Matokeo ya Kidato cha Sita kwa Mwaka 2019 yametangazwa rasmi leo

Matokeo ya Kidato cha Sita kwa Mwaka 2019 yametangazwa rasmi leo

kwa matokeo hayo MD sidhani, maana muhimbili mwaka jana almost waliopata mwisho 1.6 angalau ndo waliweza kupenya UDOM baadhi waliokuwa na 1.7 walipata bahati zao.
Ila sijajua kwa mwaka huu maana kuna kuna chuo kingine UDSM mbeya campus nahisi hadi za 1.8 zinaweza kupata mwanya.
Hapana sisemei muhas hapo najua hawezi pata maana mi nlsoma miaka hyo na ilkua ni best students tu

Sema nauliza kwa vyuo vya serikali kwanza kama anaweza kupata !
 
kwa matokeo hayo MD sidhani, maana muhimbili mwaka jana almost waliopata mwisho 1.6 angalau ndo waliweza kupenya UDOM baadhi waliokuwa na 1.7 walipata bahati zao.
Ila sijajua kwa mwaka huu maana kuna kuna chuo kingine UDSM mbeya campus nahisi hadi za 1.8 zinaweza kupata mwanya.
Kwani udom mwaka jana mwisho walchukua ngapi

Na je hicho cha mbeya mwisho walchukua ngapi

Vya private si rahisi kupata au ,?
 
Kuna dogo kapata

Physics B

Chem C

Bios C

Anaweza pata chuo cha udaktari bongo ukitoa muhimbili cha serikali , sijui hata admissions zmekaaje miaka hiki

Msaada tafadhali
Hapo mzee hawez pata MD maana kwasasa vyuo karibia vyote wanatumia vigezo sawa kudahiri na pia ukizingatia na competition. But ajaribu tu hata vyuo vya nje anapata kiurahis kabisa bongo siasa nyingi
 
Mkuu yaani huwezi kuamini, kule NACTE ambapo viana wetuwanaomba nafasi za Masomo, kuna namba za simu zaidi ya 11 lakini hakuna anayepoke. Matokeo ya Kidayp cha sita yaliyotoka leo NACTE hawana na ukiingiza namba wanasema

"Error! Provided Index/Registration number and Examination/Graduation Year not found in our database, check them and try again or Contact the your institution and advice them to submit your details to NACTE (Code 4001)"

Tulitarajia wao wawe wa kwanza kuwa nayo ili iwe rahisi sisi kuomba lakini ndugu wapo tu wanakula shushu wala mtu hapokei. Namba zenywewe hizo hapo chini. Pigeni muone. Labda watazipokea wakijiona hapa.

"For any enquiries please call NACTE on +255 22 2780077, +255 22 2780312, +255 719 222 846, +255 787 050 389, +255 768 614 045 or write to admissions@nacte.go.tz
Zonal Contacts: Northern Zone - 0658444556/0658444557, Central Zone - 0658444558/0658444559, Lake Zone - 0658444560/0658444562"


Pigeni mnisaidie.
Ungewafungulia uzi wao special ndio ingekuwa vizuri ..huku hawawezi ona
 
Graduate wajao .. .msome kozi za kujiajiri madogo huku hali ni tete.
 
Hawa madogo nao wamalize kusoma... Dingi niko anti-book tunachanganyana akili tu.

Huyu vipi huyu... Niandae pesa au nimkabidhi mtaji.

General studies - E.
History - S
Kiswahili - D
Language - D

Ni dvsn 3 ya 14.
Huyo anaenda chuo kabisa sababu amekidhi viwango vya TCU ..kuwa na principal pass mbili(Yaani kuwa na D Mbili na kuendelea) hivyo mwambie aanze kuomba mkopo wa chuo kikuu ..maana dirisha limeshafunguliwa la kuomba mkopo
 
Hapana achana na MUHAS

vyuo vingine vya serikali
Kwa serikali kwa kozi ya md hapo inakua ngumu kwa hayo matokeo.labda ajaribu kozi zingine kama hizi hapa chini
1151234
1151235
 
Pia NACTE kwa sasa bado hawajafungua dirisha la maombi. Matokeo ndio yametoka leo itabidi mifumo iwekwe sawa ili isomane ni jambo linachukua muda kidogo the same apply to vyuo chini ya TCU na HESLB
NACTE wameshafungua zamani sana fatilia mkuu
 
Huyo anaenda chuo kabisa sababu amekidhi viwango vya TCU ..kuwa na principal pass mbili(Yaani kuwa na D Mbili na kuendelea) hivyo mwambie aanze kuomba mkopo wa chuo kikuu ..maana dirisha limeshafunguliwa la kuomba mkopo
Competition hapa itamzuia japo ka'qualify.
 
Hapana sisemei muhas hapo najua hawezi pata maana mi nlsoma miaka hyo na ilkua ni best students tu

Sema nauliza kwa vyuo vya serikali kwanza kama anaweza kupata !

2012 naingia chuo, walichukua hafi washkaji zangu walikua na 2.10

Japo mwaka jana kuna dogo alikua na 1.8 alitemwa Muhas, tungoje mwaka huu

Admi ya Muhas ni 200+ kwa MD, nadhani huwa wanaangalia na background ya Olevel

Hapana, tunafanana kesi, pia dogo ana 1.8, Phys C, Bio C, Chem B
 
Ripoti ya 2019 sijaiona
Ila ya 2018 kilimanjaro tulikuwa wa 6 wakati kagera mlikuwa 14
Pia tunaongoza kwa kuwa na shule nyingi both advance na ordinary
WAITU NYEGERA View attachment 1151177
Pemba Kusini na Pemba Kaskazini masikini wana shule nne nne tu lakini ndiyo wameshika mkia dah [emoji24][emoji24]
 
Hapo mzee hawez pata MD maana kwasasa vyuo karibia vyote wanatumia vigezo sawa kudahiri na pia ukizingatia na competition. But ajaribu tu hata vyuo vya nje anapata kiurahis kabisa bongo siasa nyingi
Wanatumia vigezo vipi na kwa nini akose ?? !

Admission si eight points au

Mi sisemei muhas mzee
 
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019

Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74.
Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.

Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082.

Katibu mtendaji huyo amesema kati ya watahiniwa 91,298 waliosajiliwa kufanya mtihani , watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani na watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa na utoro.

Dk Msonde amesema watahiniwa wa shule, kati ya watahiniwa 80,216 waliosajiliwa, watahiniwa 79,770 sawa na asilimia 99,44 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 33,883 sawa na asilimia 99.57 na wavulana 45,887 sawa asilimia 99.35. Watahiniwa 446 sawa na asilimia 0.56 hawakufanya mtihani.

Amesema watahiniwa wa kujitegemea kati ya11,082 waliosajiliwa, 10,231 sawa na asilimia 92.32 walifanya mtihani na watahiniwa 851 sawa na asilimia 7.68 hawakufanya.

“Jumla ya watahiniwa 88,069 sawa na asilimia 98.32 ya watahiniwa waliofanya mtihani wamefaulu,” amesema Msonde
Haya wasalimie japani....tumeishajua ulipo.
 
Back
Top Bottom