Matokeo ya utafiti kuhusu madai ya wanawake wa Kitanzania kujiuza katika mitandao ya kijamii

Matokeo ya utafiti kuhusu madai ya wanawake wa Kitanzania kujiuza katika mitandao ya kijamii

Dr. Wansegamila

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2012
Posts
2,968
Reaction score
8,139
Wakuu salama?

Kuanzia mwezi Septemba mwaka huu, niliongoza utafiti usio rasmi juu ya madai ya mabinti wa Kitanzania kujiuza kwenye mitandao ya kijamii ya Badoo, Tinder na Hitwe.

Maswali ya utafiti (Research questions):
1. Je, ni kweli kuwa mabinti wa Kitanzania walio katika mitandao ya Badoo, Tinder na Hitwe wanajiuza kimwili?

2. Je, mabinti wa Kitanzania wanaojiuza kimwili (kama wapo kulingana na majibu ya swali la kwanza hapo juu) katika mitandao ya badoo, tinder na hitwe ni wahitimu wa vyuo vikuu?

Malengo ya utafiti (objectives)
1. Kufahamu kama mabinti wa Kitanzania walio katika mitandao ya Badoo, Tinder na hitwe wanafanya biashara ya kuuza miili yao kwa matumizi ya ngono.

2. Kufahamu kama mabinti wa Kitanzania wanaojiuza katika mitandao ya badoo, Tinder na Hitwe (kama wapo) ni wahitimu wa vyuo vikuu?

Njia iliyotumika (Methodology)
Jumla ya Profiles 120 zenye majina na picha za mabinti kutoka mitandao ya badoo (40), tinder (40) na hitwe (40) walitumiwa meseji na mmoja wa wachunguzi wetu ambae alitengeneza 'profile' za kiume kwenye mitandao hiyo

Meseji ya kwanza ilikua ni "Hi mrembo!". Baada ya meseji hii kujibiwa na mhusika, maongezi yalikua yakiendelea kwa mchunguzi wetu kumwambia kuwa, " I wanna have some fun with you, how much will it cost me?"

"Profiles" zilikua zinachaguliwa "randomly" ambapo wachunguzi wetu walikua wanaongozwa na formula ambayo imesetiwa kabla ya kuanza zoezi kuchagua profiles za kuzitumia meseji in a random fashion.

Hitimisho la maongezi haya ni kwa mchunguzi wetu kufikia makubaliano na mhusika, na binti kutoa namba ya simu kwa mawasiliano zaidi ya namna ya kukutana. Kwa utafiti huu, binti kukubaliana BEI, muda na sehemu ya kukutana na mchunguzi wetu PAMOJA NA binti kutoa namba ya simu (ni lazima vitu hivi VYOTE vitimie), kulihesabika kama 'confirmatory test' ya binti kujiuza.

Kwa upande wa lengo la pili la utafiti huu kubaini kama wasichana wa Kitanzania wanaojiuza kwenye mitandao ya kijamii (kama wapo) ni wahitimu wa vyuo vikuu, kigezo kilichotumika ni ufahamu wa lugha ya kingereza kwa binti husika kwa kadri ya "chats" za mhusika na mchunguzi wetu (hii ina limitations zake, lakini ndio ilionekana kuwa ni njia ya haraka zaidi kubaini hilo kwa vigezo vya tafiti hii kwani inategemewa kuwa mhitimu wa chuo kikuu wa Kitanzania angalau aweze kumudu kingereza cha kuandika kwani ndio lugha ya kufundishia nchini kuanzia sekondari hadi chuo kikuu)

Matokeo (Results)
Kati ya meseji 120 zilizotumwa na wachunguzi wetu, meseji 109 zilipata majibu, na meseji 11 hazikujibiwa kabisa hadi mwisho wa utafiti. Meseji zilizojibiwa kwa kadri ya mitandao wa kijamii ni kama ifuatavyo; badoo (35), tinder (37) na hitwe (37).

Kati ya meseji 109 zilizojibiwa, iligundulika kuwa wasichana wa Kitanzania 92 (ambayo ni sawa na asilimia 84.4), WANAJIUZA kwani walikubaliana na mchunguzi wetu sehemu, simu na muda wa kukutana, pamoja na kutoa namba ya simu kwa mchunguzi wetu kwa mawasiliano zaidi.

Kati ya hao waliokubali, wasichana 74 (asilimia 80.4 ya waliokubali), walikua tayari kufika eneo la miadi kwa gharama zao, kwa ahadi ya kurejeshewa gharama hiyo na mchunguzi wetu.

Pia, kati ya wasichana 92 ambao walikidhi vigezo vya KUJIUZA kwa kadri ya utafiti huu, iligundulika kuwa 62, ambayo ni sawa na asilimia 67.4 hawamudu lugha ya kingereza (waliomba wachunguzi wetu wabadili lugha na kutumia kiswahili wakati wa chats)-Hivyo basi kuwa na uwezekano mkubwa kuwa hawakufika chuo kikuu.

Majadiliano (discussion)
Hii nakuachia wewe mwana JF

Hitimisho:
Asilimia 84 ya wasichana wa Kitanzania walio kwenye mitandao ya kijamii ya Badoo, Tinder na Hitwe wanajiuza kimwili, na kati ya hao asilimia 67 hawajafika elimu ya chuo kikuu (Pamoja na 'profiles' zao kuonyesha kuwa ni wahitimu au wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini).

