Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

Mh! KIia neno ninalotaka kutumia kuelezea machungu yangu
naliona halifai. Anyway, ngoja nisome comments za wengine...
 
Maadui wakuu.....ujinga, umasiki na maradhi, 50 years ya uhuru bado ni kusadikika! CCM??????? Makes me cry aiseeh
 

Lakini hii strategy yao imepitwa na wakati, hawa wajinga wanaotujazia huku mtaani ndo watakaoenda kuwang'oa madarakani na mapanga na fimbo mikononi, bomu alilolisema mamvi ndo linazidi kukua na kupata nguvu kila mwaka, litakapolipuka tutatafutana
 
Ninapenda kukopa maneno ya makocha wa soka waliosema wachezaji wa kibongo hawafundishiki, ni. Sawa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule za umma 90% hawafundishiki. Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuinusuru elimu na KUWALIZIMISHA VIONGOZI WOTE WA UMMA WASOMESHE WATOTO WAO KATIKA SHULE ZA KATA WANAZOISHI,KUANZIA RAIS WA NCHI NA BARAZA LOTE LA MAWAZIRI NA TAASISI ZOTE ZA UMMA.LABDA WATABORESHA ELIMUNA MIUNDO MBINU YA SHULE ZA UMMA.
 
Tatizo ni kwamba huwezi kuutatua mgomo baridi,watu wanakwenda kazini na muda wa kazi wanarudi nyumbani,darasani wanaingia na home work wanatoa na wanazisahihisha.
 
Wapewe nafasi ya kureseat, sishangai kama wameingia kidato cha kwanza hawajui kusoma wala kuandika nini mmatokeo yake,kuna tatizo kubwa na wanalijua wote serikali na chama cha walimu tanzania kaeni mzungumze vinyongo mlivyoweka rohoni vinaumiza watoto wetu hasa sisi wa hali ya chini tunaosomesha ST. KAYUMBA. Ni mawazo tu,

Nawasilisha
..................!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tusubiri taarifa zaidi tujue takwimu maana nimemuona anaongopa hata kutaja ni wangapi au asilimia ngapi imefail kwa kifupi naona ni more than 75% ingekuwa hata nusu angesema ili apate sifa

Wanafunzi zaidi ya 130,000 hii ni hatari kwa taifa letu. Lakini pia hawa watu wangeweza kwenda kwenye vyuo vya ufundi mapema kabisa. Sasa ona waloshushiwa maksi za ufaulu darasa la saba, kisha hawakupata waalimu wazuri na mwisho wa wakifika kwenye shule za kata zisizo hata na mandhali nzuri za kujisomea. Taabu tupu.
 
masikini Tanzania yangu sijui inaelekea wapi jamani.
 
Tanzania nawashauri tutofautishe siasa (mambo muhimu) kama vile elimu, afya, nk. nje ya hapo ni janga kwa taifa na hasara

Mkuu upo nchi gani? Siku hizi Kila kitu ni Siasa hapa bongo, misiba, harusi, kitchen party, michezo, barabara, reli, bia, hata maradhi nayo siasa. Jionee mwenyewe wanasiasa wanavyojipendekeza kwenye hayo masuala kwa interest za Siasa
 
wameshusha na kiwango cha ufaulu std 7! siku hizi mtihani wa hesabu std 7 ni multiple choice, yaani ni ujingaaaaaaa ambao hata mayai yangu kwenye ovaries hayawezi kubali!! stupid me kuendelea kuwa na vitu vyenye rangi ya KIJANI!

pole dada! Tuliopitia hii fani tunajua kinachoendelea.
 
Na bado wasubirie zero zingine mwezi wa tano huo,wakibadilika nasi tutabadilika hivi hivi wategemee matokeao haya muda wote kudadadeki zao
 
Tulisema waalim wako kwenye mgomo mkubwa sana mkakataa!! Ukweli ni kuwa mgomo wa waalim upo kwa style ambayo mpaka serikali ikubali basi mtakuta kielimu vizazi vimeangamia!! Matokeo ya darasa la saba si wameona kwa shule za serikali? Subirini na ya kidato cha nne kwa shule za serikali? Matamko mabaya serikali inatoa kwa waalim na kuwatishia badala ya kusikiliza na kutekeleza pale inapowezekana na kuomba angalao muda wa kuyamaliza basi yatatafuna watoto wetu. Washishangae, waalim wako busy na biashara zao mashuleni au nje ya shule!!!
 
Walimu wamegoma kutoka na kutosikilizwa, wakaongezewa mzigo watoto 90 katika darasa moja, (50 hawajui kusoma na kuandika), mazingira ni magumu kupindukia (kila siku kuna tishio la kuvamiwa na kuibiwa, kubakwa, kuliwa na fisi mtu, shule ipo kilometa kadhaa kutoka makao makuu ya Kata, .........), wazazi hawakupenda wanafunzi (watoto wao) waende shule bali walitishiwa kufungwa na Mtendaji wa kiljiji n.k JE TUTARAJIE UFAULU??
 

Mikoa ya LINDI na MTWARA ndo inaongoza kwa kufanya vibaya katika mtihani huo.... Je, nako anataka kutuambia nini!
Aache porojo zake, wanapaswa kukubali kuwa utitiri wa shule za kata zisizo na walimu wala vitendea kazi pamoja kuwadharau walimu wa nchi hii ndo chanzo kikubwa,ebo....!
 
Tusubiri taarifa zaidi tujue takwimu maana nimemuona anaongopa hata kutaja ni wangapi au asilimia ngapi imefail kwa kifupi naona ni more than 75% ingekuwa hata nusu angesema ili apate sifa

Zaidi ya wanafunzi laki 3 watarudia mtihani.
 

Elimu hziwezi kuimarika ikiwa kama hao viongozi hawapo tayari 'kula wanachopika'. Naamini ili kuweka mambo sawa kila kiongozi wa umaa ampeleke mtoto wake shule ya umma. Shule za binafsi ziachiwe wafanyabiashara na raia wengine.
Najua hoja hii itabigwa vita kubwa kwa kuwa wateja wakubwa, na hata wamiliki, wa hizo shule za binafsi ni wanasiasa. Wanasiasa wanataka watoto wao wafaulu ili waje warithi viti vyao. Ikiwa kama viongozi hawazithamini hizo shule wanazojenga na kuwalazimisha wazazi kupeleka watoto wasiojua kusoma na kuandika, je nani atazithamini? Cuba ni moja ya mataifa yanayoheshika duniani kielimu kwa kuwa ni lazima kwa kiongozi wa umma kumpeleka mtoto wake shule ya umma.
 
Waalim wa Dar wako busy na miradi maana serikali ilishatupa waalim!!! Wako mgomo seriously!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…