Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

Matrillioni ya pesa yanayokusanywa na makampuni ya Bima kupitia mawakala wao ni za serikali au ni za nani?

Third party insurance sio kodi Mkuu, labda mpaka Serikali ibadilishe sheria. Bima hii inamlinda mtu nje ya mkata bima na muuza Bima (ndio maana inaitwa third party). Gari linapita barabarani, kuna watumiaji wengine wa barabara kama magari mengine, waenda kwa miguu na miundombinu kama nyumba n.k. Hawa ndio wanalindwa na hiyo bima na sio mkataji bima. Kwenye situtation kama hiyo mkataji bima hana incentive ya kukata hiyo bima kwani haimlindi yeye na ndio maana ni compusory, ingekuwa ni hiari wenye magari wasingekata hiyo bima hivyo kusababisha niliowataja hapo juu (third parties) kutolindwa. Hao askari sio kwamba wanashurutisha bali wanafanya law enforcement ambalo ni jukumu lao la msingi, kuhakikisha sheria ya bima inafuatwa. Wazo lako kutaka Serikali ikusanye hiyo hela linazungumzika. Tatizo ni kwamba Serikali ina historia ya ku-mismanage biashara au aina yoyote ya makusanyo, mfano mzuri ni kwenye mifuko ya jamii. Ndio maana watu wako sceptical na hiyo idea.
Kwani hicho unachokisema ni nani amebisha? Tunachosema ni kwamba sheria ibadilishwe ili hii kodi iliyobabatizwa jina la ‘third party’ kinyemela ifikishwe serikalini, maana ni compulsory, na ‘third party’ yeyote atapeleka claim yake serikalini kupitia shirika la bima na atalipwa, sasa sijajua kwanini unaandika vitu vingi ambavyo ni obvious na kila mtu anavifahamu.

Kuhusi biashara ni kama unavyoon Tanesco, japo kuna changamoto ili ni muhimu sekta flani flani nyeti zikabako serikalini., hiyo ni kodi ya serikali, Trillions and trillions kila mwaka zinaishia mifukoni mwa watu huku tukiendelea kukopa kama wendawazimu, mataahira aakubwa, wakati tuna akili timamu! Hii kodi inayoshuritishwa na jeshi l polisi si biashara, ni kodi, na ifikishwe serikalini.
 
Nani kasema bima haina umuhimu, tunachosema hiyo bima ikusanywe na haya makampuni kama mawakala tu, ila sio wao ndio wachukue hayo mapato, wao wapewe comission kwa kazi ya ukusanyaji, ila hiyo kodi ifikishwe serikalini, maana ni pesa ya serikali, mtu akitaka kudai bima atalipwa na serikali

Wazo zuri lakini nionavyo mimi Serikali ikiingia hapo makampuni ya bima ambayo wewe unapendekeza wawe mawakala tu ili pesa iingie serikali na wao wapewe comission hayo makampuni watashirikiana na wateja kufirisi huo mfuko wa bima maana watakuwa wakipeleka madai ya watu kulipwa kila day mpaka mfuko ufirisike
 
Sasa kwanini serikali ishurutishe raia kuchangia watu binafsi matrilion kila mwaka ilihali yenyewe inakosa hata pesa ya kuboresha miundombinu ya barabara? Ni kwanini hii pesa ya bima isiende serikalini ili ikasaidie kuboresha huduma za kijamii, na kama mtu akihitaji kulipwa bima afuatilie moja kwa moja serikalini kupitia mawakala wa bima waliopo kila kona? Kwanini tulazimishwe na polisi kuchangia watu binafsi matrilioni kila mwaka?! Why?! Trillion 3 kila mwaka tunalizimishwa kuwalipa, kwnai nchi yao hii?!!
Serikali inashurutisha kwani haiwezi kuwahudumia watu wakifikwa na majanga. Pia serikali inapata pesa za kujiendesha, hasa makapuni ya bima yakinunua hati fungate za serikali (benki kuu) n.k.
 
