Matukio ya kusikitisha katika Uongozi wa Kikwete {2010 - 2015}

Matukio ya kusikitisha katika Uongozi wa Kikwete {2010 - 2015}

KABLA ya Yusuf Makamba kung'olewa ukatibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alikuwa na msemo wa kumsifia Rais Jakaya Kikwete akisema, "Kikwete ni mtaji wetu."

Makamba ambaye baadaye aligeuzwa gamba la kwanza kuondolewa, alikuwa na maana kuwa Kikwete ni mtaji wa chama chake.

Lakini kwa maoni ya wengi sasa, Kikwete amegeuka mzigo mkubwa ndani ya chama na serikali, tofauti na majigambo ya awali ya Makamba na wenzake. Hata Makamba wa sasa – January, ambaye ni mtoto wake, anaweza kumzungumzia tofauti Kikwete wa sasa na yule wa awali.

Wa sasa anazungumza bila kupima athari ya anachokizungumza. Miongoni mwa matamshi ya Kikwete ambayo yamegeuka mzigo kwa chama chake na kumwondolea sifa ya kuitwa "mtaji wa chama," ni maelezo yake kabla ya uchaguzi mkuu uliopita.

Alisema alikuwa tayari kukosa kura za wafanyakazi kuliko kuwaahidi mishahara minono.

Katika hotuba yake kwa taifa, Rais Kikwete alimtaja mara saba Nicholaus Mgaya kana kwamba tatizo la mishahara ya wafanyakazi lilikuwa tatizo binafsi la Mgaya.

Hii inaonyesha wazi kuwa kauli ya rais halikuwa jambo aliloshauriana na wenzake kabla ya kulisemea.

Kauli nyingine tata aliyoitoa Kikwete inayomfanya aonekane mzigo kwa chama chake, ni ya kudai kuwa baadhi ya viongozi wa kidini walijiingiza kwenye siasa. Kauli hiyo ilisababisha umaarufu wake mbele ya wananchi kupungua.

Kauli hii ilifuatiwa na harakati za CCM kufanya mikutano wilaya zote nchini kujichunguza kwa nini kura za "kiongozi wao mpendwa" zilipungua. Wengi tulisikia na kuambiwa kwamba udini ulichangia.

Hadi leo, hatujaambiwa ilikuaje Kikwete ambaye ni muislam alipata kura nyingi kuliko Dk. Willibrod Slaa mkiristo katika mikoa yenye wakristo wengi kama Ruvuma, Kagera, Morogoro, Singida na Mbeya! Hii peke yake ni sababu tosha kuwa tathmini ya CCM ilikosa mashiko.

Rais Kikwete kwa sasa anawapa kazi ngumu watetezi wake baada ya kutoa kauli nyingine tata na isiyo na mashiko ya kuwaomba wenzake katika chama kujivua gamba.

Kama vile amesahau ni yeye mwenyewe aliwainua majukwaani – hata wale waliotuhumiwa kwa ufisadi – na kuwapigia debe.

Eti chama tawala kimekosa mvuto kwa vijana na hivyo kinapaswa kujivua gamba ili kipendwe na vijana. Nini?

Nikiri kwamba sielewi kujivua gamba kutaisaidiaje CCM kupata umaarufu kwa vijana wakati siku zote zinatolewa kauli tata na za kinafiki. Je, kijana gani atayemwamini mnafiki?

Iweje leo mwenyekiti atake wenzake katika CCM wajivue gamba kwa kuwatosa watu ambao yeye mwenyewe aliwatetea jana akidai hakuna ushahidi wa kuwachukulia hatua za kisheria?

Kabla ya uchaguzi wa 2010 tulielezwa kuwa hakuna ushahidi wa kuwajibisha wanaodaiwa kuhusika na kashfa za EPA, Meremeta, Richmond/Dowans, rada na ndege ya rais tunayoambiwa inatua viwanja vitano tu nchini.

Elimu hii kuwa hakuna ushahidi ilifuatiwa na taarifa za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kwamba kashfa kadhaa zimefanyiwa uchunguzi na penye ushahidi wa kutosha watapelekwa mahakamani, lakini mpaka leo wananchi wanaendelea kusubiri.

