengu swala tu ukipata kimo cha hicho kitu kwa namna yeyote.

Na kwa kutumia ratio hiyo tunapata design ya vitu vyote kama vile zile Pyramid zilivyojengwa ukifatilia design yake yote inaangukia kwenye golden ratio.

Na pia kutokea hapa kwenye golden ratio pia kuna sequence za namba ambazo ziligunduliwa na jamaa anayeitwa Fibonacci yeye alikuja na mtiririko wa namba ambazo ni 0,1,1,2,3,5,8,13,21,34,..........

Na mtiririko huu ulipatikana kwa kujumlisha namba mbili za mwanzo unapata inayofata alianza na 0,1 ukijumlisha unapata 1, na 1+1, unapata 2 na kuendelea.

Mtiririko huu wa hizi namba unapata maumbo mbali hata wa vidole vyako kwenye pingili pingili zinaangukia kwenye hizi namba.

Unaweza Fatilia Fibonacci sequence & Golden Inaelezea Sana Namna Ulimwengu Ulivyojengeka Na Existence Ya Vitu.
 
Hizo namba zimeshobekewa sana na wataalamu wa unajimu, bila ya sababu ya msingi, hakuna chochote wanachokielezea zaidi ya ushirikina....
 
Ni kweli kabisa. Ukitaka kufahamu hesabu vizuri kabisa, mwombe Bwana Yesu awe mwalimu utafahamu hesabu zote hata za Ellien.
 
Umetisha mkuu ila tatizo ni wapi walipokuwa wanapeleka izo gold?
Gold from Earth to Nibiru/planet X for covering atmosphere sababu sayari Yao iliharibiwa na mionzi ya Nuclear baada ya kupigana vita ya kugombania madaraka iliyopelekea kuharibika Kwa anga lao,
Ndio mission ya kuja duniani ilianza na imerekodiwa na Sumerians tablets ya Kwamba walikuja na Spaceships zaidi ya miaka laki Tano BCE huko nyuma
Na ushahidi upo Dunia nzima Kuanzia Mesopotamia,Misri,Indus valley mpaka Mesomerica kuonesha uwepo wao hapo kale!
 
Ni kweli kabisa. Ukitaka kufahamu hesabu vizuri kabisa, mwombe Bwana Yesu awe mwalimu utafahamu hesabu zote hata za Ellien.
Bwana yesu hesabu zilimshinda akaishia kukongomekwa na warumi kwenye msalaba
Hesabu Gani anazoweza Yesu?
Kutembea Kwa miguu kutoka galilaya to Jerusalem kuasali?

Be serious dude!
 
Gold from Earth to Nibiru/planet X for covering atmosphere sababu sayari Yao iliharibiwa na mionzi ya Nuclear baada ya kupigana vita ya kugombania madaraka iliyopelekea kuharibika Kwa anga lao,
Ndio mission ya kuja duniani ilianza na imerekodiwa na Sumerians tablets ya Kwamba walikuja na Spaceships zaidi ya miaka laki Tano BCE huko nyuma
Na ushahidi upo Dunia nzima Kuanzia Mesopotamia,Misri,Indus valley mpaka Mesomerica kuonesha uwepo wao hapo kale!

mmmmmh! ngumu kumeza hii
 
Funguo ya ulimwenguni juu ya kitu gani??, nadhani concept yake kuhusu hizo namba bado ni ambiguous kwani mtu anaweza kuuliza kwa nini siri ya funguo hizo isiwe namba 0 au namba 8 au namba zinginezo??!!, hizo namba 3,6 na 9 kazipanga katika mfumo huu; 3×1, 3×2, na 3×3. Sasa kimahesabu namba tatu zinazofuatia baada ya 3×3=9 ni 3×4=12, 3×5=15 na 3×6=18, hivyo utaona sequence hadi kufikia 18 ipo hivi; 3,6,9,12,15,18 -----. au labda aliposema namba hizo ni ufunguo wa siri ya ulimwengu alikuwa na maana kwamba; 3 (30°), 6 (60°) na 9 (90°), katika angles ni angle zinazojitoleza katika trigonometry.
 
Na mie naomba kuchangia hii mada ya hesabati ju ya ufunguo wa siri za ulimwengu,
Hii ipo hivi, kiuhalisia hisabati ndio kufuli ya siri za ulimwengu na sio hisabati pekee masomo yote tunayofundishwa skuli kisaikologia yana kuwa ni kufuli za kuifunga akili ya mwanadamu isotoke nje ya ufahamu unaojengwa na mafunzo hayo,
Hesabati sio zao la uhalisi au nature, hisabati ni man-made structure kama ilivyo mifumo ya masaa tarehe,siku,miezi na miaka, hii yote ni mifumo ya kutunga na sio natural, na sababu za kutunga mifumo yote hii ni kutia kufuli akili ya mwanadamu isitoke nje ya box,akili ya mwanadamu isiwe free kuwaza mambo yake yenyewe na iwe imefungika kwenye hii mifumo ya hesabati na tarehe,n.k

Tuutazame mfano huu wa kufuli ya hesabati¡.
inalazimisha namba zianzie 0 mpaka 9 hii maana yake akili haiwezi tena kutoka nje ya namba 9 na akili haiwezi tena kuvumbua namba mpya zaidi ya namba 9, na haiwezi kuja na maarifa zaidi yatokayo nje ya 0 to 9, yaani kwenye akili zetu mwangaza upo kuanzia 0 mpaka 9 tu baada ya hapo ni kiza kitupu na blockage

Twende kwenye Siri za ulimwengu hizo zinazotarajiwa kufumguliwa kwa hesabati [emoji75],
Siri za ulimwengu haziwezi kufunguliwa na elimu au mfumo wowote tunaoufahamu sisi binadamu, yaani kiuhalisia hizi elimu na mifumo inayotujenga sisi binadamu ipo kwa ajili ya kutuweka mbali na ufahamu wa mifumo halisi ya ulimwengu, na mifumo yote tuliyofunzwa ya ulimwengu sio ya ukweli yote ni uzushi. Na hii mifumo ya uzushi imejengwa kwa kukubaliana na hesabati na kwenye akili zetu chochote kinachokubaliana na hesabati ni kitu halisi.
Kuanzia dunia yenyewe ilivyo, upatikanaji wa seasons, kinachosababisha usiku na mchana, uhalisi wa jua,mwezi,nyota na sayari, upepo ni kitu gani na unasababishwa na nini, mvua inapatikanaje na mengi mengineyo haya yote yanatolewa maelezo yake katika elimu za kutunga za kutunga na sio katika uhalisi wake.
Sisi binadamu sote dunia nzima tunaishi maisha yote hapa duniani hatuwezi kujua kabisa dunia ni kitu gani kiuhalisia, tunaelimishwa kwa kuoneshwa picha za kuchora na video za animations tu, na hakuna hata picha moja ya dunia ambayo ni ya kweli,binadamu hatutakiwi kuijua dunia ni nini na pia hatutakiwi kujua siri halisi za ulimwengu, mambo tunayofunzwa ni mambo ya kutupumbaza tu na kuupoteza wakati wetu wa maisha bure, na kutufanya tusijielewe hata sisi wenyewe ni nani hasa

Nadhani ntarudi tena baadae kuendelea
umeongea kitu kikubwa sana mkuu
 
Back
Top Bottom