zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
1) Mkuu uwe unatumia data, mbona TIRA inatoa data Kila mwaka za claims. Mfano mwaka 2020 ripoti ya TIRA inasema kampuni za bima ziliingia hasara ya Billion 30 ikiwemo uwepo wa ajali nyingi hivyo claims zilikua juu sana. Njoo na takwimu mkuu sio maneno, kama wewe haufati sheria usidhani nchi nzima hawafuati sheria. Huwezi lazimisha serikali ibadili sera ya bima eti kisa wahuni wachache mnataka shortcut za kulipana kinyume na utaratibu.1.) Na ndio maana nikasema legeza ubongo, itakusaidia. Hatukatai kwamba hiyo ndio mifumo na utaratibu iliyopo, ambayo sasa tunapendekeza ibadilike kisheria, kwamba sheria iboreshwe ili ku-accomdate mawazo mapya, this being said; unapolipa pesa dukani kwa ajili ya ‘fire extinguisher’ maana yake unapewa ‘fire extinguisher’ unaondoka nayo, na hata ukitaka unaweza ukamuuzia mtu mwingine kama bado hauja expire na ukarudisha pesa yako ukitaka.
Sasa unapolipa kodi ya ‘third parry’ ambayo wewe unaiita ni bima, ni kwamba unapata tu uhuru wa kutumia barabara bila bughudha trfiki polisi, kwa sababu mwisho wa siku hata ukamgonga mtu, haiwezekani ukakubali hii kesi ipelekwe mahakamani ili tu kampuni ya bima wamlipe huyo uliyemgonga, maana mwisho wa siku, bima watamtibia huyo uliyemgonga na kumpa fidia kwa madhara aliyopata, lakini wewe uliyefanya uzembe ni lazima uadhibiwe kidogo, maana huwezi ukawa kila siku wewe kazi yako ni kugonga watu na kuwavunja miguu na kugonga taa za barabarani na kusababisha uharibifu eti kisa umelipa kodi ya ‘third party’ hivyo itakulipia tu halafu basi, lazima pawe na consequences, kama umegonga gari ya mtu na ukavunja taa zake, basi bima italipa lakini na wewe unaweza kwenda jela, hata kama ni wiki 1 tu, ila lazima uadhibiwe, hivyo kwa madereva wenye akili timamu, huwa wanaongea na waliyemgonga, wanaenda wote dukani, anamnunulia taa mpya anamfungia mambo yanaisha. Mimi mwenyewe huwa nakata comprehensive, lakoni niliwahi kugonga gari ya mtu ila trafiki alivyokuja nikaomba nimtengenezee gari yake na tukamalizana, maana hakuna mtu anayetaka kufikishwa mahamani!!
Sasa kwa wale wachache ambao uharibifu waliofanya upo nje ya uwezo wao kulipia ndio wanajikuta kesi inaenda mahakamani na bima wanalipa (kwa barabarani hii ni asilimia ndogo sana!)
Kwahiyo mwisho wa siku, hii kodi ya ‘third pary’ inaenda tu kwenye mifuko ya watu, na kidoogo sana ndio italipa claims, watu wanaogaopa jela, nani aje adai hiyo pesa ilipe halafu yeye aende jela, huu ni uwendawazimu, hii kodi ifikishwe serikalini.
Kodi hii tunalipa kwa lazima na ni fixed price kwa mujibu wa sheria, hiyo kusema kulipa kidogo kidogo no utaratibu wa kazi tu na si ushindani, hata TRA wapo watu wanalipa kwa awamu 4 (installments), sasa TRA anashindana nani? Au kuna TRA nyingine wanashindana nayo?
2.)Wanapeleka sehemu isiyo sahihi baada ya wewe kukubali kwanza hii ni kodi na siyo bima, kubali kwanza hilo ndio utaona kwamba wanapeleka sehemu isiyo sahihi, kodi hii ifikishwe serikalini, na zile third party claims chache (kama zitakuwepo), zitalipwa na serikali kupitisha shirika la bima la taifa na mawakala watapewa comission yao kwa kazi ya kukusanya kodi ya serikali. Kodi hii ni ‘fixed amount’ , ni ‘compulsory’ na unapoilipa unapata ruhusa tu ya kutumia barabara bila bughudha, and thats it, ni kama leseni flani hivi, hivyo ni kodi, (rejea point namba 1 hapo juu).
3.) Hakuna aliyebisha juu ya hilo, kwa bima zingine ambazo sio za kulazimishana mfano za comprehensive, bima za nyumba , na za afya huo mfumo uendelee tu kutumika, lakini kwa kodi ya ‘third party’ serikali itaunda sera zake za kuisimamia kodi hii na kulipa claim( if they arise).
4.) Rejea point namba 1 na 2, hii ni kodi na ifikishwe serikalini, hakuna upatu wa kulazimishana kwenye jasho la mtu, hii ni kodi.
2. Ile sio Kodi ni mchango maana hakuna ajali utakayofidia 120k haipo!! Fidia ya taa tu inazidi huo mchango wako kwa mwaka mzima. Kingine Ile hulipii kuepuka bugudha Bali ni usalama barabarani maana unaweza mgonga mtu na hauna Hela so Ile itaguarantee kwamba haki itapatikana kwa madhara uliyosababisha. Nachokiona watu msiopenda compliance ndio mnaiona kama Kodi, Ile sio "stika ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani" Ile ni package ya kufidia majeraha ya gari na mtu. Bima wanachukua 120k ila watalipa mara 20 ya hiyo sasa unaposema ni Kodi serikali itaweza kulipa mara 20 ya mahari ya nchi nzima? Si madai yatafikia trillion 1 kwa mwaka!!!
3. Sio za kulazimishana? Kaombe mkopo benki kama nyumba Yako haina bima ya moto hupewi!! Hata ukisafirisha mzigo wa thamani huwezi pewa tender ya Lori lako kama halina bima ya kusecure mzigo Au wizi!! Sababu tu hamshikiwi fimbo haimaanishi sio lazima, tukienda kwa staili hiyo mtarudi hapa kulialia kua tozo zimezidi.
4. Mbona fire extinguisher ni lazima ila sijaona ukisema tukanunue pale OSHA? Kodi ni pesa ila Bima ni mchango maana ukiidai haupewi 120k ila utapewa Mamillioni..... So nachoshauri kaongeze Elimu ya bima kabla ya kuhalalisha uvunjifu wa sheria wa kuepuka mahakama Ili mlipane mtaani!!!