Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

Ukitaka kuona umuhimu wa bima usilipe uone....

Magari mengi sana hupata ajali na bima hulipia.
Nani kasema bima haina umuhimu, tunachosema hiyo bima ikusanywe na haya makampuni kama mawakala tu, ila sio wao ndio wachukue hayo mapato, wao wapewe comission kwa kazi ya ukusanyaji, ila hiyo kodi ifikishwe serikalini, maana ni pesa ya serikali, mtu akitaka kudai bima atalipwa na serikali
 
Bima ni biashara kama nyingine. Kwa bahati mbaya wengi wanafahamu bima za magari tu, kuna aina chungu nzima za bima, na hizo hubuniwa au kutekelezwa na wajuzi wa bima.

Pia kufanya analsis ya risk na claims si jambo rahisi na kama Serikali itaamua kufanya wao itakuwa na urasimu mkubwa sana. Mfano rahisi ni mtu anayefuatilia mafao yake NSSF, anahitajika kuwa na viambatanishi vingi sana wakati kwa muda wa zaidi ya miaka 30 wamekuwa wakichukua makato yake na teknolojia ipo kubaini kama ni halali kwake kulipwa, just imagine iwe ni bima ya gari yako ya mizigo imepata ajali halafu unahitaji ulipwe au utengenezewe gari na serikali kwa kipindi cha ndani ya mwezi!

Mfano mwingine rahisi, tuna shirika la bima la taifa NIC nalo linafanya biashara ya bima kama makampuni mengine, hushangai halipo hata kwenye top three ya makampuni ya bima yenye mapato makubwa, kwa nini wateja hawalikimbilii?
Bima ni biashara ila si biashara kama biashara zingine, hii ni aina ya biashara inayohusisha kushurutishwa kulipa ,utake usitake lazima ulipe, na wanaoshurutisha ni maaskari wanaolipwa kwa kodi zetu, maana yake hizo pesa zinazokusanywa ji kodi ya seriakali na zinatakiwa zifikishwe serikalini, mawakala wanaokusanya wapewe comission kwa kazi hiyo ya ukusanyaji kodi / mapato ya serkali..,madai yote yatalipwa na serikali; ni kama tusema biashara anayofanya Tamesco ni biashra kama biashara zingine, si kweli, huko ni kujitoa ufahamu!!
 
Hivyo ndivyo nilikuwa nadhani na ndivyo inapaswa kuwa, trillion 3 kodi inakusanywa na hao mawakala lakini badala ya kuipeleka shirika la bima la taifa (NIC) wao wanabaki nazo mifukoni, halafu wanakuja kurudisha kodi yabkichwa wakati kodi kuna watu wanakaa nazo hawazifikishi serikalini, trillion 3 kila mwaka, ni pesa ya serikali hii, wao walipaswa wachukua comission tu kwa kazi ya kukusanya waliyofanya, baada ya hapo wapeleke shirika la bima la taifa!
Kweli hili NI shamba la Bibi..Kuna watu WANAKULA kilaini Sana.
 
Bima ni biashara ila si biashara kama biashara zingine, hii ni aina ya biashara inayohusisha kushurutishwa kulipa ,utake usitake lazima ulipe, na wanaoshurutisha ni maaskari wanaolipwa kwa kodi zetu, maana yake hizo pesa zinazokusanywa ji kodi ya seriakali na zinatakiwa zifikishwe serikalini, mawakala wanaokusanya wapewe comission kwa kazi hiyo ya ukusanyaji kodi / mapato ya serkali..,madai yote yatalipwa na serikali; ni kama tusema biashara anayofanya Tamesco ni biashra kama biashara zingine, si kweli, huko ni kujitoa ufahamu!!
Ndiyo maana nimekwambia bima una uwanja mpana. Kwa mfano hakuna anayekushurutisha kuwa na bima ya goods on transit, money on transit insurance, bulgraly insurance, fidelity guarantee, professional indemnity nk. Bima ambayo ni shuruti kisheria ni ya magari, na hapo unaweza kuchukua third party au comprehensive. Labda uwe specific unazungumzia bima gani.
 
Nani kabisha hilo, pesa iende serikalini, huyo third party atalindwa tu na serikali, hatuwezi kushindwa kumlinda kama taifa. Kama Umeme hakuna anaeruhusiwa kusambaza, basi hata hii inapaswa iwe chini ya serikali, watu tunalazimishwa kuwalipa watu binafsi trillion 3 kila mwaka kiulaini tu bila jasho, na usipolipa polisi wanakukamata, hivi ni ubongo au makalio tunayotumia kuwaza? Seriously?! Halafu watu wanarudisha kodi ya kichwa ili kuungeza mapato, wakati tumewcha wahindi wanachota tu pesa matrillion kwa kutulazimisha?!
Biashara tangu lini ikawa ya kulazimishana? Huu si ujambazi, kama ni lazima means hii ni kodi kama kodi zingine, sasa iweje mtu binafsi anachukua kodi trillion 3 , sisi ni mataahira??!!
Mkuu, fahamu kwanza mfumo wa insurance unavyofanya kazi. Ukifahamu mfumo wa bima na aina zake ulivyo utafahamu premiums zinavyogawanyika kutegemeana na aina ya bima, wajibu wa TIRA, Insurers, broker na agents. Au Nenda TIRA upate elimu.
 
