Wote mnakumbuka enzi za Sadam Hussein wa Iraqi. Ikumbukwe kwamba Wasuni ni wachane kwa idadi ukilinganisha na washia na baada ya hapo kuna wa Kurds.
Nilikua sijui chanzo cha haya maajabu kwamba Pamoja na upinzani mkubwa Sadam aliokua akiupata toka kwa washia na wakurds, bado kwenye chaguzi za Urais alikua anashinda kwa kwa asilimia 90 na kuna uchaguzi alishinda kwa asilimia mia. Kumbe inawezekana. CCM na mwenyekiti wao wa chama wametutoa tongotongo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Kwanza mwenyekiti wao nasikia hakuwahi kuruhusu ushindani kwenye jimbo lake. Basi hiyo tabia kaihamishia kwenye taifa zima bila kujali anatuharibia mshikamano wetu. Kwa Wakumbukao, kwenye kampeni 2015 huyu bwana alilalamika kuonewa kwa Sadam na aliowaita mabeberu kila alikopita.
Walichofanya CCM ni typical ya enzi za Sadam Hussein kwamba zuia kwa namna yoyote ile mchakato huru wa uchaguzi then tengeneza mazingira raghai kuonesha ushindi wa kishindo.
CCM wanajua kwamba Jinsi siku zinavoenda, Chama kimepoteza uungwaji mkono, kilichobaki sasa hata uchaguzi hawautaki.
Watajitofautisha vipi na kikundi cha watawalao inchi kimabavu, au enzi za ukoloni sijui.