1. Mkuu kuna kitu naona hatuelewani, ulazima wa kuilipa haimaanishi ni Kodi au stahiki ya serikali kumbuka Kodi inakatwa kwenye faida sio mapato. Sasa hiyo Premium ya third party ni "income" ndio maana kuna commission ya agent. Ni sawa tu na fire extinguisher ni lazima uwe nayo ila ulazima huo haimaanishi sasa fire extinguisher tuzinunue serikalini.
NB: ushindani haupo kwenye Bei tu mkuu, mfano KCB wanatoa mkopo wa bima yaani mfano hiyo 3rd party wanakulipia yote alafu wewe unapeleka labda elfu 12 Kila mwezi mpaka mwaka unaisha ushailipa kidogo kidogo. So unaweza ona competition Bado ipo ingawa Bei ni Ile Ile. Ukienda NMB nao utasikia lipia bima kidogo kidogo yaani muamala mpaka wa Buku unapokelewa!! So compeititon is still possible kwa product zenye fixed price.
2. Hawafikishi sehemu sahihi kivipi? Kampuni ya Bima inachukua risk so unakuta imewekeza kukulipia ajali ikitokea hivyo mteja hachukui hiyo 120k Bali italingana na ajali husika sasa hiyo risk ya Kampuni ya Bima ndio Ina charge premium kama mchango wa mteja how comes hiyo 120k ni ya serikali?? Embu ondoa kwanza wazo la Kodi hii ni mchango tu kama wa Upatu au Kikoba ambacho kampuni ya Bima ndio inachanga kwa wateja Ili mmoja wenu anapoleta claim basi atalipiwa hizo gharama ambazo mara nyingi huzidi hiyo 120k so Ile sio TAX ni CONTRIBUTION/PREMIUM.
3. Ndio maana nimekwambia kwa miongozo wa TIRA Kila kampuni ya Bima au Agency Inaweka dhamana BOT ya pesa Fulani ambayo italingana na mtaji hivi. So ikitokea mchango uliopitia kwa wakala haujafika NIC au Jubilee the TIRA itaenda kunyofoa kwenye dhamana Yako hivyo si kweli kuwa michango haifiki mahali sahihi.
4. Hakuna Kodi hapo huo ni mchango tu kama wa UPATU, gharama ni ya Kampuni ya Bima ambayo ita convert hiyo 120k ifike hata million 2 ikulipie ukipata claim.
TLDR; Ulazima wa kulipa 3rd party hakuifanyi kuwa Kodi maana Ile ni revenue tu. Kodi hukatwa kwenye benefit sio cost!!
1.) Na ndio maana nikasema legeza ubongo, itakusaidia. Hatukatai kwamba hiyo ndio mifumo na utaratibu iliyopo, ambayo sasa tunapendekeza ibadilike kisheria, kwamba sheria iboreshwe ili ku-accomdate mawazo mapya, this being said; unapolipa pesa dukani kwa ajili ya ‘fire extinguisher’ maana yake unapewa ‘fire extinguisher’ unaondoka nayo, na hata ukitaka unaweza ukamuuzia mtu mwingine kama bado hauja expire na ukarudisha pesa yako ukitaka.
Sasa unapolipa kodi ya ‘third parry’ ambayo wewe unaiita ni bima, ni kwamba unapata tu uhuru wa kutumia barabara bila bughudha trfiki polisi, kwa sababu mwisho wa siku hata ukamgonga mtu, haiwezekani ukakubali hii kesi ipelekwe mahakamani ili tu kampuni ya bima wamlipe huyo uliyemgonga, maana mwisho wa siku, bima watamtibia huyo uliyemgonga na kumpa fidia kwa madhara aliyopata, lakini wewe uliyefanya uzembe ni lazima uadhibiwe kidogo, maana huwezi ukawa kila siku wewe kazi yako ni kugonga watu na kuwavunja miguu na kugonga taa za barabarani na kusababisha uharibifu eti kisa umelipa kodi ya ‘third party’ hivyo itakulipia tu halafu basi, lazima pawe na consequences, kama umegonga gari ya mtu na ukavunja taa zake, basi bima italipa lakini na wewe unaweza kwenda jela, hata kama ni wiki 1 tu, ila lazima uadhibiwe, hivyo kwa madereva wenye akili timamu, huwa wanaongea na waliyemgonga, wanaenda wote dukani, anamnunulia taa mpya anamfungia mambo yanaisha. Mimi mwenyewe huwa nakata comprehensive, lakoni niliwahi kugonga gari ya mtu ila trafiki alivyokuja nikaomba nimtengenezee gari yake na tukamalizana, maana hakuna mtu anayetaka kufikishwa mahamani!!
Sasa kwa wale wachache ambao uharibifu waliofanya upo nje ya uwezo wao kulipia ndio wanajikuta kesi inaenda mahakamani na bima wanalipa (kwa barabarani hii ni asilimia ndogo sana!)
Kwahiyo mwisho wa siku, hii kodi ya ‘third pary’ inaenda tu kwenye mifuko ya watu, na kidoogo sana ndio italipa claims, watu wanaogaopa jela, nani aje adai hiyo pesa ilipe halafu yeye aende jela, huu ni uwendawazimu, hii kodi ifikishwe serikalini.
Kodi hii tunalipa kwa lazima na ni fixed price kwa mujibu wa sheria, hiyo kusema kulipa kidogo kidogo no utaratibu wa kazi tu na si ushindani, hata TRA wapo watu wanalipa kwa awamu 4 (installments), sasa TRA anashindana nani? Au kuna TRA nyingine wanashindana nayo?
2.)Wanapeleka sehemu isiyo sahihi baada ya wewe kukubali kwanza hii ni kodi na siyo bima, kubali kwanza hilo ndio utaona kwamba wanapeleka sehemu isiyo sahihi, kodi hii ifikishwe serikalini, na zile third party claims chache (kama zitakuwepo), zitalipwa na serikali kupitisha shirika la bima la taifa na mawakala watapewa comission yao kwa kazi ya kukusanya kodi ya serikali. Kodi hii ni ‘fixed amount’ , ni ‘compulsory’ na unapoilipa unapata ruhusa tu ya kutumia barabara bila bughudha, and thats it, ni kama leseni flani hivi, hivyo ni kodi, (rejea point namba 1 hapo juu).
3.) Hakuna aliyebisha juu ya hilo, kwa bima zingine ambazo sio za kulazimishana mfano za comprehensive, bima za nyumba , na za afya huo mfumo uendelee tu kutumika, lakini kwa kodi ya ‘third party’ serikali itaunda sera zake za kuisimamia kodi hii na kulipa claim( if they arise).
4.) Rejea point namba 1 na 2, hii ni kodi na ifikishwe serikalini, hakuna upatu wa kulazimishana kwenye jasho la mtu, hii ni kodi.