Matokeo Kidato cha Nne 2016 yatoka, Feza Boys yaongoza!

Matokeo Kidato cha Nne 2016 yatoka, Feza Boys yaongoza!

Elimu ina umuhimu sana ndio manake kwa miongo kadhaa tumeona shule za madhehebu zikifanya vizuri hata baada ya shule nyingi za madhehebu kutaifishwa wakati wa awamu ya kwanza bado kuliendelea kuibuka uanzishwaji wa hizi shule ni wakati muafaka wa kwenda kujifunza kwa hizi shule wanavyofanya kazi na mazingira ya elimu inayotolewa.
 
Je katika wanaomiliki 80% ya uchumi hapa bongo ni wakatoliki?, wanaomiliki sheli na masupermarket makubwa ni wakatoliki?, wanaomiliki mabasi ni wakatoliki?............ weka list yamatajiri mia hapa bongo kama wakatoliki watafika hata
Huyu kasifia Shule za Kanisa Katoliki...Mambo ya matajiri yametoka wapi..?
 
Je katika wanaomiliki 80% ya uchumi hapa bongo ni wakatoliki?, wanaomiliki sheli na masupermarket makubwa ni wakatoliki?, wanaomiliki mabasi ni wakatoliki?............ weka list yamatajiri mia hapa bongo kama wakatoliki watafika hata kumi, lengo langu suo ofensive kwa wakatoliki(wanisamehe), ila tu ninkukuonesha kichwa chako jinsi kilivyojaa kamasi, Miaka kumi iliyopita MARIAN na shule nyingine zinajitahidi kutoa division one wanaoishia kufanya kazi kwa wahindi tu........ Highly stupidity

MAISHA MAZURI NI ZAIDI YA KUPATA DIVISION ONE.
umenena vema wakatoliki huwa hatuna kawaida ya kujisifia, huyo kateleza sisi kwetu elimu ni kama afya tu, ukiwa na afya njema huwezi mcheka aso na afya bali kumuombea awe na afya
 
Kwa sasa suala la Elimu ya Msingi na ile ya Upili imekuwa ni jukumu la sekta binafsi
Sekta binafsi ndio inajenga mazingira bora ya elimu na watoto kufanya vizuri kuliko serikali.

Lakini "Social Contract" kati ya wananchi na serikali kila baada ya miaka mitano ya kuomba kura huwa ni malipo ya elimu bora,afya bora na huduma bora za maji na maisha.

Serikali imekuwa mdau mkubwa wa kutokufuata masharti haya ya "Social Contract" kati yake na wapiga kura.Kuwepo na ukosefu wa shule za serikali ktk kumi bora,ni moja ya uvunjwaji mkubwa wa "mkataba wa kijamii" kati ya serikali na wananchi.Na hapa Serikali inapswa kuadhibiwa.

Unawekaje kipimo sawa kati ya mwanafunzi anayesoma kwa kibatari na chemli kule Iselamagazi Tabora na yule anafanya study Tour Uturuki huku akiwa na mazingira bora ya kusoma?

Na hili kudhihirisha hivyo,kwa sasa huwezi kukuta viongozi wa serikali wakipeleka watoto wao ktk shule za serikali kwa maana na wao hawaamini ktk ubora wa elimu inayotolewa na shule za umma.

Ilboru,Tabora Boys,Mzumbe,Kibaha,Weruweru,Tabora Girls,Kilakala,Msalato na Korogwe Girls zimebaki magofu ya historia ya elimu bora ya Tanzania.Majengo ni toka ya mkoloni.Hakuna jitihada za kimkakati za kurudisha ubora.

Elimu imekuwa biashara badala ya Huduma.Na hao watunga sera wanaopaswa kuirudisha elimu ktk mstari mnyoofu ndio wafanyabishara wa elimu.Waziri anamiliki shule,mbunge anayeisimamia serikali naye anamiliki shule au kuwa na hisa ktk biashara ya elimu.

Katika nchi zilizoendelea,Elimu ya msingi na upili sio biashara,bali ni huduma.Ni huduma kwa sbb ni haki ya kimsingi ya kila mtu kupata elimu ya msingi na ya upili.Ndio maana nchi kama Sweden ni fahari kuwa sehemu ya shule ya serikali kuliko binafsi.

Mazingira ya kielimu ya mtoto aliyeko Kwa Msisi Handeni,ambapo zaidi ya kuwaza masomo,anawaza wapi atapata maji ya kuoga na kunywa si sawa na Marian Girls,ambapo mpaka pedi mtoto anaikutq kati vyoo vya shule,hawa hawawezi kuwa sawa kieleimu na kimtazamo.

Hii ni sawa na kuwaweka ulingoni Dula Mbabe anyecheza ngumi za amacha na Myweather
Its like feather weight boxer vs heavyweight boxer!!Kwa hili tujitathmini upya


Barafu shkamoo....halafu hapohapo ulipo geuka kushoto au kulia ukion BAR au Restaurant agiza kinywaji mi nipo nakuja mkuu
 
Back
Top Bottom