Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

Matokeo kidato cha pili 2012 hatimae yatolewa, mkoa wa D'salaam washika mkia.

Hatutaki kufikiri na wanaotaka kufikiri hutuwaachi wafikiri, tunawazui ili tuwe na kizazi cha watu wasiofikiri. ELIMU NI ENGINE YA MAENDELEO, SISI TUMEBAKI KUREMBA BODI WAKATI ENGINE ILISHAOZA. Mara oooo "Kilimo kwanza" halafu elimu baadae. "Mara barabara kwanza" elimu baadae, "kusafiri kuomba misaada kwanza"elimu baadae. Anyway! hili nalo litapita na utazuka mjadala mwingine, na future za wanetu walalahoi ndo wameshaziharibu.
 
Amekosea kutamka desimali.....45 (desimali) inatamkwa nukya nne tano sio arobaini na tano!!alikuwa anasoma matokeo ya zimbabwe!
 
habari wana jf. leo naibu waziri wa elim Mulugo ametangaza matokeo kidato cha 2 na zaidi ya wanafunzi 136000 watalazimika kukariri darasa. je taifa linaelekea wapi?
 
shule zilizofanya vibaya ni kutoka mikoa ya kusini mwa Tanzania, Lindi na Pwani. naona mkoa wa Pwani nao kauhamishia kanda ya kusini. . mh kweli wizara imepata naibu

Chezea Mulugo veve! kabla hata hawajachakachua ye keshatangaza.
 
Matokeo ya mtihani wa taifa ya kidato cha pili yametoka leo ambapo:-
1.Waliofanya mtihani walikuwa 386,248
2.Waliofaulu walikuwa 249,325 (65%)
3.Waliofeli walikuwa 136,923 (35%). Ilielezwa kuwa mkoa wa DSM ndo umefelisha vijana wengi zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine.Je,vijana wamefeli ama serikali? Je,walichofeli walifundishwa? Tumejikwaa wapi?
 
Hao watoto wa DSM wengi madaftari yao yamejaa mistari ya Bongofleva.
 
Kesho maandamano kulekea NECTA kumng'oa Joyce, halafu kurudi wizarani kumng'oa Phillipo. Shukuru tusimguse kwa kuwa yeye ni mwenzetu
 
Safi............ifike pahala serekali itambue umuhimu wa waalimu yote haya ni kwa sababu ya kutokuwajali waalimu.
 
Wakati huu ambapo wadau wa elimu wakichambua matokeo ya kidato cha Pili, na kutoa maoni yao juu ya kushindwa kwa wanafunzi, na nini kifanyike.
Naomba ikiwa kama kuna mtu yeyote yule anayekumbuka ufaulu (kwa maana ya asilimia) ulikuwa wa kiasi gani miaka ya 2004 kurudi nyuma (wakati mtihani wa kidato cha Pili ukiwa na heshima) atujuze. Hii itasaidia, kwa namna moja au nyingine, kuyapima matokeo ya wakati huu. Karibuni sana.
 
Dar lazima iburute mkia..we vitoto vya form 2 tunagongana navyo machi machi annex vinapiga kazi hatari..ysani kama ni midifidi basi iniesta...
 
Matokeo ya mtihani wa taifa ya kidato cha pili yametoka leo ambapo:-
1.Waliofanya mtihani walikuwa 386,248
2.Waliofaulu walikuwa 249,325 (65%)
3.Waliofeli walikuwa 136,923 (35%). Ilielezwa kuwa mkoa wa DSM ndo umefelisha vijana wengi zaidi ikilinganishwa na mikoa mingine.Je,vijana wamefeli ama serikali? Je,walichofeli walifundishwa? Tumejikwaa wapi?
Mkuu yanapatikana wapi?
Queen Esther
 
Labda nichukue fursa hii kumkumbusha Naibu Waziri Mh (Amin) Philipo Mulugo kuwa NG'OMBE JIKE ASIPOLISHWA VIZURI HAWEZI KUTOA MAZIWA. Leo tunashangaa matokeo na kujadili kuhusu sababu ya kufeli na cha kushangaza zaidi anatoa wito kwa wazazi kufuatilia maendeleo ya watoto shuleni, hii haisaidii kabisa. Mwaka jana kulikuwa na mgomo wa watukufu walimu nchi nzima na hata baada ya mgomo walimu hao waliahidi kundelea na mgomo kwa style ya kutofundisha kwa weledi. Kifupi cha mambo haya ni kwamba matokeo ya kidato cha pili, cha nne cha sita na mengine yatakayokuwa chanzo chake ni serikali yenyewe. Yaelekea Philipo ni msahaulifu sana juzi tu kasababisha leo anashangaa.
Mh Mulugo that is YOU.

Kwani viongozi wetu wa kisiasa wanajali ng'ombe asipotoa maziwa?
 
Walimu wamegoma kutoka na kutosikilizwa, wakaongezewa mzigo watoto 90 katika darasa moja, (50 hawajui kusoma na kuandika), mazingira ni magumu kupindukia (kila siku kuna tishio la kuvamiwa na kuibiwa, kubakwa, kuliwa na fisi mtu, shule ipo kilometa kadhaa kutoka makao makuu ya Kata, .........), wazazi hawakupenda wanafunzi (watoto wao) waende shule bali walitishiwa kufungwa na Mtendaji wa kiljiji n.k JE TUTARAJIE UFAULU??

Nijuavyo mimi elimu ya msingi ni lazima kisheria? Je, elimu ya sekondari nayo ni lazima hata wazazi walazimishwe kupeleka watoto wao huko?
 
Hivi mnategemea watoto wanaoshinda kutwa nzima na Watsapp na BBM wataingiza nini kichwani....kuna mwaka mtakuja kutangaziwa "TANZANIA NZIMA HAKUNA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI ALIYEFAULU KWENDA KIDATO CHA TATU" mtafanya nini?
 
Kiukweli waliofauli ni chini ya 35% tulio sahisha tunajua pass mark badala ya 30% wastani masomo yote wakashusha hadi 15% kwa masomo yote ili kila shule zipate kidato cha 3. Hali ni mbaya.
 
Mleta mada naona umeamua kuongezea na chumvi chumvi!
hizo shule za kikristo zilizofaulu masomo ya kiarabu sijui umeziona wapi?
 
Back
Top Bottom