Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

Either hukusoma nilichoandika au hujaelewa nilichoandika, nimeshaeleza kwamba watafidiwa na shirika la bima la taifa, maana hiyo pesa kuna fungu watapewa kwa ajili hiyo, na kama litabaki basi litatunika kutop up fungu la mwaka unaofuata, na kama fungu litapelea (highly unlikely) basi kutawekwa mechanism ya hazina kutop up kilichopelea. Sasa iweje mimi nieleze hayo halafu uje kuuliza tena nikicho kwisha eleza, au una mtindio wa ubongo labda. Pia ni ‘thirdparty’ wangapi kwa mwaka huwa wanatoboa mahakamani na kulipwa? Ukichunguza takwimu za kiasi kinacholipwa kwa thirdparty kama fidia kwa mwaka ndio utacheka uzimie.

Sheria ibadilishwe kadri itakavyohitajika ili kodi ya ‘third party’ iende serikalini, na wenye makampuni wa bima walipwe commission kidogo kwa uwakala wao wa kukusanya kodi ya serikali. Simple and clear.
Una point sema Am sorry unaitoa wakati ambao sio sahihi
Tupo kipindi cha capitalism na hoja yako ilikuwa na mashiko kipindi cha ujamaa

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Good morning, tunaomba sasa kodi ya ‘third party’ ianze kuwasilishwa serikalini
 
Habari, ni wakati muafaka sasa kodi ya ‘Third party’ ikaanza kuwasilishwa seriakalini
 
Morning, tunasubiri kwa shauku kubwa kodi ya ‘Third party’ kuanza kuwasilishwa serikalini
 
Tujiandae sasa kupokea malipo ya kodi ya ‘third party’ serikalini, naona mambo yameanza huko .., 😂😂😂😂😃😃
 
Sasa kwanini serikali ishurutishe raia kuchangia watu binafsi matrilion kila mwaka ilihali yenyewe inakosa hata pesa ya kuboresha miundombinu ya barabara? Ni kwanini hii pesa ya bima isiende serikalini ili ikasaidie kuboresha huduma za kijamii, na kama mtu akihitaji kulipwa bima afuatilie moja kwa moja serikalini kupitia mawakala wa bima waliopo kila kona? Kwanini tulazimishwe na polisi kuchangia watu binafsi matrilioni kila mwaka?! Why?! Trillion 3 kila mwaka tunalizimishwa kuwalipa, kwnai nchi yao hii?!!
nani alikudanganya serikali haina hela
 
Muda umefika sasa, kodi ya ‘third party’ ianze kuwasilishwa serikalini
 
Third party insurance sio kodi Mkuu, labda mpaka Serikali ibadilishe sheria. Bima hii inamlinda mtu nje ya mkata bima na muuza Bima (ndio maana inaitwa third party). Gari linapita barabarani, kuna watumiaji wengine wa barabara kama magari mengine, waenda kwa miguu na miundombinu kama nyumba n.k. Hawa ndio wanalindwa na hiyo bima na sio mkataji bima. Kwenye situtation kama hiyo mkataji bima hana incentive ya kukata hiyo bima kwani haimlindi yeye na ndio maana ni compusory, ingekuwa ni hiari wenye magari wasingekata hiyo bima hivyo kusababisha niliowataja hapo juu (third parties) kutolindwa. Hao askari sio kwamba wanashurutisha bali wanafanya law enforcement ambalo ni jukumu lao la msingi, kuhakikisha sheria ya bima inafuatwa. Wazo lako kutaka Serikali ikusanye hiyo hela linazungumzika. Tatizo ni kwamba Serikali ina historia ya ku-mismanage biashara au aina yoyote ya makusanyo, mfano mzuri ni kwenye mifuko ya jamii. Ndio maana watu wako sceptical na hiyo idea.
Naomba kujua mfano mimi nimekata hyo third part bahati mbaya nikagonga taa ya barabarani ni wao watalipa au mimi niliegonga. Naomba ufafanuzi hapa.
 
Serikali haiwezi kufanya biashara na haina ubavu wa kuhudumia aina zote za bima kwa watu wote.

Bima ni biashara kama zingine ambazo faida lazima iwe inaonekana.

Kulazimisha kukata bima ni kukukinga wewe na hasara ya majanga usiyotegemea.

Sawa na vile unalazimishwa kufunga mkanda kwenye gari, kufuata sheria zote za barabarani.

Serikali inafaidika vile hamfi hovyo.

hapa kwenye serikali inafaidika vile hamfi hovyo pamenichekesha[emoji16]
 
Kuna hii bima ya vyombo vya matairi mawili huku Zanzibar niliuliza faida yake nikaambiwa ikitokea umemgonga mtu wao ndo watamtibia.
 
