shule zilizofanya vibaya ni kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania, Lindi na Pwani. naona mkoa wa Pwani nao kauhamishia kanda ya kusini. . mh kweli wizara imepata naibu
Hao watoto wa DSM wengi madaftari yao yamejaa mistari ya Bongofleva.
Mkuu yanapatikana wapi?Matokeo ya mtihani wa taifa ya kidato cha pili yametoka leo ambapo:-
1.Waliofanya mtihani walikuwa 386,248
2.Waliofaulu walikuwa 249,325 (65%)
3.Waliofeli walikuwa 136,923 (35%). Ilielezwa kuwa mkoa wa DSM ndo umefelisha vijana wengi zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine.Je,vijana wamefeli ama serikali? Je,walichofeli walifundishwa? Tumejikwaa wapi?
Labda nichukue fursa hii kumkumbusha Naibu Waziri Mh (Amin) Philipo Mulugo kuwa NG'OMBE JIKE ASIPOLISHWA VIZURI HAWEZI KUTOA MAZIWA. Leo tunashangaa matokeo na kujadili kuhusu sababu ya kufeli na cha kushangaza zaidi anatoa wito kwa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni, hii haisaidii kabisa. Mwaka jana kulikuwa na mgomo wa watukufu walimu nchi nzima na hata baada ya mgomo walimu hao waliahidi kundelea na mgomo kwa style ya kutofundisha kwa weledi. Kifupi cha mambo haya ni kwamba matokeo ya kidato cha pili, cha nne cha sita na mengine yatakayokuwa chanzo chake ni serikali yenyewe. Yaelekea Philipo ni msahaulifu sana juzi tu kasababisha leo anashangaa.
Mh Mulugo that is YOU.
Walimu wamegoma kutoka na kutosikilizwa, wakaongezewa mzigo watoto 90 katika darasa moja, (50 hawajui kusoma na kuandika), mazingira ni magumu kupindukia (kila siku kuna tishio la kuvamiwa na kuibiwa, kubakwa, kuliwa na fisi mtu, shule ipo kilometa kadhaa kutoka makao makuu ya Kata, .........), wazazi hawakupenda wanafunzi (watoto wao) waende shule bali walitishiwa kufungwa na Mtendaji wa kiljiji n.k JE TUTARAJIE UFAULU??