Kama ni hivyo, hizo bima zote za hiari, ziendelee tu kufanywa na hayo makampuni ya bima, maana hakuna anaekushururutisha kulipa, lakini Bima zote zinazoshurutishwa, zilipwe moja kwa moja serikalini maana hayo ni mapati ya serikali, na madai yatalipwa na serikali. Hizo za hiari hakuna shida, maana mtu ni uamuzi wako ulipie au usilipie. Hapa nazungumzia bima za kushurutishwa!!
 
Niandike policy ya third party yako au sheria ya bima? Sorry boss, I wont.
Kwani umelazimishwa kuchangia uzi, nyamaza tu, hata sio lazima kunijibu, achilia mbali hiyo policy
 
Mkuu, fahamu kwanza mfumo wa insurance unavyofanya kazi. Ukifahamu mfumo wa bima na aina zake ulivyo utafahamu premiums zinavyogawanyika kutegemeana na aina ya bima, wajibu wa TIRA, Insurers, broker na agents. Au Nenda TIRA upate elimu.
Nimesema naomba kuelimishwa halafu wewe unasema nifahamu kwanza, sasa kwanini usinifahamishe, kumbe common sense isn’t so common!
 
Bima ni biashara ila si biashara kama biashara zingine, hii ni aina ya biashara inayohusisha kushurutishwa kulipa ,utake usitake lazima ulipe, na wanaoshurutisha ni maaskari wanaolipwa kwa kodi zetu, maana yake hizo pesa zinazokusanywa ji kodi ya seriakali na zinatakiwa zifikishwe serikalini, mawakala wanaokusanya wapewe comission kwa kazi hiyo ya ukusanyaji kodi / mapato ya serkali..,madai yote yatalipwa na serikali; ni kama tusema biashara anayofanya Tamesco ni biashra kama biashara zingine, si kweli, huko ni kujitoa ufahamu!!
Hii inamsaidia hata ambaye hahusiki na kulipa bima mf watembea kwa miguu, ukiwaumiza Bima ndo yatakiwa iwagharamikie etc
 
Kwani nani kabisha, ninachosema hizo bima za kushurutishwa zilipwe serikalini, na serikali italipa hao wa third party If and when required
 
Kwani umelazimishwa kuchangia uzi, nyamaza tu, hata sio lazima kunijibu, achilia mbali hiyo policy
Unataka nisichangie uzi sababu nimekuambia sitakupa policy na sheria ya bima? Aisee😀
 
Nimesema naomba kuelimishwa halafu wewe unasema nifahamu kwanza, sasa kwanini usinifahamishe, kumbe common sense isn’t so common!
Huwezi kuelimishwa hapa sababu swali lako ni pana mno, umeuliza kwann serikali isikusanye premium 100% sasa majibu humo ndani kuna sheria ya bima, kuna sera na uchumi unaingia ndo maana kuna minimum deposits lazima Insurers wawe nazo wamezifix.

Hili Swali lako ni carrier mtu anasomea mpaka msc

Ukiwatembelea TIRA utapata maelezo kwa kutegemeana na mtoa elimu atakavyojudge uwezo wako wa akili.

Hapa ni ngumu, utapata majibu mepesi sana au mazito sana. Unless unataka tu ukosoe upige pige porojo serikali ichekwe na wale wanaoikosoa na kufurahia ikipondwa halafu basi.
 
Hahaha, kumbe hujui maana ya jukwaa, jukwaa haimaanishi kufuata tu mfumo kama ulivyo, bali ni kuoendekeza maboresho ya hiyo mifumo (adjustments) kwa manufaa ya umma at large. Sasa ninchopendekeza ni hiki, bima zote za third party zilipwe serikalini kupitia wakala wa bima wa taifa, na malipo yatafanywa na wakala huyo kwa hao third party. Hayo matrillion yakaboreshe huduma za elimu, afya na miundombinu. Ifike mahala tuache kukopa wakati matrilioni yanabebwa na hawa wenye makampuni ya bima tena ni wageni, wanaenda kuwekeza kwao huko. Pendekezo ni hilo, sheria husika zirekebishwe ku-accomodate mtazamo huu mpya, na radical kabisa!
 
Nimepiga hesabu za haraka haraka, na kugundua kwamba makampuni ya Bima hukusanya wastani wa Trilioni 3.5 kila mwaka kama malipo ya bima za aina mbali mbali, na pia malipo kwa ajili ya bima (hasa hasa kwa wahindi wanaochoma moto viwanda vyao kwa makusudi) kwa mwaka huwa hayazidi bilioni 100, na ukitoa gharama za uendeshaji utaona inabaki kama trillion 3 hivi.