Naomba kujua mfano mm nimekata hyo third part bahati mbaya nikagonga taa ya barabarani ni wao watalipa au mm niliegonga..naomba ufafanuzi hapa.
Kama utakubali kulipa basi Tantoads watakupa bill yao ya kurepair damages na mtamalizana. Ila kama huna pesa au hutaki kulipa, Bima yako watalipa halafu wewe utaenda gerezani. Ndio maana madai ya thirdparty huwa ni kidogo sana, na hizi pesa zote huishia mifukoni mwa wageni hasa wahindi.

Ila tunachosema ni kwamba, hii kodi ya ‘Thirdparty’ iwasiliahwe serikalini, na madai yote ya thirdparty yatalipwa na shirika la bima la taifa.
 
Naomba kujua mfano mm nimekata hyo third part bahati mbaya nikagonga taa ya barabarani ni wao watalipa au mm niliegonga..naomba ufafanuzi hapa.
Bima yako ndio itatakiwa kufidia hiyo hasara na sio wewe. Tofauti ni kwamba WEWE hutafidiwa gari lako.
 
Kama utakubali kulipa basi Tantoads watakupa bill yao ya kurepair damages na mtamalizana. Ila kama huna pesa au hutaki kulipa, Bima yako watalipa halafu wewe utaenda gerezani. Ndio maana madai ya thirdparty huwa ni kidogo sana, na hizi pesa zote huishia mifukoni mwa wageni hasa wahindi.

Ila tunachosema ni kwamba, hii kodi ya ‘Thirdparty’ iwasiliahwe serikalini, na madai yote ya thirdparty yatalipwa na shirika la bima la taifa.
Acha upotoshaji Mkuu. Yaani bima yangu ilipe halafu mimi niende gerezani? Naanza kupata wasiwasi kuhusu uelewa wako wa masuala ya bima.
 
Either hukusoma nilichoandika au hujaelewa nilichoandika, nimeshaeleza kwamba watafidiwa na shirika la bima la taifa, maana hiyo pesa kuna fungu watapewa kwa ajili hiyo, na kama litabaki basi litatunika kutop up fungu la mwaka unaofuata, na kama fungu litapelea (highly unlikely) basi kutawekwa mechanism ya hazina kutop up kilichopelea. Sasa iweje mimi nieleze hayo halafu uje kuuliza tena nikicho kwisha eleza, au una mtindio wa ubongo labda. Pia ni ‘thirdparty’ wangapi kwa mwaka huwa wanatoboa mahakamani na kulipwa? Ukichunguza takwimu za kiasi kinacholipwa kwa thirdparty kama fidia kwa mwaka ndio utacheka uzimie.

Sheria ibadilishwe kadri itakavyohitajika ili kodi ya ‘third party’ iende serikalini, na wenye makampuni wa bima walipwe commission kidogo kwa uwakala wao wa kukusanya kodi ya serikali. Simple and clear.
Nilichogundua ni kwamba una wivu kwamba kuna watu wanapata hela kutokana na biashara halali ya bima, unataka hiyo hela iende Serikalini kana kwamba Serikali ina sifa ya kutumia hela vizuri. Pili huna uelewa kuhusu sheria na taratibu za biashara ya bima ndio maana bima unaita kodi. I rest my case.
 
Acha upotoshaji Mkuu. Yaani bima yangu ilipe halafu mimi niende gerezani? Naanza kupata wasiwasi kuhusu uelewa wako wa masuala ya bima.
Kwahiyo kisa una bima basi uwe reckless kugonga gonga tu mali za watu? Ingekuwa hivyo watu wangeharibu mali za watu kwa makusudi wakijua bima ipo, in anycase nipo hapa kuelimishwa. Either way, kodi ya ‘third party’ iwasilisjwe serikalini.
 
Nilichogundua ni kwamba una wivu kwamba kuna watu wanapata hela kutokana na biashara halali ya bima, unataka hiyo hela iende Serikalini kana kwamba Serikali ina sifa ya kutumia hela vizuri. Pili huna uelewa kuhusu sheria na taratibu za biashara ya bima ndio maana bima unaita kodi. I rest my case.
Sawa. Tunapendekeza sasa, kodi ya ‘third party’ ifikishwe serikalini ili tuache kukopa kopa kama mataahira.
 
Ni muda muafaka wa serikali kuanza kupokea kodi yake halali kabisa ya ‘third party’
 
Back
Top Bottom