Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wajinga kweli, sasa wavumilie tu sababu kuna vitu bi mkubwa anazingua na atakula spana kama kawaWanasema tukazikwe nae Chato, dah
Tusi liko Wapi Mpwa? Tozo ni tusi? Kwahio tunaliPIA MATUSI? I don't see any logic kwenye hili, mbona Maji ya kiroba yaliiitwa Kandoro? Kama uko Dar utakua unanielewa, mbona Kandoro Hadi anakufa hajawahi kuwa mkali kisa Maji ya lowest quality yanaitwa Kandoro? Mbona hakukua na issue kama hizi? Kama kweli Tozo ni kitu chema basi we need to be proud kumuita Hivyo kama muasisi Wake...Kwani mawazo tofauti ni kuwatukana wengine?
Akiitwa hivyo jua kazingua mbona ya sifa hamlalamiki.Tabia hii sio utamaduni wa mtanzania
Kuheshimu watawala hapana lkn kuheshimu viongozi ni kweli nimo kwani ni kosa?Ukitaka kuwa rais ujue kuwa rais umekubali kuitwa majina ya ajabu, kwa haki na bila haki.
Watanzania wengi tatizo lao wanaheshimu sana watawala. Hilo ndilo tatizo.
Na wewe ni mfano wa tatizo hilo.
We acha Ukenge tusitishane.Sawa utakula matusi yako
Mimi CCM damu damu, ila Rais Samia anachukiwa kuzidi hata Dkt Kikwete. Yaani sasa hivi Rais Samia kila hotuba yake watanzania wanasonya. Yaani hili la tozo ni baya ila kuna baya zaidi la chanjo ya COVID-19 ambayo mijini wameogopa wameenda kuwatishia watu vijijini na watu wengi sana wamekufa huko vijijini tangu aanzishe kampeni yake ya chanjo. Inakuwa hivi, watu wa vijijini ni elimu duni, wahudumu wa afya wanakataa kuwapa huduma yeyote bila chanjo, hivyo wengine wanaogopa chanjo mtu anaona bora afe, wengine inabidi wachanje na hatujui madhara yake. Hivyo Rais Samia hilo nalo alijue kuwa chuki iliyopo juu yake ni mbaya sana ktk nchi hii haijawahi tokea maana yeye ndiye kazitafuta. Mfano hiliNawasalimu kwa jina la JMT
Watanzania ni watu wakulalamika Kila kitu. Hawana jema Wala shukrani kwa kweli.
Ninasikitishwa sana na matusi, kejeli na majina ya hovyo hovyo anayopewa AMIRI JESHI MKUU, Rais na Mama yetu mpendwa SAMIA hasa hili jina la kipuuzi kabisa HETI mama TOZO mara nchi yetu imepachikwa TOZONIA hawa wapuuzi wanaudhi sana.
Nimeamini watanzania wachache hasa wajiitao upinzani wanautumia uhuru wao vibaya.
Ukiacha urais mama SAMIA ni mtanzania anayepaswa kuheshimiwa kama mtanzania mwingine, kumkejeli na kumtukana hovyo si sawa kabisa.
Mama SAMIA ni nguli na jabali la siasa Tanzania na AFRIKA nina amini kejeli matusi na Majina haya ya hovyo hayawezi kusababisha ashindwe kuwatumikia na kuwaletea maendeleo watanzania, atawapuuza Wapuuzi hao.
lkn Hoja yangu ni kwamba kwa Nini watanzania baadhi yetu tunashindwa kuheshimiana tukipewa uhuru tunageuka watukanaji, waasi, na wasioheshimuna kujali utu wa wengine.
Kumbukeni uhuru ni Bora kuliko tozo ni lazima tujitolee kuijenga Tanzania yetu.
Pia tunakupongeza sana mama HATUA ZOTE zinazohusu mchakato wa SENSAYA WATU NA MAKAZI zinaendelea vizuri sana wananchi wako tayari kuhesabiwa.