Kama hiyo haitoshi, kabla ya watetezi wa Kikwete kupata majibu ya hoja za wanaohoji umakini wake, yeye amekuja na kauli nyingine tata.

Alipokaribishwa katika hafla ya kumsimika askofu mjini Songea wiki mbili zilizopita, aliamuru maaskofu waache kuuza madawa ya kulevya (unga).

Kauli hii ya maaskofu kuuza unga ilifuatiwa na vipindi vya televisheni kwenye TBC vilivyoandaliwa kuhalalisha hoja hiyo. Katika moja ya taarifa hizo, walionyeshwa vijana walioathirika na madawa ya kulevya wakieleza kuwa madawa hayo huingizwa nchini na viongozi wa dini.

Mimi naungana na wale wanaosema rais wetu huwa hatafakari kwa pamoja na washauri wake kauli anazolenga kwenda kuzitoa hadharani.

Chukulia mfano wa hoja hii madawa ya kulevya. Hata kama kweli askofu mmoja au wawili wamewahi kuhusika, kauli yenyewe kaitolea wapi?

Wewe unakwenda kwenye mkutano wa maaskofu na waumini wao kumsimika askofu halafu unawaambia maaskofu hao waliokualika kuwa ni wauza madawa ya kulevya tena maneno yenyewe unayasema mbele ya waumini wao?

Na madai haya ya maaskofu kuuza unga unayasema leo wakati jana ulisema maaskofu walihusika katika kampeni chafu dhidi yako na kwamba walisababisha umaarufu wako upungue hata ukapata asilimia 60 chini kabisa ya asilimia 90 za mwaka 2005!

Sasa, kama Rais Kikwete hakuambiwa na washauri wake au kama hakufahamu uzito wa madai yake, najitolea kumwelimisha. Maana ya madai yake ni mbaya sana sawa na madai kuwa ‘Yesu si Mungu' yakitolewa sokoni.

Maana ya madai yale ya maaskofu kuuza unga kutolewa mbele ya waumini wa kikristo ni sawasawa na kuwaambia waumini hao kwamba "ninyi wakristu msiwafuate viongozi wenu hawa kwa sababu wao si lolote si chochote bali wauza unga."

Madai haya, hata yangekuwa na ukweli kiasi gani, yanamaanisha kashfa na matusi dhidi ya waumini hao, familia na rafiki zao. Umetukana mke, ndugu, mtoto wa askofu mbele yao.

Kueleza kuwa maaskofu wanauza unga ni sawa na kuwakashifu au kuwavunjia heshima mbele ya waumini wao na familia zao.

Mwambie Mhaya mambo ya kumkashifu mbele ya mkewe uone. "Wangambira stupid infront of my wife" ndivyo utajibiwa. Hao ni Wahaya. Bali kauli yenye maana hiyohiyo itatolewa na mtu yeyote atakayekashifiwa namna hiyo mbele ya wale anaojua wanamheshimu.

Alichokifanya rais ni sawa na kuwazuia waumini kutoa sadaka na zaka makanisani kwa sababu kufanya hivyo ni sawa na kuwawezesha wauza unga kwa kuwapa pesa wapate nauli ya kusafiria Ulaya na Marekani kufanya biashara ya unga.

Mimi sijawahi kuona mtu amekaribishwa mahali, badala ya kutoa ahadi za ushirikiano na kusifia ushirikiano katika mambo yaliyopita, akaanza kutusi waliomkaribisha. Diplomasia ya aina hii ni mpya kwangu.

Niseme kutoka rohoni kabisa kwamba kiongozi anayelalamikiwa kutodhibiti mafisadi, aliyeshindwa kutumia vyombo vyote vya dola kuwakamata na kuwafikisha mahakamani wahusika wa kashfa za kampuni ya Kagoda Agriculture, Meremeta na Deep Green hapaswi kutuhumu mtu.

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wakiwemo polisi, usalama wa taifa, jeshi na hata TAKUKURU, ambaye serikali yake imeshindwa kuwaambia wananchi wake kuwa mmiliki wa Kagoda ni nani, hakutarajiwa kabisa kurusha kombora kwa maaskofu.

