MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

wadau nielekezeni nifanyeje, website ya necta hayadisplay. Ni ufedhuli wametufanyia wananchi? Nina madogo zangu nashindwa kuona matokeo yao, na niko ulaya. Hawa necta wana wazimu? Halafu mbona hawajayatangaza?

sasa uko ulaya matokeo ya huku ya nini
 
Shule nyingi za KATA sasa zimeanza kutoa wahitimu wa kidato cha nne. Kwa hiyo haya matokeo siyo ya ajabu. Ni jambo lililotarajiwa. Tunavuna QUANTITY badala ya QUALITY. Na madhara yake yatakuwa ya muda mrefu kama yalivyokuwa ya UPE.
 
Mafisadi wanapeana tenda!Nothing new there!

kWA HILI NITATOFAUTIANA NAWE KIDOGO MKUU! NCHI YETU NI KUBWA SANA NA HUDUMA YA INTERNENT ASILIMIA KUBWA KTK NCHI YETU HAKUNA.UTAKUMBUKA HAPO AWALI ILI MATOKEO MWANAFUNZI AYAPATE ILIMBIDI AENDE MKOANI AU SHULENI KUANGALIA KWENYE VITABU VYA MATOKEO PUNDE VIKIFIKA MIKOANI BAADA YA MATOKEO KUTANGAZWA. (1) KWA UTARATIBU HUO MWANAFUNZI ALICHELEWA KUPATA MATOKEO YAKE (2) ILIKUWA NI GHARAMA KUBWA KWA WANAFUNZI (3) URASMU MWINGINE ULIANZA JITOKEZA KWA MIUNGU MTU MIKOANI NA AU MASHULENI. MTANDAO AMBAO UMEENEA KARIBU KILA SEHEMU NI WA SIMU. KWA NIONANYO MIMI KURUHUSU MWANAFUNZI KUJUA MATOKEO YAKE KWA SMS SHS 400 (1) NI GHARAMA NDOGO UKILINGANISHA NA WALIYOKUWA WAKIPATA AWALI-HII INAWAPA UNAFUU (2) INAMFANYA AJUE MATOKEO YAKE KWA HARAKA, IMEDIATELY, YANAPOTANGAZWA (3) INAONDOA URASMU NA UKIRITIMBA WA KUPATA MATOKEO YAKE. HOJA YA MAKAMPUNI MENGINE KUSHINDWA TOA HUDUMA HIYO HAPO NDO SWALI LA MTOA HOJA!!! AMBALO LINAENEA AKILINI MWANGU PIA. KWA KUWA WATEJA (WANAFUNZI) WENGINE WANAWEZA KUWA HAWANA VODA NA MAENEO MENGINE NCHINI HUENDA HAYAFIKIWI NA MTANDAO WA VODA PIA. HILI NALO KWA KUWA NI UHURU WA MTOA HUDUMU (MTANDAO) HUENDA CHA KUJIULIZA KWA NINI MAKAMPUNI MENGINE HAYATAKI SAIDIA WATUMIAJI WAKE KUTOA HUDUMA HIYO PIA.
 
1. Wajameni, hili nalo litasaidiaje watoto kufaulu kidato cha nne?
2. Shule kama haitoi elimu bora, usimpeleke mwanao. Sasa mwanao kashindwa interview kwenye shule nzuri (nyingi za Katoliki) inabidi umpeleke popote; na matunda yake ndiyo hayo. Lingine ni kwamba shule nzuri gharama yake ni kubwa, hivyo ukichagua gharama ndogo si budi hukubali matokeo.

hakuna mxzazi mwenye uwezio anaye weza kumpeleka mwanae kwenye hizi shule so solition ni serikali kutatua hili tatizo na wala hii sio solution..wazazi ambao hawana uwezo ndio wapo wengi nchini
 
mkuu naona unajaribu saana ku divert issue..hamna mtu anayelalamika majibu kutopatikana kwa wananchi..issue ni kwamba iweje wizara iwatumie voda peke yake?? Na pili kwanini voda icharge watu wakati wizara ina budget maalum ya kutangazia wanafunzi kama wanavyofanya kwenye magazeti? Unachoshindwa kuelewa wewe ni nini ??

sasa mkuu ukitaka wizara itangaze kwenye magazeti itakuwa gharama kubwa kwa mwanafunzi kunua hayo magazeti, nafuu na sms.na magazeti vijijini ambako ndo kwenye wanafunzi wengi yatafika lini?? Mwanafunzi atachelewa pata matokeo. Swala la kwa nini voda pekee, mkuu hii inaonekana ni kama mwenye mtandao kutoa hudumu, hoja ni je kwa vipi mitandao mingine nayo isione haja ya kusaidia watumiaje wake kupata matokeo kwa namna hiyo!!!
 
