wadau nielekezeni nifanyeje, website ya necta hayadisplay. Ni ufedhuli wametufanyia wananchi? Nina madogo zangu nashindwa kuona matokeo yao, na niko ulaya. Hawa necta wana wazimu? Halafu mbona hawajayatangaza?
Mafisadi wanapeana tenda!Nothing new there!
1. Wajameni, hili nalo litasaidiaje watoto kufaulu kidato cha nne?
2. Shule kama haitoi elimu bora, usimpeleke mwanao. Sasa mwanao kashindwa interview kwenye shule nzuri (nyingi za Katoliki) inabidi umpeleke popote; na matunda yake ndiyo hayo. Lingine ni kwamba shule nzuri gharama yake ni kubwa, hivyo ukichagua gharama ndogo si budi hukubali matokeo.
mkuu naona unajaribu saana ku divert issue..hamna mtu anayelalamika majibu kutopatikana kwa wananchi..issue ni kwamba iweje wizara iwatumie voda peke yake?? Na pili kwanini voda icharge watu wakati wizara ina budget maalum ya kutangazia wanafunzi kama wanavyofanya kwenye magazeti? Unachoshindwa kuelewa wewe ni nini ??
Wakuu, Mi niefuatilia matokeo ya Form four yanatiusha sana, kiwango kimeshuka sana mwaka huu. Ila kuna mambo mengi sana yanachangia
•Kumjaribu mtu kwa masaa 2-3 ni uonevu mkubwa. Inawezekana mwanafunzi akawa anfanya vizuri sana darasani laniki siku ya mtihani akawa hajisikii vizuri. Cha kufanya ni kwamba, NECTA ingeanzisha utaratibu mpya wa kutahini wanafunzi kwa awamu mbili. Moja kuchukua wastani wa miaka yote mine na uwe na uzito wa alama 30%, then mtihani wa mwisho uwe na uzito wa alama 70%. Hata vyuo wanafanya hivi pia. Waanade form za kujazwa ambazo pia mkurugenzi wa elimu wilaya na kanda atazikagua ili kupunguza degree ya kuchakachua. Hii itasaidia pia wanafunzi kusoma kwa bidii.
•Serikali kuangalia upya utitiri wa mashule yanayofunguliwa yasiyo na ubora wala walimu wa kudumu.
•Kuwe na Library ya kujisomea shuleni, shule nyingi za kata hazina library.
•Kupiga marufuku Tuition zote na kupitisha sheria kufanya kitendo hiki kua kosa la jinai.
•Kufanya elimu ya form Six kua ya lazima.
•Kubadilisha mitaala shule ili kumwezesha mwanafunzi pindi amalizapo form four angalau awe na ujuzi wowote kama userimala, ufundi, upishi, ufugaji wa kuku, kitimoto n.k
•Shule ambazo azifaulishe zipewe adhabu kali kwani wanakula ada tu za wanafunzi bila kutoa elimu bora.
ahahah!! Hapa mchemsho. Hii ni huduma inayotolewa na mtandao wowote ukitaka, unaomba ridhaa tu necta-kama magazeti yafanyavyo. Kila mtandao huanzisha huduma zake mbalimbali kwa minajiri ya kuvutia wateja wake. Hoja inayotaka kujionesha hapa ni kuwa kuna mkataba pengine voda wamepewa na wengine kunyimwa; mi sidhani hiyo ndo direction; hoja ni kuwa voda wameomba waunganishe kutoa huduma hiyo kwa wateja wao. Sasa tuombe na mitandao mingine nayo iombe uwezekano huo namna ya ku-configarate mitandao yao ili watumiaji wao nao wanufaike!!!!!! HII NI BIASHARA HURIA, HUWE MLAZIMISHA MTOA MTANDAO KUWA LAZIMA NAWE UTANGAZE MATOKEO YA F.4; AU KULAZIMISHA GAZETI FULANI. NADHANI WENYE VYOMBO HUSIKA HUOMBA RIDHAA ILI KUFIKISHA HUDUMA KWA UMMA. SASA TIGO, AIRTEL,ZANTEL. ETC MKO WAPI JAMANI????kawambwa inabidi aingilie hili
hawezi kukaa kimya ili hali watu wanalazimishwa kuwa na network ya voda kupata matokeo.
Tunajua fika kuwa walalahoi wengi network yao ni tigo , hivi waziri kivuli wa elimu wa cuf na chadema mbona wako kimya?
Maskini Shule Yangu Azania, umefikia kiwango hiki?
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
CSEE 2010 EXAMINATION RESULTS
P0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL CENTRE <H3>DIV-I = 0 DIV-II = 0 DIV-III = 0 DIV-IV = 10 FLD = 2
Hussein Mwinyi na alumni wengine wa Azania fanyeni hima kuiokoa shule yenu iliyowapa ujiko hadi kuwa hivi mlivyo. Msiiache shule yenu itumbukie shimoni hivi wakati nyie mkishuhudia!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
</H3>
Azania original ni hapa
S0101 AZANIA SECONDARY SCHOOL
DIV-I = 56 DIV-II = 62 DIV-III = 122 DIV-IV = 207 FLD = 159