Ni muhimu Rais ajue kuwa kila kauli moja potofu anayoitoa, kila tuhuma isiyo na mashiko na kila hoja muflisi anayoitamka, inapandisha chati wapinzani wake
 
me ni msomi tena nilyeelimika na ambaye nasimama kwa miguu yangu kuendesha maisha yangu. kudhani kuwa ubunge ni ajira ni kufilisika kwa mawazo. kazi gani qualifications zake ni kujua kusoma na kuandika tu? hivi mnyika naye atasema kuwa ana kazi?
kweli mkuu
 
mkuu, usihangaike na hawa wenye mawazo ya bavicha. hata katibu mkuu wao ndoa ilipomshinda alikimbilia kutelekeza familia na kupora mke wa mtu badala ya kurekebisha ndoa yake

We mbona mkeo anakushinda watu tunapakata tu ma kukusomeshea mtoto ...kaa kimya
 
gharama ya kuendesha mchakato wa katiba tu mnailalamikia. sembuse uchaguzi? chadema dhaifu sana

sasa kama mnafanya madudu na nyie ndio mna vyombo vote wataacha kulalamika?? Kama mkifanya mambo vizuri na kwa haki hakuna atakayelalamika wala kuandamana.
Ukiona unalalamikiwa ujue unakasoro kubwa...
 
me ni msomi tena nilyeelimika na ambaye nasimama kwa miguu yangu kuendesha maisha yangu. kudhani kuwa ubunge ni ajira ni kufilisika kwa mawazo. kazi gani qualifications zake ni kujua kusoma na kuandika tu? hivi mnyika naye atasema kuwa ana kazi?

Uhouse boy wako kwj Mwingulu nao unahitaji elimu zaidi ya matusi
 
Kwa asivokuwa na mshipa wa aibu, akisoma hii sredi ataanza kutabasamu. JK ni mwana jukwaa ajibu hoja.....
 
KAMBI ya upinzani imerejesha mjadala wa “udhaifu wa rais” bungeni kwa kutaja maeneo mbalimbali ambayo Rais Jakaya Kikwete alitakiwa kuchukua hatua, lakini badala yake alikaa kimya.

Michango ya wabunge wa upinzani, hata “majasiri” wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekariri orodha ya mambo ambayo serikali ya Rais Kikwete ilipaswa kuyachukulia hatua lakini haikufanya hivyo.

Tangu Jumanne wiki iliyopita, wakati John Mnyika (Ubungo- CHADEMA) alipotolewa nje ya bunge kwa kusema “rais ni dhaifu,” wabunge wamezidisha lawama kwa serikali kusita, kushindwa au kudharau kuchukua hatua katika mambo muhimu ya kitaifa.

Alikuwa Freeman Mbowe, kiongozi wa upinzani na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, aliyesema bungeni Dodoma juzi, kuwa hata mshikamano wa taifa umeachwa kumomonyoka.

Akijadili bajeti ya waziri mkuu, Mbowe alisema kutokana na propaganda za chuki zinazofanywa na viongozi wa CCM na vyama washirika, sasa mshikamano wa taifa uko hatarini kubomoka.

Alitoa mfano wa kauli za viongozi wa CCM kwamba chama chake ni cha kikabila na kikanda; na hivyo kupanda mbegu za ubaguzi katika jamii iliyokuwa imeungana.

Kinachofanywa na chama cha Kikwete, “…kinapandikiza chuki na mpasuko miongoni mwa Watanzania; kwani maneno huumba,” amesema Mbowe na kuongeza kuwa sura hiyo ya mpasuko kwa misingi ya ukanda na ukabila, imeanza kujitokeza hata wakati wa mijadala ndani ya bunge.

Mbowe ametaja mambo ambayo serikali ya Rais Kikwete haijatolea kauli kuwa ni pamoja na taarifa za makusanyo ya mabilioni ya shilingi na matumizi yake wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.

“Kambi ya upinzani inaitaka serikali kutoa mchanganuo wa matumizi hayo…ili kutekeleza dhana ya uwazi ambayo ni msingi wa utawala bora,” amesema Mbowe.

