Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema anawasiliana na Familia ya Mtoto Anna Zambi kwa ajili ya kuangalia namna ya kumuendeleza kimasomo, baada ya Anna kufaulu kwenye matokeo ya kidato cha 4 kwa kupata Division Two ya 20.
"Nashukuru Mungu licha ya wasiwasi mkubwa niliokuwa nao wakati nafanya Mtihani kutokana na kutokuwa na mawasiliano na Wazazi wangu lakini nimefaulu, matarajio yangu yalikuwa kupata Division One naamini bila ule wasiwasi ningepata Division One”- Ameyasema Hayo Anna ZAMBI
"Napenda kusomea Sheria nitimize Wosia wa Marehemu Baba maana Baba alitaka Watoto wake tusomee Sheria ili tutetee Wananchi waliombakiwa kesi, Baba wakati akiwa hai alikuwa Mtumishi wa Serikali alikuwa na Kesi TAKUKURU na alilalamika kosa si lake ”-Anna Zambi -
“Nikianza kidato cha tano nitapenda nichukuliwe kama wanafunzi wengine, yaliyopita yamepita kupewa pole tena ni kukumbushia yaliyopita, nawashukuru wote walionifariji na kuonesha nia ya kunisaidia kimasomo, nawashukuru sana Walimu wangu” - Anna Zambi