‘Third party’ ni malipo anayolipwa mtu ambaye ameathirika na chombo kilicholipiwa kodi ya ‘third party’, na hailipwi hivi hivi.., kama kuna ajali imetokea basi vielelezo vitaonekana tu, sasa utafake vipi mtu aliyegongwa na gari husika na traffic police kadhibitisha tukio husika, au gari imegongwa na traffic amedhibitisha, infact wenyewe magari huamua kumalizana wenyewe (matengenezo / matibabu) ili kuepuka jailtime, yaani wewe uliginga mtu au gari ya mwenzako, utalipiwa madhara uliyosababisha ila ni lazima kesi kwanza iamuliwe na upewe jail time kwa uzembe, hivyo ili ku-deter udanganyifu kama huo unaosema, basi sheria itaboreshwa ili jailtime iwe kubwa sana, ikiwezekana miezi 12 na kuendelea, na hii isiwe na mbadala wa faini, yaani ni jailtime tu, sasa hapo mtu ataona ni mara 100 amtibu huyo mtu aliyemgknga, kuliko kesi iende mahakamani, bima imlioie halafu eyey aende jela mwaka mzima! So sheria ya adhabu pia itarekebishwa kuendana na mfumo huu mpya.
 
Serikali inashurutisha kwani haiwezi kuwahudumia watu wakifikwa na majanga. Pia serikali inapata pesa za kujiendesha, hasa makapuni ya bima yakinunua hati fungate za serikali (benki kuu) n.k.
Hakuna sasa haja ya kuacha hayo matrillion ya ‘kodi’ iliyobabatizwa jina la ‘third party’ kinyemela yaingie mifukono mwa watu binafsi, maana kama watu wanalipa tena kwa kushurutishwa na polisi, basi pesa hizo hizo zitakazolipwa, sehemu kidogo itatumika kuwahudumia hao ‘third party’ watakaofikwa na majanga, sasa itashindwa vipi wakati mfuko wa bima wa taifa upo na watu wamechangia tena kwa lazima. Na ni kwanini sasa serikali ipewe comission kidogo au ikopeshwe kodi yake yenyewe kwa huo ununuzi wa hizo hati, yaani pesa yetu wenyewe halafu mnatukopesha at an intrest?! Huo ni utaahira, hiyo kodi ya ‘third party’ iende serikalini moja kwa moja, hivyo hakuna tena haja ya kukopa pesa yetu wenyewe kwa huo mfuko wa bonds. Tutaendelea kukopa kama wendawazimu hadi lini wakati tunaacha watu wanachukua kodi kiulaini tena tunayoshurutishwa na mapolisi wanaolipwa kwa kodi zetu tena?! Hii kodi ifikishwe serikalini
 
Serikali ina chake kwenye hizo bima...
Ni nani aliyebisha juu ya hilo? Tunachosema ni kwamba hiyo kodi ya ‘third party’ ifikishwe serikalini, makampuni ya bima yapewe tu comission kwa kazi yao ya ukusanyaji kodi hii ya serikali ambayo tunashurutishwa na polisi kuilipa. Mtu akiwa na madai yake ataenda serikalini kuliowa kupitia shirika la bima la taifa.
 
Ni wakti muafaka sasa kwa hii kodi ya ‘third party’ kufikishwa serikalini
 
Habari za asubuhi. Tunasubiri kwa hamu kubwa kodi ya ‘third party’ kuanza kufikishwa serikalini.
 
Habari, kodi ya ‘third party’ ni halali kufikishwa serikalini
 
Bima ni biashara kama nyingine. Kwa bahati mbaya wengi wanafahamu bima za magari tu, kuna aina chungu nzima za bima, na hizo hubuniwa au kutekelezwa na wajuzi wa bima.

Pia kufanya analsis ya risk na claims si jambo rahisi na kama Serikali itaamua kufanya wao itakuwa na urasimu mkubwa sana. Mfano rahisi ni mtu anayefuatilia mafao yake NSSF, anahitajika kuwa na viambatanishi vingi sana wakati kwa muda wa zaidi ya miaka 30 wamekuwa wakichukua makato yake na teknolojia ipo kubaini kama ni halali kwake kulipwa, just imagine iwe ni bima ya gari yako ya mizigo imepata ajali halafu unahitaji ulipwe au utengenezewe gari na serikali kwa kipindi cha ndani ya mwezi!

Mfano mwingine rahisi, tuna shirika la bima la taifa NIC nalo linafanya biashara ya bima kama makampuni mengine, hushangai halipo hata kwenye top three ya makampuni ya bima yenye mapato makubwa, kwa nini wateja hawalikimbilii?
bima ya hovyo kabisa ukifanya nao kazi wale.
 