Ametaka pia kuwepo uwazi kuhusu matumizi katika kukimbiza mwenge – makusanyo na matumizi – ili wananchi waweze kuona iwapo bado kuna haja ya kuwa na zoezi hilo katika mazingira ya sasa kisiasa.

Kauli ya Mbowe ilitonesha vidonda vya lawama na shutuma kwa rais kutochukua hatua katika masuala mazito.

John Mnyika, katika andishi maalum kwa vyombo vya habari, akieleza alichotaka kusema bungeni kabla hajatolewa nje, anafafanua udhaifu wa rais.

Anasema katiba imempa rais mamlaka makubwa juu ya bunge. Kwa mfano, bunge likikataa bajeti ya serikali (Ibara 90 (2) (b)); rais analivunja.

“Kadhalika, udhaifu wa kanuni za Kudumu za Bunge umefanya wabunge kuwekewa mipaka (Kanuni 97 (2)). Hawaruhusiwi kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya serikali,” anasema.

Anahitimisha kwa kusema, udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa rais juu ya bajeti na uendeshaji nchi; kwa hiyo, udhaifu wa rais unaathiri maisha ya wananchi.

Mnyika anasema woga wa wabunge wengi, hususan wa chama kinachotawala ndio huwafanya wapige kura ya NDIYO hata kama walikosoa bajeti wakati wa kuchangia. Wanaogopa bunge likivunjwa huenda wasirudi “mjengoni.”

Hoja za rais kuwa dhaifu zilianza kujitokeza tangu miaka ya awali ya utawala wake. Ilifika mahali, aliyekuwa spika wa bunge, Samuel Sitta akamwambia aongeze “ukali kidogo” au alete bungeni muswada maalum wa kumwongezea makali ya kufanya maamuzi magumu.”

Udhaifu wa serikali ya Rais Kikwete ambao unawekwa kichwani kwake, ni pamoja na kushindwa kukusanya kodi kwa kiwango cha kuwezesha serikali kujitegemea kwa fedha za ndani ya nchi.

Mfano ni serikali kushindwa kukusanya kodi na huku ikitoa misamaha ya zaidi ya Sh. 1.7 trilioni wakati haina dawa, barabara wala vifaa vya shule, mishahara ya walimu na madaktari.

Udhaifu mwingine ni ule wa serikali kutumia zaidi ya kile inachokusanya na kusababisha serikali kukopa kutoka benki za kibiashara tena kwa matumizi ya kawaida na siyo maendeleo.

Kinachoonekana kukera wananchi, hasa katika siku za karibuni, ni serikali ya Rais Kikwete kukaa kimya juu ya madai ya walimu na madaktari.

Ni mwaka sasa tangu waahidiwe kutimiziwa madai yao; lakini serikali, ama imeshindwa, imesahau wajibu, ni dhaifu au haitaki kutimiza ahadi zake.

Yamekuwa mazoea kwa serikali kukimbilia mahakama kuu, katika dakika za mwisho, kuzuia migomo; wakati tayari wananchi wameanza kuumia na hata wengine kufa.

Rais na serikali yake wamelaumiwa kwa udhaifu wa kutochukua hatua dhidi ya mafisadi – ndani ya serikali na CCM.

Ama wamepuuza, wamekaa kimya, wamekuwa wapole, au wamesamehe tu kwa misingi ya kulindana kama ilivyoonyesha katika wizi mpevu na ufisadi wa akaunti ya madeni ya nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT).

Kwa mfano, wizi wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited wa zaidi ya Sh. 40 bilioni; unaoelezeka kuhusu nani alichukua fedha, kupitia benki ipi na baadaye katika benki zipi, umeachwa bila kushughulikiwa.

Katika midomo ya wahisani, neno udhaifu limekuwa msamiati wa kudumu. Wamekuwa wakitaka serikali kuondoa udhaifu katika matumizi ya fedha za umma na katika kukabiliana na rushwa kubwa na ndogo.

Kuna wakati wafadhili walitishia, na hata kusitisha misaada kwenye bajeti ya taifa, kwa kukerwa na udhaifu katika utekelezaji wa makubaliano na serikali.

