Matokeo ya Uhuru kuzidi sana ni ujeuri

Kwani mawazo tofauti ni kuwatukana wengine?
Tusi liko Wapi Mpwa? Tozo ni tusi? Kwahio tunaliPIA MATUSI? I don't see any logic kwenye hili, mbona Maji ya kiroba yaliiitwa Kandoro? Kama uko Dar utakua unanielewa, mbona Kandoro Hadi anakufa hajawahi kuwa mkali kisa Maji ya lowest quality yanaitwa Kandoro? Mbona hakukua na issue kama hizi? Kama kweli Tozo ni kitu chema basi we need to be proud kumuita Hivyo kama muasisi Wake...
 
Ukitaka kuwa rais ujue kuwa rais umekubali kuitwa majina ya ajabu, kwa haki na bila haki.

Watanzania wengi tatizo lao wanaheshimu sana watawala. Hilo ndilo tatizo.

Na wewe ni mfano wa tatizo hilo.
Kuheshimu watawala hapana lkn kuheshimu viongozi ni kweli nimo kwani ni kosa?
 
Mimi CCM damu damu, ila Rais Samia anachukiwa kuzidi hata Dkt Kikwete. Yaani sasa hivi Rais Samia kila hotuba yake watanzania wanasonya. Yaani hili la tozo ni baya ila kuna baya zaidi la chanjo ya COVID-19 ambayo mijini wameogopa wameenda kuwatishia watu vijijini na watu wengi sana wamekufa huko vijijini tangu aanzishe kampeni yake ya chanjo. Inakuwa hivi, watu wa vijijini ni elimu duni, wahudumu wa afya wanakataa kuwapa huduma yeyote bila chanjo, hivyo wengine wanaogopa chanjo mtu anaona bora afe, wengine inabidi wachanje na hatujui madhara yake. Hivyo Rais Samia hilo nalo alijue kuwa chuki iliyopo juu yake ni mbaya sana ktk nchi hii haijawahi tokea maana yeye ndiye kazitafuta. Mfano hili
la chanjo mbona Dkt Magufuli alikuwa keshatuambia yeye alipaswa kufuata nyendo zake. Ila kwa sasa yaani ni ngumu sana Rais Samia kupata kura 2025 na kibaya sana anawadharau watu wa kanda ya ziwa na kuwabeza kwa kuonesha Dkt Magufuli alikuwa hapendwi. Asichokijua Rais Samia kuwa kanda ya ziwa siyo wana harakati na siku zote maamuzi yao huwa ya chinichini.
 
C
Chanjo ni hiari Kijiji Gani wanalazimishwa mkuu
 
Acha kutumia uhuru vibaya mkuu ukuku wake Nini Sasa, maana hats Mimi sipendi kabisa kuitana Majina ya kuudhi
Lakini kwa watanzania majina kama hayo huwa hayamaanishi kwamba ni matusi ! Watanzania wana tabia za mzaha mzaha yaani huwa wanapenda sana utani ! Na wala hii kitu haijaanza kwenye awamu hii tu ! Hata kwenye awamu ya kwanza Mwalimu alipewa majina mengi tu ! Kwa mfano alikuwa akiitwa Haambiliki ! Mchonga meno n.k !! Kwa kifupi wabongo Utani ni sehemu yao ya maisha ! Na hayo wala sio matusi japo mtoa mada anataka kuaminisha watu kwamba mheshimiwa eti anatukanwa ! Sio kweli hata kidogo , Matusi yanajulikana na maneno ya mizaha inajulikana ! Hata watoto wa kitanzania huwa wanawaita Baba zao “ Dingi “ je nalo ni tusi ?? !! Kwa watanzania Usimba na Uyanga ndio maisha yao !! Ni watu wa Utani utani tu wala huwa hawatukanani !!
 
Vichwa maji kama wewe, Huwa mnapewa teuzi lkn msijue nn Cha kuzifanyia .

Ulichoona wewe ni malalamiko... Ila akili yako imeshindwa hata kuishauri serikali namna gan iwaspunguzie Watanzania hii dhahama.


Kitunguu swaumu Mkubwa wee!!
Kitunguu swaumu mkubwa Mimi duuuu! Umenitusi sana mkuu Mungu anakuona hasira za Nini? TOZO ni kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe
 
Wewe unaona ni halali kumtoza mtu , kutoa fedha kwenye account yake ya benki ?!. Mshahara tayari umekatwa kodi. Bado kuitoa benki umtoze ?! Huo ni zaidi ya uwizi ni ujangili
Kama Kuna changamoto tushauri kistaarabu sio kejeli na majina ya hovyo hovyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…