Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Nimepiga hesabu za haraka haraka, na kugundua kwamba makampuni ya Bima hukusanya wastani wa Trilioni 3.5 kila mwaka kama malipo ya bima za aina mbali mbali, na pia malipo kwa ajili ya bima (hasa hasa kwa wahindi wanaochoma moto viwanda vyao kwa makusudi) kwa mwaka huwa hayazidi bilioni 100, na ukitoa gharama za uendeshaji utaona inabaki kama trillion 3 hivi.

Sasa najiuliza, hii pesa tunayolazimishwa na matrafiki police huku barabarani kwamba ni lazima tulipe, inaenda serikalini na makampuni kubaki na comission tu au yote inaenda kwa haya makampuni ya Bima?!

==========================

Sasa ninachopendekeza ni hiki, bima zote za third party zilipwe serikalini kupitia wakala wa bima wa taifa, na malipo yatafanywa na wakala huyo kwa hao third party. Hayo matrillion yakaboreshe huduma za elimu, afya na miundombinu.

Ifike mahala tuache kukopa wakati matrilioni yanabebwa na hawa wenye makampuni ya bima tena ni wageni, wanaenda kuwekeza kwao huko. Pendekezo ni hilo, sheria husika zirekebishwe ku-accomodate mtazamo huu mpya, na radical kabisa!

==========================
Update: 17/05/2023

Tundu Lissu - “Pesa yoyote ni kodi”

Ungejiuliza kwanza kwamba ukipata ajali ya gar anaekulipa ni Serikali ama Kampuni ya Bima hapo ndio.utajua inaenda wap

Anyways siku hzi kuna kodi kwenye Bima so serikali inchukua chake hapo
Sasa kwanini serikali ishurutishe raia kuchangia watu binafsi matrilion kila mwaka ilihali yenyewe inakosa hata pesa ya kuboresha miundombinu ya barabara?

Ni kwanini hii pesa ya bima isiende serikalini ili ikasaidie kuboresha huduma za kijamii, na kama mtu akihitaji kulipwa bima afuatilie moja kwa moja serikalini kupitia mawakala wa bima waliopo kila kona? Kwanini tulazimishwe na polisi kuchangia watu binafsi matrilioni kila mwaka?! Why?! Trillion 3 kila mwaka tunalizimishwa kuwalipa, kwnai nchi yao hii?
 
Sasa kwanini serikali ishurutishe raia kuchangia watu binafsi matrilion kila mwaka ilihali yenyewe inakosa hata pesa ya kuboresha miundombinu ya barabara? Ni kwanini hii pesa ya bima isiende serikalini ili ikasaidie kuboresha huduma za kijamii, na kama mtu akihitaji kulipwa bima afuatilie moja kwa moja serikalini kupitia mawakala wa bima waliopo kila kona? Kwanini tulazimishwe na polisi kuchangia watu binafsi matrilioni kila mwaka?! Why?! Trillion 3 kila mwaka tunalizimishwa kuwalipa, kwnai nchi yao hii?!!
Ile third party unayokata umeshawahi kusoma policy yake? Kama utakuwa na muda isome halafu ujisomee sheria ya bima nchini kwetu.
 
Sasa kwanini serikali ishurutishe raia kuchangia watu binafsi matrilion kila mwaka ilihali yenyewe inakosa hata pesa ya kuboresha miundombinu ya barabara? Ni kwanini hii pesa ya bima isiende serikalini ili ikasaidie kuboresha huduma za kijamii, na kama mtu akihitaji kulipwa bima afuatilie moja kwa moja serikalini kupitia mawakala wa bima waliopo kila kona? Kwanini tulazimishwe na polisi kuchangia watu binafsi matrilioni kila mwaka?! Why?! Trillion 3 kila mwaka tunalizimishwa kuwalipa, kwnai nchi yao hii?!!
Serikali haiwezi kufanya biashara na haina ubavu wa kuhudumia aina zote za bima kwa watu wote.