Sasa kwanini serikali ishurutishe raia kuchangia watu binafsi matrilion kila mwaka ilihali yenyewe inakosa hata pesa ya kuboresha miundombinu ya barabara? Ni kwanini hii pesa ya bima isiende serikalini ili ikasaidie kuboresha huduma za kijamii, na kama mtu akihitaji kulipwa bima afuatilie moja kwa moja serikalini kupitia mawakala wa bima waliopo kila kona? Kwanini tulazimishwe na polisi kuchangia watu binafsi matrilioni kila mwaka?! Why?! Trillion 3 kila mwaka tunalizimishwa kuwalipa, kwnai nchi yao hii?!!
Kwenye malipo ya bima kuna kodi ya ongezeko la thamani, (18%) hivyo serikali inapata mgao wake kutoka kwenye huduma hiyo.
 
Kwenye malipo ya bima kuna kodi ya ongezeko la thamani, (18%) hivyo serikali inapata mgao wake kutoka kwenye huduma hiyo.
Kwani nani amebisha hilo? Tunachosema ni kwamba badala ya serikali kupewa hako ka commission cha 18% ukizingatia wao ndio wanawalipa matrafiki mishahara na kushurutisha rais kulipa hiyo kodi ilibambikizwa jina la ‘thirdparty’, ni kwanini basi hiyo kodi isifikishwe serikalini halafu hao mawakala wa Bima wapewe commission ya 10% kwa kazi yao ya kukusanya kodi ya serikali? , na thirdparty yeyote atakayetaka kulipwa bima atakapeleka madai yake serikalini kupitia shirika la bima la taifa
 
Kwani hicho unachokisema ni nani amebisha? Tunachosema ni kwamba sheria ibadilishwe ili hii kodi iliyobabatizwa jina la ‘third party’ kinyemela ifikishwe serikalini, maana ni compulsory, na ‘third party’ yeyote atapeleka claim yake serikalini kupitia shirika la bima na atalipwa, sasa sijajua kwanini unaandika vitu vingi ambavyo ni obvious na kila mtu anavifahamu.

Kuhusi biashara ni kama unavyoon Tanesco, japo kuna changamoto ili ni muhimu sekta flani flani nyeti zikabako serikalini., hiyo ni kodi ya serikali, Trillions and trillions kila mwaka zinaishia mifukoni mwa watu huku tukiendelea kukopa kama wendawazimu, mataahira aakubwa, wakati tuna akili timamu! Hii kodi inayoshuritishwa na jeshi l polisi si biashara, ni kodi, na ifikishwe serikalini.
Ungekuwa unajua usingeita hiyo bima ni kodi. Pili hiyo bima ambayo wewe unaiita kodi wakati sio kodi haikuanzishwa kinyemela labda kama hujui maana ya neno kinyemela. Kinachonishangaza ni wewe kung'ang'ania kwamba Serikali ikusanye hiyo hela wakati sio kodi. Wakibadilisha sheria ili hiyo hela iende Serikalini kama kodi waathirika watafidiwa kwa basis zipi? Nani atahakikisha Serikali inalipa wahanga wa hizo ajali? Kwa sababu hayo mabilioni ilyatakuwa sio bima tena bali ni makusanyo ya Serikali ambayo watatumia watakavyoona wao inafaa.
 
Either hukusoma nilichoandika au hujaelewa nilichoandika, nimeshaeleza kwamba watafidiwa na shirika la bima la taifa, maana hiyo pesa kuna fungu watapewa kwa ajili hiyo, na kama litabaki basi litatunika kutop up fungu la mwaka unaofuata, na kama fungu litapelea (highly unlikely) basi kutawekwa mechanism ya hazina kutop up kilichopelea. Sasa iweje mimi nieleze hayo halafu uje kuuliza tena nikicho kwisha eleza, au una mtindio wa ubongo labda. Pia ni ‘thirdparty’ wangapi kwa mwaka huwa wanatoboa mahakamani na kulipwa? Ukichunguza takwimu za kiasi kinacholipwa kwa thirdparty kama fidia kwa mwaka ndio utacheka uzimie.

Sheria ibadilishwe kadri itakavyohitajika ili kodi ya ‘third party’ iende serikalini, na wenye makampuni wa bima walipwe commission kidogo kwa uwakala wao wa kukusanya kodi ya serikali. Simple and clear.
 
Back
Top Bottom