Wanasomaje shule za kata mkuu?? Mwalimu mmoja hadi 3?? Wengine just form 6 level bado hawajasomea ualimu?? Mazingira ya shule duni yasiyo motisha mwalimu kubaki shuleni!!!!, vifaa hakuna, maabara hakuna-shule za kisiasa ambazo kwa sasa ndo 95% ya shule za sekondari nchini. What do you expect?? Matokeo ya necta ni reality na sasa shule na usomaje wake huko ni politically motivated. Mkuu shule za sekondari, haki, zinahali mbaya sana- you can not imagine!!
 
Kawambwa inabidi aingilie hili

hawezi kukaa kimya ili hali watu wanalazimishwa kuwa na network ya Voda kupata matokeo.

tunajua fika kuwa walalahoi wengi network yao ni TIGO , hivi waziri KIvuli wa ELIMU wa CUF na CHADEMA mbona wako kimya?
 
Kinashoshangaza pia ni kwamba mwaka huu hata zile za private naona nazo zimefanya vibaya. Au labda sikuangalia vizuri?? Kuna kitu hapa si bure. Waalimu wantakiwa watupe majibu hapa. Aidha safari hii hawakufuata syllabus inavyosema? Au ndiyo kusema ni kwa mara ya kwanza mitihani haikuvujishwa kabla ya tarehe zake?? Ngumu kuelewa.
 
Wakuu, Mi niefuatilia matokeo ya Form four yanatiusha sana, kiwango kimeshuka sana mwaka huu. Ila kuna mambo mengi sana yanachangia

•Kumjaribu mtu kwa masaa 2-3 ni uonevu mkubwa. Inawezekana mwanafunzi akawa anfanya vizuri sana darasani laniki siku ya mtihani akawa hajisikii vizuri. Cha kufanya ni kwamba, NECTA ingeanzisha utaratibu mpya wa kutahini wanafunzi kwa awamu mbili. Moja kuchukua wastani wa miaka yote mine na uwe na uzito wa alama 30%, then mtihani wa mwisho uwe na uzito wa alama 70%. Hata vyuo wanafanya hivi pia. Waanade form za kujazwa ambazo pia mkurugenzi wa elimu wilaya na kanda atazikagua ili kupunguza degree ya kuchakachua. Hii itasaidia pia wanafunzi kusoma kwa bidii.
•Serikali kuangalia upya utitiri wa mashule yanayofunguliwa yasiyo na ubora wala walimu wa kudumu.
•Kuwe na Library ya kujisomea shuleni, shule nyingi za kata hazina library.
•Kupiga marufuku Tuition zote na kupitisha sheria kufanya kitendo hiki kua kosa la jinai.
•Kufanya elimu ya form Six kua ya lazima.
•Kubadilisha mitaala shule ili kumwezesha mwanafunzi pindi amalizapo form four angalau awe na ujuzi wowote kama userimala, ufundi, upishi, ufugaji wa kuku, kitimoto n.k
•Shule ambazo azifaulishe zipewe adhabu kali kwani wanakula ada tu za wanafunzi bila kutoa elimu bora.


Rejea kwenye hizo rangi nyekundu!
Ingawa mie si Dk kawambwa naomba nikujibu kama ifuatavyo kama mdau, Toka mwaka 2009, assessment system ya nchi yetu imebadilika na kutegemea continuous assessment na final assessment ambayo inatolewa na baraza la mitihani, Kwa maana hiyo hizo failures zote zimejumlishwa na mitihani waliyokuwa wakifanya katika shule zao. Sikumbuki vizuri secondari ni asilimia ngapi, lakini kwenye vyuo vya ualimu mazoezi ya madarasani na mitihani ya ndani ni 50% na baraza nalo lina 50% jumla ni 100%
Sasa tuition zikifutwa walimu watakula wapi? huo mshahara wa mwl unatosha wiki moja tu, au mbili unakuwa umekwisha sasa unategemea mwalimu afundishe akiwa na njaa na familia ikifa na njaa? Walimu wengi wanafundisha tuition si kwa kupenda bali ni shida tu, ni njia ya kuongeza kipato ili angalau waweze kumudu maisha ya kila siku
 
kawambwa inabidi aingilie hili

hawezi kukaa kimya ili hali watu wanalazimishwa kuwa na network ya voda kupata matokeo.