Udhaifu mwingine umeonekana katika kwenda nje ya nchi kuomba misaada, wakati huohuo misaada anayopewa hailingani na thamani na raslimali zinazovunwa kwenye nchi anakotoka rais.

Au kutoa ahadi 99 ambazo thamani yake ni zaidi ya Sh. 9 trilioni wakati ahadi hizo hazitekelezeki; au serikali kutenga asilimia 70 kwa matumizi kwenye bajeti yake na asilimia 30 kwenye maendeleo. Huu dhahiri ni aina ya udhaifu wa serikali na viongozi wavivu wa kufikiri.

Inatarajiwa neno “udhaifu” litatawala mjadala wa mkutano wa bajeti hadi Agosti; huku wabunge wa CCM wakijibu mapigo na hata kutishia kupigana na kutishia kifo.
 
KAMBI ya upinzani imerejesha mjadala wa "udhaifu wa rais" bungeni kwa kutaja maeneo mbalimbali ambayo Rais Jakaya Kikwete alitakiwa kuchukua hatua, lakini badala yake alikaa kimya.

Michango ya wabunge wa upinzani, hata "majasiri" wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamekariri orodha ya mambo ambayo serikali ya Rais Kikwete ilipaswa kuyachukulia hatua lakini haikufanya hivyo.

Tangu Jumanne wiki iliyopita, wakati John Mnyika (Ubungo- CHADEMA) alipotolewa nje ya bunge kwa kusema "rais ni dhaifu," wabunge wamezidisha lawama kwa serikali kusita, kushindwa au kudharau kuchukua hatua katika mambo muhimu ya kitaifa.

Alikuwa Freeman Mbowe, kiongozi wa upinzani na mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, aliyesema bungeni Dodoma juzi, kuwa hata mshikamano wa taifa umeachwa kumomonyoka.

Akijadili bajeti ya waziri mkuu, Mbowe alisema kutokana na propaganda za chuki zinazofanywa na viongozi wa CCM na vyama washirika, sasa mshikamano wa taifa uko hatarini kubomoka.

Alitoa mfano wa kauli za viongozi wa CCM kwamba chama chake ni cha kikabila na kikanda; na hivyo kupanda mbegu za ubaguzi katika jamii iliyokuwa imeungana.

Kinachofanywa na chama cha Kikwete, "…kinapandikiza chuki na mpasuko miongoni mwa Watanzania; kwani maneno huumba," amesema Mbowe na kuongeza kuwa sura hiyo ya mpasuko kwa misingi ya ukanda na ukabila, imeanza kujitokeza hata wakati wa mijadala ndani ya bunge.

Mbowe ametaja mambo ambayo serikali ya Rais Kikwete haijatolea kauli kuwa ni pamoja na taarifa za makusanyo ya mabilioni ya shilingi na matumizi yake wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru.

"Kambi ya upinzani inaitaka serikali kutoa mchanganuo wa matumizi hayo…ili kutekeleza dhana ya uwazi ambayo ni msingi wa utawala bora," amesema Mbowe.

Ametaka pia kuwepo uwazi kuhusu matumizi katika kukimbiza mwenge – makusanyo na matumizi – ili wananchi waweze kuona iwapo bado kuna haja ya kuwa na zoezi hilo katika mazingira ya sasa kisiasa.

Kauli ya Mbowe ilitonesha vidonda vya lawama na shutuma kwa rais kutochukua hatua katika masuala mazito.

John Mnyika, katika andishi maalum kwa vyombo vya habari, akieleza alichotaka kusema bungeni kabla hajatolewa nje, anafafanua udhaifu wa rais.

Anasema katiba imempa rais mamlaka makubwa juu ya bunge. Kwa mfano, bunge likikataa bajeti ya serikali (Ibara 90 (2) (b)); rais analivunja.

"Kadhalika, udhaifu wa kanuni za Kudumu za Bunge umefanya wabunge kuwekewa mipaka (Kanuni 97 (2)). Hawaruhusiwi kupendekeza mabadiliko katika makadirio ya mapato na matumizi ya serikali," anasema.

