Matokeo ya Uhuru kuzidi sana ni ujeuri

'Tozonia'....πŸ™„πŸ™„πŸ™„...dah!... Maana yake nini Sasa ?
 
Ninachompendea Rais Samia Suluhu yeye hajari maneno ya watu anachojari ni utekelezaji na kuleta maendeleo kwa hao hao wananchi wanaomdhihaki hii inadhibitisha uimara wake
 
Unaujua ule msemo wa mti wenye matunda ndio unapigwa mawe sasa Rais Samia anaifungua Tanzania subiri baada ya muda kidogo utashuhudia Tanzania itakua na kila kitu kama maji yamefika mpaka vijijini umeme umefika pia miundombinu imeboleshwa
 
Kuheshimu watawala hapana lkn kuheshimu viongozi ni kweli nimo kwani ni kosa?
Nakwambia hivi, Africa tuna tatizo la heshima ya kijinga.

Sio kwa watawala na viongozi tu, hta kwa wazazi.

Mtu anatakiwa kuwa na autonomy, kuhoji, kukataa ujinga, hata ukiwa umesemwa na mtawala, kiongozi au hata mzazi.

Unakubali au unakataa?
 
Ninachompendea Rais Samia Suluhu yeye hajari maneno ya watu anachojari ni utekelezaji na kuleta maendeleo kwa hao hao wananchi wanaomdhihaki hii inadhibitisha uimara wake
Rais Samia ni kati ya marais walio sensitive sana kuhusu maneno ya watu.

Na ni rahisi sana kutolewa relini na watu kwa maneno.Juzi hapa kagombana na wapiga picha wake hadharani kwa sababu ya maneno ya watu wamesema mikutano yake haihudhuriwi na watu wengi.

Hii habari ya kwamba rais Samia hajali maneno ya watu si kweli.

Siyo tu hajali, anayasikia na kujibizana nao kutoka jukwaani kama muimba taarabu.
 
Kwani hatuwezi kukosoa bila kupachikana Majina ya hovyo?
Hivi wewe unataka kuchagulia watu majina ya kumwita Chief hangaya. Mwambie aondoe hizo tozo kama Hilo jina utalisikia. Na walivyo wajinga wakasuburia bunge la Budget kuisha ndo wanalianzisha Sasa hivi.

Make walijua wakilianzisha kipindi Cha budget watu wangepiga sana kelele. Yaani Ina maana hakuna hata mbuge mmoja aliyeona aina hii mpya ya Kodi ya tozo. Walificha wakajua watu watapiga kelele
 
TOZO ni jina la hovyo? Kwahio tunalipishwa vitu vya hovyo? Wisdom will kill me [emoji13]
Haya majina wanayataka wenyewe make huitwa pale wanapofanya kinyume na katiba yetu na matakwa ya wananchi
 
1. Sio jabali wala nguli wa siasa Tanzania
2. Umekosea sana kuwatukana watu ambao wewe unapenda wamkosoe kwa staha huyo rais
3. Ukijiita nguli na jabali la siasa hutakiwi kulalamika kutokana na kukosolewa isivyo staha ila jirekebishe kwa matendo yako watakuheshimu tu
4. Kuongozwa na mtu haimaanishe wewe ndio una akili nyingi, umesoma sana, unayafahamu mambo kwa kiwango cha juu sio kweli
5. Wanaolalamika wameathiriwa vibaya na hicho unachodai ni kejeli ila kwa kuwa hawana nguvu na uwezo wa kusema na wakasikilizwa hapo ndio unadai kudhalilishwa
6. Mbona enzi za JPM ambaye ndio aliongoza kudhalilishwa hukuwahi kukemea nini?
7. Mbona viongozi hao hao ambao walifanya kazi chini ya JPM ndio ni miongoni mwa watu wanaomkejeli hayati JPM ambaye kwa sasa hayupo duniani kujitetea na husemi chochote wakati ukijua ana familia, marafiki, ndugu na hadhi ya urasi kwamba wanaumizwa kutokana na kejeli hizo mpaka wengine wakidai wanaomkumbuka kwa mazuri yake basi wakazikwe naye Chato pia hukemei?