Bima ni biashara kama zingine ambazo faida lazima iwe inaonekana.

Kulazimisha kukata bima ni kukukinga wewe na hasara ya majanga usiyotegemea.

Sawa na vile unalazimishwa kufunga mkanda kwenye gari, kufuata sheria zote za barabarani.

Serikali inafaidika vile hamfi hovyo.
 
Pia kumlimda mhusika wa tatu. Third party asiyehusika na gari lako endapo utafanya maamuzi yatakayosababisha uharibifu.
 
Kuna biashara na biashara, mbona sioni kampuni zikizalisha na kusambaza umeme nchini? Bali wote wanazalisha kama mawakala na kumpa Tanesco? Muda mwingine tuwe tunalegeza ubongo kidogo.
 
Pia kumlimda mhusika wa tatu. Third party asiyehusika na gari lako endapo utafanya maamuzi yatakayosababisha uharibifu.
Nani kabisha hilo, pesa iende serikalini, huyo third party atalindwa tu na serikali, hatuwezi kushindwa kumlinda kama taifa. Kama Umeme hakuna anaeruhusiwa kusambaza, basi hata hii inapaswa iwe chini ya serikali, watu tunalazimishwa kuwalipa watu binafsi trillion 3 kila mwaka kiulaini tu bila jasho, na usipolipa polisi wanakukamata, hivi ni ubongo au makalio tunayotumia kuwaza? Seriously?! Halafu watu wanarudisha kodi ya kichwa ili kuungeza mapato, wakati tumewcha wahindi wanachota tu pesa matrillion kwa kutulazimisha?!
Biashara tangu lini ikawa ya kulazimishana? Huu si ujambazi, kama ni lazima means hii ni kodi kama kodi zingine, sasa iweje mtu binafsi anachukua kodi trillion 3 , sisi ni mataahira??!!
 
Ukitaka kuona umuhimu wa bima usilipe uone....

Magari mengi sana hupata ajali na bima hulipia.
 
Bima ni biashara kama nyingine. Kwa bahati mbaya wengi wanafahamu bima za magari tu, kuna aina chungu nzima za bima, na hizo hubuniwa au kutekelezwa na wajuzi wa bima.

Pia kufanya analsis ya risk na claims si jambo rahisi na kama Serikali itaamua kufanya wao itakuwa na urasimu mkubwa sana. Mfano rahisi ni mtu anayefuatilia mafao yake NSSF, anahitajika kuwa na viambatanishi vingi sana wakati kwa muda wa zaidi ya miaka 30 wamekuwa wakichukua makato yake na teknolojia ipo kubaini kama ni halali kwake kulipwa, just imagine iwe ni bima ya gari yako ya mizigo imepata ajali halafu unahitaji ulipwe au utengenezewe gari na serikali kwa kipindi cha ndani ya mwezi!

Mfano mwingine rahisi, tuna shirika la bima la taifa NIC nalo linafanya biashara ya bima kama makampuni mengine, hushangai halipo hata kwenye top three ya makampuni ya bima yenye mapato makubwa, kwa nini wateja hawalikimbilii?
 
Maada nzuri Sana hata Mimi Nilikuwa najiuliza maswali...mwanzo nilidhani shirika la bima NI Moja TU la taifa nikadhani wao wengine NI mawakala tu
Hivyo ndivyo nilikuwa nadhani na ndivyo inapaswa kuwa, trillion 3 kodi inakusanywa na hao mawakala lakini badala ya kuipeleka shirika la bima la taifa (NIC) wao wanabaki nazo mifukoni, halafu wanakuja kurudisha kodi yabkichwa wakati kodi kuna watu wanakaa nazo hawazifikishi serikalini, trillion 3 kila mwaka, ni pesa ya serikali hii, wao walipaswa wachukua comission tu kwa kazi ya kukusanya waliyofanya, baada ya hapo wapeleke shirika la bima la taifa!
 
Back
Top Bottom