Sasa najiuliza, hii pesa tunayolazimishwa na matrafiki police huku barabarani kwamba ni lazima tulipe, inaenda serikalini na makampuni kubaki na comission tu au yote inaenda kwa haya makampuni ya Bima?!
Ukimaliza kuuliza hizi uje kuulizia zile za Mafao

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Hahaha, kumbe hujui maana ya jukwaa, jukwaa haimaanishi kufuata tu mfumo kama ulivyo, bali ni kuoendekeza maboresho ya hiyo mifumo (adjustments) kwa manufaa ya umma at large. Sasa ninchopendekeza ni hiki, bima zote za third party zilipwe serikalini kupitia wakala wa bima wa taifa, na malipo yatafanywa na wakala huyo kwa hao third party. Hayo matrillion yakaboreshe huduma za elimu, afya na miundombinu. Ifike mahala tuache kukopa wakati matrilioni yanabebwa na hawa wenye makampuni ya bima tena ni wageni, wanaenda kuwekeza kwao huko. Pendekezo ni hilo, sheria husika zirekebishwe ku-accomodate mtazamo huu mpya, na radical kabisa!
Okey, Unasahau kuwa sisi sio wajamaa 100% tunaruhusu makampuni binafsi yaje kufanya biashara na sisi tunakusanya kodi.

Naomba nikuulize kuhusu data zako za 3T ili tuone oportunity cost unayoizungumzia:

1.) Serikali amekusanya kiasi gani cha VAT + Kodi kutoka hizo kampuni?

2.) Amelipwa damage kiasi gani kama third party pale aliposababishiwa hasara?

3.) Iwapo yeye ndo angekuwa insurer(Ameamua kubeba hiyo risk) angetumia kiasi gani kufanya compasation kutoka katika makusanyo na angebakiwa na nn?

4.) Hizi deposit za kisheria ambazo makampuni yatatakiwa kuweka, serikali ingepoteza nini kwa kukosa ongezeko la huo mzunguko katika uchumi kama sheria inavyotaka?
20. -(1) Every insurer shall establish and maintain, at the Bank of Tanzania, a security deposit of at least fifty percent of the prescribed minimum paid up capital of the Company.

Nakuuliza hivi ili tupime kwa uelewa wa kawaida kabisa tunachokikosa kwa kutokufanya biashara ya bima sisi kama nchi.
 
1.) Suala la kwamba sisi sio wajamaa ni kweli, ila kuna biashara (sekta maalum) tunaruhusu wawekezaji kama mawakala au wasaidizi tu, mfano ni sekta ya umeme, muwekezaji atazalisha lakini lazima apitie Tanesco, uwekezaji wake unaishia kudeal na Tanesco, na sio kuuza moja kwa moja kwa mteja. Hata bima ni kwamba muwekezaji aje kuwekeza kama wakala tu, ila mapato yote ni mali ya serikali, hizi kampuni za bima zinaweza zikawa zinakusanya pesa nyingi kuliko serikali at times, kiulaini kabisa, tena nyenzo yao kubwa ni traffic police, ambao wanalipwa kwa kodi zetu, bila traffic hakuna mtu angelipa hiyo pesa.

2.)Hizo taarifa unazotaka, wewe ndio uzitafute halafu uweke, ila kwa hesabu zangu, ukitoa gharama zote na risk zote, atleast kuna Trillion 3 safi kabisa wanabaki nayo kwa mwaka, tungejemga flyover ngapi kwa hizp pesa? Kama unaona makadirio yangu yako off, basi lete wewe hizo data zako, na sio uniulize mimi
 
Chukua hio trilioni 3...asilimia 18 ndo hela ya serikali pia hizo zinazobaki zingine serikali inakuja kuzichukua interms of corporate tax..mleta mada shule ulikimbia ama?
 
Nani kabisha hilo, pesa iende serikalini, huyo third party atalindwa tu na serikali, hatuwezi kushindwa kumlinda kama taifa. Kama Umeme hakuna anaeruhusiwa kusambaza, basi hata hii inapaswa iwe chini ya serikali, watu tunalazimishwa kuwalipa watu binafsi trillion 3 kila mwaka kiulaini tu bila jasho, na usipolipa polisi wanakukamata, hivi ni ubongo au makalio tunayotumia kuwaza? Seriously?! Halafu watu wanarudisha kodi ya kichwa ili kuungeza mapato, wakati tumewcha wahindi wanachota tu pesa matrillion kwa kutulazimisha?!
Biashara tangu lini ikawa ya kulazimishana? Huu si ujambazi, kama ni lazima means hii ni kodi kama kodi zingine, sasa iweje mtu binafsi anachukua kodi trillion 3 , sisi ni mataahira??!!
Ainisha jinsi ulivyopata hizo Trillion 3
 
Back
Top Bottom