Waacheni wananchi watoe ya moyoni maana hawana tumaini tena...........................
 
Acha kuwalaumu upinzani, unashindwa kupunguza mfumuko wa Bei na gharama za Maisha wananchi wasilalamike? Unaongeza tozo kila kukicha lakini bei ya mafuta inapanda Kika uchao.
Sijawalaumu upinzani nimesema baadhi ya watanzania mkuu
 
Wanakuudhi wewe unayedhani Tanzania ni Mali binafsi ya CCM. Unaongeza tozo huku unashidwa kupunguza mfumuko wa Bei. Acheni kuwadharau watanzania kisa ni wapole, tumieni upole kuwaletea unafuu wa Maisha.
Gharama za maisha haziwez kuwa kostanti Kila mwaka mkuu Tanzania sio kisiwa
 
Wanakuudhi wewe unayedhani Tanzania ni Mali binafsi ya CCM. Unaongeza tozo huku unashidwa kupunguza mfumuko wa Bei. Acheni kuwadharau watanzania kisa ni wapole, tumieni upole kuwaletea unafuu wa Maisha.
Nafuu inaletwa na SS watanzania wenyewe mkuu kwa kukaza mkanda na hizi TOZO ni kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya watanzania hawa hawa
 
Nchi ni yetu lazima tuijenge wenyewe hayupo wa kufanya baraka yetu
Watanzania wamevumilia mwishowe wameamua kutema nyongo. Unakopa kila uchao na tozo juu, huku Kodi mnasema imeongezeka. Jana mama yako alipata fresh kwenye Twitter watu walimpa makavu mpaka Msigwa akajitokezaza kutoa ufafanuzi.
 
Rais wetu amejishusha kwa watanzania ni mnyenyekevu TOZO ni kwa ajili ya maendeleo ya watanzania, magufuli ndie aliongoza kwa kuwakejeli na kuwatukana watanzania pia hata viongoz aliowateua mwenyewe na alijitetea mwenyewe kama ulivyoshuhudia mama SAMIA ni mpole mnamtukana, watanzania wachache mnatuharibia ustaarabu na utamaduni wetu jambo ambalo sio jema
 
Umesahau kuweka namba ya simu mwisho wa chapisho lako
Hayo mambo yalikua ya enzi za giza mkuu...sasa hivi kama haujashikwa mkono teuzi utasikia kwenye bomba...πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Unashambulia zega la nyuki halafu hutaki kungatwa. Nyie ibeni kura watanzania hawana shida ila kuingilia uchumi wao kininga na kitapeli mtatukanwa mpaka mkimbie. Na hivi hakuna ajira watu wamechoka mtakubali tu.
Serikali haiwezi kuwaajiri watanzania wote kwa mkupuo ni awamu kwa awamu
 
Wizi wa kura zipi kama ni uchaguzi Dunia yote ni mashahidi kwamba ulikuwa huru na haki Na ccm ilishinda wa kishindo na halali kama unaushahidi wa wizi mahakama zetu zipi na zinatenda haki kwa nn mlielie mutandaoni Kila mwaka wa uchaguzi?
 
Acha kujifnya nchi ya babaako. Akina Nyerer waligombea Uhuru wa maoni, wewe unaleta mambo ya ukoloni eti chunga ulimi wako. Wewe Ni Nani. Mnatishia wananchi lakini baada ya miaka mitano mnakuja kupiga magoti mnaomba kura
Mama ni mama yko mzazi tu mbwa wewe kutoka nchi ya TOZONIA
Hasira za nn mkuu TOZO ni kwa ajili ya mipango ya maendeleo ya watanzania
 
Hapana mkuu sio unafiki ninaumia sana na hizi Tania ya kumtukana viongoz ambalo hawalali kuhangaikia shida za watanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…