Wakuu, Mi niefuatilia matokeo ya Form four yanatiusha sana, kiwango kimeshuka sana mwaka huu. Ila kuna mambo mengi sana yanachangia
•Kumjaribu mtu kwa masaa 2-3 ni uonevu mkubwa. Inawezekana mwanafunzi akawa anfanya vizuri sana darasani laniki siku ya mtihani akawa hajisikii vizuri. Cha kufanya ni kwamba, NECTA ingeanzisha utaratibu mpya wa kutahini wanafunzi kwa awamu mbili. Moja kuchukua wastani wa miaka yote mine na uwe na uzito wa alama 30%, then mtihani wa mwisho uwe na uzito wa alama 70%. Hata vyuo wanafanya hivi pia. Waanade form za kujazwa ambazo pia mkurugenzi wa elimu wilaya na kanda atazikagua ili kupunguza degree ya kuchakachua. Hii itasaidia pia wanafunzi kusoma kwa bidii.
•Serikali kuangalia upya utitiri wa mashule yanayofunguliwa yasiyo na ubora wala walimu wa kudumu.
•Kuwe na Library ya kujisomea shuleni, shule nyingi za kata hazina library.
•Kupiga marufuku Tuition zote na kupitisha sheria kufanya kitendo hiki kua kosa la jinai.
•Kufanya elimu ya form Six kua ya lazima.
•Kubadilisha mitaala shule ili kumwezesha mwanafunzi pindi amalizapo form four angalau awe na ujuzi wowote kama userimala, ufundi, upishi, ufugaji wa kuku, kitimoto n.k
•Shule ambazo azifaulishe zipewe adhabu kali kwani wanakula ada tu za wanafunzi bila kutoa elimu bora.