Tunajua fika kuwa walalahoi wengi network yao ni tigo , hivi waziri kivuli wa elimu wa cuf na chadema mbona wako kimya?
ahahah!! Hapa mchemsho. Hii ni huduma inayotolewa na mtandao wowote ukitaka, unaomba ridhaa tu necta-kama magazeti yafanyavyo. Kila mtandao huanzisha huduma zake mbalimbali kwa minajiri ya kuvutia wateja wake. Hoja inayotaka kujionesha hapa ni kuwa kuna mkataba pengine voda wamepewa na wengine kunyimwa; mi sidhani hiyo ndo direction; hoja ni kuwa voda wameomba waunganishe kutoa huduma hiyo kwa wateja wao. Sasa tuombe na mitandao mingine nayo iombe uwezekano huo namna ya ku-configarate mitandao yao ili watumiaji wao nao wanufaike!!!!!! HII NI BIASHARA HURIA, HUWE MLAZIMISHA MTOA MTANDAO KUWA LAZIMA NAWE UTANGAZE MATOKEO YA F.4; AU KULAZIMISHA GAZETI FULANI. NADHANI WENYE VYOMBO HUSIKA HUOMBA RIDHAA ILI KUFIKISHA HUDUMA KWA UMMA. SASA TIGO, AIRTEL,ZANTEL. ETC MKO WAPI JAMANI????
 
Maskini Shule Yangu Azania, umefikia kiwango hiki?

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

CSEE 2010 EXAMINATION RESULTS​



P0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL CENTRE <H3>DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 0 DIV-IV = 10 FLD = 2


Hussein Mwinyi na alumni wengine wa Azania fanyeni hima kuiokoa shule yenu iliyowapa ujiko hadi kuwa hivi mlivyo. Msiiache shule yenu itumbukie shimoni hivi wakati nyie mkishuhudia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
</H3>
 
Hiyo ni Azania CENTRE(kwa private candidates tu).See the prefix P before the centre code.Azania sec itakuwa na prefix S.Go figure..
 
CSEE 2010 EXAMINATION RESULTS

S0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 56 DIV-II = 62 DIV-III = 122 DIV-IV = 207 FLD = 159

Hata hivyo matokeo sio mazuri kiazania ninayoijua mimi
 
Azania original ni hapa

S0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL


DIV-I = 56 DIV-II = 62 DIV-III = 122 DIV-IV = 207 FLD = 159
 
Masikini shule yangu tulikuwa hatupigi mizinga namna hii, japo GORA tulikuwa tunaenda kuchungulia MENDE. Wakati Ngayoma irigi lilochanganywa na mafuta ya taa zikifanya kazi

S0104 BWIRU BOYS SECONDARY SCHOOL


DIV-I = 12 DIV-II = 13 DIV-III = 28 DIV-IV = 63 FLD = 31
 
Maskini Shule Yangu Azania, umefikia kiwango hiki?

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

CSEE 2010 EXAMINATION RESULTS​



P0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL CENTRE <H3>DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 0 DIV-IV = 10 FLD = 2


Hussein Mwinyi na alumni wengine wa Azania fanyeni hima kuiokoa shule yenu iliyowapa ujiko hadi kuwa hivi mlivyo. Msiiache shule yenu itumbukie shimoni hivi wakati nyie mkishuhudia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
</H3>

S0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 56 DIV-II = 62 DIV-III = 122 DIV-IV = 207 FLD = 159
SOURCE: NECTA

Azania wanaporomoka kila mwaka, wale Alumni wa Azania inatuuma sana hali hii!​
 
Azania original ni hapa

S0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL


DIV-I = 56 DIV-II = 62 DIV-III = 122 DIV-IV = 207 FLD = 159

hayo ni matokeo ya aibu sana 159FLD, ni hatari kubwa
 
Back
Top Bottom