Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiki kinachofanyika ni makusudu kabisa kwa hii Serikali ya CCM
- Kwani wao Ujinga wa Watanzania ndiyo manufaa yao kuendelea kututawala, kwani haiingii akilini mtu apewe Kofia, Fulana na scaf halafu hakipigie kura hicho chama kama shukhrani kwa zawadi hiyo
- Huku kudumaza kwa elimu kwa walala hoi ni manufaa yao pia kwani watoto wao shule wanazosoma ni tofauti na hizi shule kwahiyo watoto wao mwisho wa siku tukiingia kwenye soko la ajira wao watapewa kipaumbele kutokana na CV zao
- Kama Hii serikali ingekuwa na nia ya dhati kutatua tatizo la elimu katika nchi hii kwa nini wameshindwa kutatua tatizo la walimu kimaslahi? kwani tukilinganisha shule za Private na hizi za Mchangani(Serikali) zinatofautiana sana kiufauru kwani wenzetu wa Private walimu wanafanya kazi pasipo manung'uniko na wanakubaliana na malipo wanayopata kutokana na makubaliano ya mikataba yao.
Tusubiri taarifa zaidi tujue takwimu maana nimemuona anaongopa hata kutaja ni wangapi au asilimia ngapi imefail kwa kifupi naona ni more than 75% ingekuwa hata nusu angesema ili apate sifa
Tanzania nawashauri tutofautishe siasa (mambo muhimu) kama vile elimu, afya, nk. nje ya hapo ni janga kwa taifa na hasara
wameshusha na kiwango cha ufaulu std 7! siku hizi mtihani wa hesabu std 7 ni multiple choice, yaani ni ujingaaaaaaa ambao hata mayai yangu kwenye ovaries hayawezi kubali!! stupid me kuendelea kuwa na vitu vyenye rangi ya KIJANI!
Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi, waziri Mulugo, ameshangazwa na matokeo mabaya kwa wanafunzi wa kidato cha pili ambapo Dar es salaamu ndiyo mkoa ambao wanafunzi wamefanya madudu sana! Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akiyatangaza matokeo ya kidato cha pili, ametumia muda huo kupinga dhana iliyoyojengeka kwamba wanafunzi wanafeli kwa sababu hakuna walimu akitolea mfano jiji la Dar es salaam kuwa na walimu wengi na bado wanafunzi wamefeli. Ametoa wito kwa wazazi kufatilia maendeleo ya watoto wao mashuleni, na pia akawataka waalimu wajiulize sababu ya hawa wanafunzi kufeli.
MY TAKE:
Sijui mulugho anataka kusema nini lakini wizara ndiyo ambayo inapaswa kutupa majibu, kama waziri anayehusika na elimu anaona matokeo mabovu anashangaa na kuuliza maswali sijui wananchi watakua katika hali gani, ni miaka mingi sasa wizara ya elimu inafanya madudu na kuchezea elimu za watoto wetu, tunaomba Rais aitizame elimu kama kitovu cha maendeleo!
Tusubiri taarifa zaidi tujue takwimu maana nimemuona anaongopa hata kutaja ni wangapi au asilimia ngapi imefail kwa kifupi naona ni more than 75% ingekuwa hata nusu angesema ili apate sifa
Ninapenda kukopa maneno ya makocha wa soka waliosema wachezaji wa kibongo hawafundishiki, ni. Sawa kwa wanafunzi wanaosoma katika shule za umma 90% hawafundishiki. Kuna haja ya kuwa na mjadala wa kitaifa kuinusuru elimu na KUWALIZIMISHA VIONGOZI WOTE WA UMMA WASOMESHE WATOTO WAO KATIKA SHULE ZA KATA WANAZOISHI,KUANZIA RAIS WA NCHI NA BARAZA LOTE LA MAWAZIRI NA TAASISI ZOTE ZA UMMA.LABDA WATABORESHA ELIMUNA MIUNDO MBINU YA SHULE ZA UMMA.