KWELI kabisa maendeleo ya wengi yanaletwa na wengi yanaliwa na wachacheKweli maendeleo ya wengi hayaletwi na wachache
Chanjo ni hiari Kijiji Gani wanalazimishwa mkuuMimi CCM damu damu, ila Rais Samia anachukiwa kuzidi hata Dkt Kikwete. Yaani sasa hivi Rais Samia kila hotuba yake watanzania wanasonya. Yaani hili la tozo ni baya ila kuna baya zaidi la chanjo ya COVID-19 ambayo mijini wameogopa wameenda kuwatishia watu vijijini na watu wengi sana wamekufa huko vijijini tangu aanzishe kampeni yake ya chanjo. Inakuwa hivi, watu wa vijijini ni elimu duni, wahudumu wa afya wanakataa kuwapa huduma yeyote bila chanjo, hivyo wengine wanaogopa chanjo mtu anaona bora afe, wengine inabidi wachanje na hatujui madhara yake. Hivyo Rais Samia hilo nalo alijue kuwa chuki iliyopo juu yake ni mbaya sana ktk nchi hii haijawahi tokea maana yeye ndiye kazitafuta. Mfano hili
la chanjo mbona Dkt Magufuli alikuwa keshatuambia yeye alipaswa kufuata nyendo zake. Ila kwa sasa yaani ni ngumu sana Rais Samia kupata kura 2025 na kibaya sana anawadharau watu wa kanda ya ziwa na kuwabeza kwa kuonesha Dkt Magufuli alikuwa hapendwi. Asichokijua Rais Samia kuwa kanda ya ziwa siyo wana harakati na siku zote maamuzi yao huwa ya chinichini.
Wewe unaona ni halali kumtoza mtu , kutoa fedha kwenye account yake ya benki ?!. Mshahara tayari umekatwa kodi. Bado kuitoa benki umtoze ?! Huo ni zaidi ya uwizi ni ujangiliWanaudhi sana
Lakini kwa watanzania majina kama hayo huwa hayamaanishi kwamba ni matusi ! Watanzania wana tabia za mzaha mzaha yaani huwa wanapenda sana utani ! Na wala hii kitu haijaanza kwenye awamu hii tu ! Hata kwenye awamu ya kwanza Mwalimu alipewa majina mengi tu ! Kwa mfano alikuwa akiitwa Haambiliki ! Mchonga meno n.k !! Kwa kifupi wabongo Utani ni sehemu yao ya maisha ! Na hayo wala sio matusi japo mtoa mada anataka kuaminisha watu kwamba mheshimiwa eti anatukanwa ! Sio kweli hata kidogo , Matusi yanajulikana na maneno ya mizaha inajulikana ! Hata watoto wa kitanzania huwa wanawaita Baba zao “ Dingi “ je nalo ni tusi ?? !! Kwa watanzania Usimba na Uyanga ndio maisha yao !! Ni watu wa Utani utani tu wala huwa hawatukanani !!Acha kutumia uhuru vibaya mkuu ukuku wake Nini Sasa, maana hats Mimi sipendi kabisa kuitana Majina ya kuudhi
Kitunguu swaumu mkubwa Mimi duuuu! Umenitusi sana mkuu Mungu anakuona hasira za Nini? TOZO ni kwa ajili ya maendeleo yetu wenyeweVichwa maji kama wewe, Huwa mnapewa teuzi lkn msijue nn Cha kuzifanyia .
Ulichoona wewe ni malalamiko... Ila akili yako imeshindwa hata kuishauri serikali namna gan iwaspunguzie Watanzania hii dhahama.
Kitunguu swaumu Mkubwa wee!!
Kama Kuna changamoto tushauri kistaarabu sio kejeli na majina ya hovyo hovyoWewe unaona ni halali kumtoza mtu , kutoa fedha kwenye account yake ya benki ?!. Mshahara tayari umekatwa kodi. Bado kuitoa benki umtoze ?! Huo ni zaidi ya uwizi ni ujangili
Huwezi kuwabadili watu na tabia zao !! Kama anavyosemaga Bongo Zozo “ Fujo isiyoumiza “ !!Kwani hatuwezi kukosoa bila kupachikana Majina ya hovyo?