Mengineyo
Utafiti huu pia uligundua vitu vingine ambavyo havikwepo kwenye malengo ya awali ya utafiti kama vile:

1. Kati ya wasichana 92 ambao walikidhi vigezo vya kujiuza kwa kadri ya utafiti huu, 81 (asilimia 88) walikubali kuwa wanatoa huduma ya ngono kinyume cha maumbile walipoulizwa na wachunguzi wetu iwapo wanatoa huduma hiyo.

2. Bei ya wastani kwa wasichana wanaojiuza kwa kadri ya makubaliano na wachunguzi wetu ilikua kati ya shilingi 20,000-100,000 kwa usiku mmoja. (Wengine walikua wanatoa bei kwa bao na sio kwa usiku).

3. Kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna wanaojiuza ambao eidha bado wako chini ya uangalizi wa wazazi/walezi au labda hata wake za watu? Kwa sababu kulikua na idadi ya kutosha ya mabinti ambao walisema kuwa wao hawawezi kutoa huduma ya kulala usiku mzima, lakini wanaweza kutoa game mida ya kuanza asubuhi hadi jioni (Hili ni eneo lingine la utafiti kubaini hawa wanaojiuza mitandao ni ni kina nani hasa?)

Je, wapo pia watoto wetu tunaoishi nao majumbani wanafanya hii biashara? pengine na wake za watu? Wazazi na walezi tuwe makini sana kujua nyendo za watoto wetu tunaoishi nao.

Mapungufu ya utafiti huu (limitations)
1. Kuna uwezekano wa kuwepo 'profiles' ambazo zina majina na picha za mabinti, ila ni za wanaume, hasa kwa wale ambao walikataa makubaliano ya kufika eneo la ahadi kukutana na mchunguzi wetu bila kutumiwa nauli-Utafiti huu haukuweza kueliminate hili kwa asilimia 100.

2. Kuna uwezekano pia ya baadhi ya mabinti ambao wanajua kingereza lakini hawakufika chuo kikuu (au kinyume chake pia), hivyo kwa lengo namba mbili la kubaini level ya elimu kwa kigezo cha kingereza inawezekana kutoa matokeo ambayo si uhalisia. Ila utafiti huu uwezo wake umeishia hapa.

Naomba kuwasilisha.
 
Sijui niseme nini

But first ni hongera Kwa utafiti.

Labda niseme now hiyo biashara imeahamia Telegram zaidi.

Halafu wanafunzi wa vyuo hawajiuzi waziwazi sana ingawa nao wapo.

Next time weka profile kama ya mzungu ushangae zaidi.

Huko Telegram kama hujawahi kwenda basi ukienda hutaamini utakachoona
 
Mlitumia njia gani kuchagua hizo profiles?

Labda mkiona picha ya profile MTU kavaa kihasara hasara. Katika maelfu ya profile zilizopo.

Nini tafsiri ya kujiuza kwa mujibu was utafiti wenu?
Swali zuri sana ambalo lina address kitu kikubwa kwenye utafiti, bias.

Kuna kitu sijakiongelea kwenye methodology ambacho ni technical, profiles zilikua zinachaguliwa na wachunguzi wetu randomly kwa kufuata a specified formula. Hivyo selection ilikua random kulingana na formula iliyokua set ambayo ndio ilikua inamuongoza mchunguzi wetu (eg after every three profiles, the fourth profile has to be picked).

Swali lako la pili nimelijibu kwenye maelezo yangu mkuu, angalia sehemu ya Njia iliyotumika (Methodology)
Mzingo
 
Sijui niseme nini
But first ni hongera Kwa utafiti..

Labda niseme now hiyo biashara imeahamia telegram zaidi..
Halafu wanafunzi wa vyuo hawajiuzi waziwazi sana ingawa nao wapo..

Next time weka profile kama ya mzungu ushangae zaidi....

Huko telegram kama hujawahi kwenda basi ukienda hutaamini utakachoona
Ahsante sana mkuu.

Next time nitashawishi team yangu tufanye a bigger research kwenye telegram kama ulivyosuggest, maana wadau wengi wameongea kama ulivyosema wewe.

Shukrani sana.
 
Hizi tafiti ziende na telegram. Kule kuna uchafu sana na lugha ya kificho ya k.toleo la pili na hakuna shoga 😂😂

Hii dunia ya utandawazi tujitahidi kuwapa maadili mema watoto wetu huko tuendako ni kubaya sana hasa life style ya walezi wa siku hizi.

Wazazi tuwe makini sana na mienendo ya watoto wetu na hizi smartphone.
 
Kama hutojali, ongeza na hili.

Wanaojiuza ni kweli wanatoka familia zenye Hali ngumu??Au ni kama lifestyle?

Wapo wake za watu? Wachumba?

Wanaojiuza kwenye mitandao na wanajiuza mitaani pia? Au mitaani wanafanya shughuli zingine? Wanazuga?

Je, kujiuza kumewawezesha kitu gani?
 
Nipe link mkuu nikafanye artificial intelligence...
Sijui niseme nini
But first ni hongera Kwa utafiti..

Labda niseme now hiyo biashara imeahamia telegram zaidi..
Halafu wanafunzi wa vyuo hawajiuzi waziwazi sana ingawa nao wapo..

Next time weka profile kama ya mzungu ushangae zaidi....

Huko telegram kama hujawahi kwenda basi ukienda hutaamini utakachoona
 
Back
Top Bottom