Mfumo kama mfumo unaweza ukawa ni mzuri, ila tatizo linakuja ni kwanini wameshusha grade.
Kwann A imeshuka mpk 75% n.k, hapa unamshawish mtu aamin serikali inaficha uozo wa shule za kata na ufaulu kwa ujumla ili watu wengi wasijue elimu inavyoshuka.
Mfumo wa GPA ni mzur na lengo linaweza kuwa zuri, shida ni kwenye grading system. Inaamana walishindwa kuweka huu mfumo wa GPA kwa grading zile zile za zaman? Kulkuwa na ulazima gani wa kulazimisha kila kitu kifanane na chuo?
Na pia tunajidanganya wenyewe tu na mataifa mengine yatakuwa yanaticheka tu, tunaposema eti GPA 0.3-1.5 ni PASS. Hapa tunajidanganya wenyewe tu. Huu ufaulu wa asilimia 68 umechukua mpk hy PASS jamaniiii, hapa tunajidanganya wenyewe.
Mfumo ni mzuri ila kwa kushusha hizi grade na kuiweka GPA ya 0.3-1.5 kuwa PASS tunashusha elimu yetu wenyewe.