Anahitimisha kwa kusema, udhaifu wa kikatiba umetoa nguvu kubwa kwa rais juu ya bajeti na uendeshaji nchi; kwa hiyo, udhaifu wa rais unaathiri maisha ya wananchi.

Mnyika anasema woga wa wabunge wengi, hususan wa chama kinachotawala ndio huwafanya wapige kura ya NDIYO hata kama walikosoa bajeti wakati wa kuchangia. Wanaogopa bunge likivunjwa huenda wasirudi "mjengoni."

Hoja za rais kuwa dhaifu zilianza kujitokeza tangu miaka ya awali ya utawala wake. Ilifika mahali, aliyekuwa spika wa bunge, Samuel Sitta akamwambia aongeze "ukali kidogo" au alete bungeni muswada maalum wa kumwongezea makali ya kufanya maamuzi magumu."

Udhaifu wa serikali ya Rais Kikwete ambao unawekwa kichwani kwake, ni pamoja na kushindwa kukusanya kodi kwa kiwango cha kuwezesha serikali kujitegemea kwa fedha za ndani ya nchi.

Mfano ni serikali kushindwa kukusanya kodi na huku ikitoa misamaha ya zaidi ya Sh. 1.7 trilioni wakati haina dawa, barabara wala vifaa vya shule, mishahara ya walimu na madaktari.

Udhaifu mwingine ni ule wa serikali kutumia zaidi ya kile inachokusanya na kusababisha serikali kukopa kutoka benki za kibiashara tena kwa matumizi ya kawaida na siyo maendeleo.

Kinachoonekana kukera wananchi, hasa katika siku za karibuni, ni serikali ya Rais Kikwete kukaa kimya juu ya madai ya walimu na madaktari.

Ni mwaka sasa tangu waahidiwe kutimiziwa madai yao; lakini serikali, ama imeshindwa, imesahau wajibu, ni dhaifu au haitaki kutimiza ahadi zake.

Yamekuwa mazoea kwa serikali kukimbilia mahakama kuu, katika dakika za mwisho, kuzuia migomo; wakati tayari wananchi wameanza kuumia na hata wengine kufa.

Rais na serikali yake wamelaumiwa kwa udhaifu wa kutochukua hatua dhidi ya mafisadi – ndani ya serikali na CCM.

Ama wamepuuza, wamekaa kimya, wamekuwa wapole, au wamesamehe tu kwa misingi ya kulindana kama ilivyoonyesha katika wizi mpevu na ufisadi wa akaunti ya madeni ya nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT).

Kwa mfano, wizi wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited wa zaidi ya Sh. 40 bilioni; unaoelezeka kuhusu nani alichukua fedha, kupitia benki ipi na baadaye katika benki zipi, umeachwa bila kushughulikiwa.

Katika midomo ya wahisani, neno udhaifu limekuwa msamiati wa kudumu. Wamekuwa wakitaka serikali kuondoa udhaifu katika matumizi ya fedha za umma na katika kukabiliana na rushwa kubwa na ndogo.

Kuna wakati wafadhili walitishia, na hata kusitisha misaada kwenye bajeti ya taifa, kwa kukerwa na udhaifu katika utekelezaji wa makubaliano na serikali.

Udhaifu mwingine umeonekana katika kwenda nje ya nchi kuomba misaada, wakati huohuo misaada anayopewa hailingani na thamani na raslimali zinazovunwa kwenye nchi anakotoka rais.

Au kutoa ahadi 99 ambazo thamani yake ni zaidi ya Sh. 9 trilioni wakati ahadi hizo hazitekelezeki; au serikali kutenga asilimia 70 kwa matumizi kwenye bajeti yake na asilimia 30 kwenye maendeleo. Huu dhahiri ni aina ya udhaifu wa serikali na viongozi wavivu wa kufikiri.

Inatarajiwa neno "udhaifu" litatawala mjadala wa mkutano wa bajeti hadi Agosti; huku wabunge wa CCM wakijibu mapigo na hata kutishia kupigana na kutishia kifo.

zote hizi ni porojo za mfa maji asiyeisha kutapatapa,sijui huu utoto utawaisha lini lakini hamtapata mnalolitaka.
 
Back
Top Bottom