Matukio ya kusikitisha katika Uongozi wa Kikwete {2010 - 2015}

Matukio ya kusikitisha katika Uongozi wa Kikwete {2010 - 2015}

itakuwa vizuri wakifanya hivyo kwani uzi utaimarishwa zaidi kwan uchunguzi utatiwa moyo na kuwekwa vitu muhimu sana kwa ajili ya mustakabali ya taifa la sasa na baadae.

Mods wafanye hivyo
 
Ikiwa tuko mbioni kumuaga raisi Jakaya baada ya miaka 10 ya utawala wake, ni mambo gani yamekuwa na uzito sana katika utawala wake?

1. Skendo za BOT
2. Safari za nje kavunja rekodi
3.
4.
5.
6.
7.
8.
9.
10.
 
3. Wizi wa EPA warudishe pesa bila kushtakiwa (Sijui zilirudi???!!!!)
4.
 
1..ni raisi aliyevunja baraza la mawaziri mara nyingi,
2..raisi anayehudumia na kuteua VIKI KAMATA WENGI kwa mabilioni ya kodi zetu huku anasema serikali haina hela ya kuwaongezea walimu mshahara
3..raisi aliyekua anajua MAFISADI NA WAUZA MADAWA YA KULEVYA ila hakuwashughulikia it means ANASHIRIKIANA NAO
4..Raisi aliyeendeleza utawala wa kifalme na kushndwa kuwawajibisha viongozi aliowateua na VIMADA wake wanapokosea
5...raisi anayeshnda angani kwenda kuomba BILION 20 AU 30 NJE huku hapa nchini KUNA UFISADI HADI WA BILION 500 unafanyika
6.,Sea wanipalo, mama sea sea
 
Meno na kucha umeviacha nyumbani au bado unatembea navyo,??, Nauliza tu.
 
Kwa kuacha tembo wachache na vifaru kuliko rais yeyote
Pia kwa kuzika wasanii na kupiga nao picha
 
... Pia kwa kuzika wasanii na kupiga nao picha
mkuu unaweza ukawa na ile picha ya mkulu na Boys II Men bila kusahau zile za kwenye bembea, nataka niwawekee kumbukumbu watoto, zitakuja wasaidia kujua kwa nini maliasili za nchi hii nyingi zimepotea kipindi cha utoto wao pia zitawasaidia kupembua aina ya kiongozi watakaye mchagua kwa wakati wao.
 
Matukio ya upinzani 2010
Slaa amtelekeza mzazi mwenzie

Slaa apora mke wa mtu na kuzaa nae.
Mbowe apora mke wa Mtoto wa mbunge wa Moshi mjini
Mbowe akatisha ziara ya ki umbunge ya Joyce mukyi nchini marekani nakumuita dubai ili wajivinjali.
Chadema wajilipuwa wenyewe ktk mkutano wao Arusha kutafuta umaarufu.
Lema ambaka flora njau UK.
Lema aliwa kabang baada ya kurudi UK.
Na wengine waendeleee.......
 
hata watoto watacheka
Matukio ya upinzani 2010
Slaa amtelekeza mzazi mwenzie

Slaa apora mke wa mtu na kuzaa nae.
Mbowe apora mke wa Mtoto wa mbunge wa Moshi mjini
Mbowe akatisha ziara ya ki umbunge ya Joyce mukyi nchini marekani nakumuita dubai ili wajivinjali.
Chadema wajilipuwa wenyewe ktk mkutano wao Arusha kutafuta umaarufu.
Lema ambaka flora njau UK.
Lema aliwa kabang baada ya kurudi UK.
Na wengine waendeleee.......
 
Lets be realist jaman kipindi kile cha Nyerere kutawala illikuwa ni ngumu zaidi kuliko sasa sababu wengi walikuwa hawana kipato elimu wala muelekeo vingi vilifanyika kwa uzalendo ambayo ndio kazi kubwa Nyerere alifanya baada ya kugundua huo ndio utakuwa msingi wa watu wake kufanikisha na kupata vile ambavyo hawakuwa navyo kwa kipindi cha nyuma. Na kudhibitishi ili angalia wazee wengi waliokuwa kipindi cha Nyerere wengi ni waadilifu na wazalendo sana kwa nchi yao ambapo iyo ni moja ya sifa kuu ambayo Nyerere aliwajengea na milele atakumbukwa kwa ilo, haitoshi pia kama alivyoamini kweli watu wake walianza kupata yale aliyoamini wangepata kama imani ya uzalendo ingejenga miyoyoni mwao ikiwa ni kuanzisha vyama na taasisi mbali mbali za maendeleo pamoja na benki,miradi pamoja na makazi ya wafanya kazi takribani wote wa Umma(Serekali) ili hali wakijikongoja kwenye maswala mengine kama afya na elimu .... Sasa turudi kwenye zama hizi za ndugu Kikwete kwanza vile ambavyo vilikuwa ni vikwazo kwa kipindi cha Nyerere kwake ni mteremko sana wananchi wanakipato na kodi inalipwa(japo si kwa namna inayostahili na yeye ndio ana engineer hivo,sababu wasiolipa kodi anawajua na ila hawachukulii hatua yeyote pasi taifa kujua nini sababu) pia hali ya uwelewa kwa watanzania wengi imeongezeka kwa maana ya elimu na utaalamu katika nyanja nyingi tu ikiwa ni pamoja na elimu yenyewe afya chakula malazi na makazi (basic human needs) ambayo imepelekea industrialization na hii ni moja ya sifa ya nchi inayokuwa kiuchumi...... Swali langu ni Je hivi vingine kama vile uzalendo, uwadilifu, uungwana, uwajibikaji, utumishi uliotukuka na kadhalika inakuwaje anashindwa kuusimamia ambavyo kwa mtazamo wangu mimi ni vyepesi kuliko hivyo walivyofanya wenzie? Je angepewa kipindi hicho nchi angeweza kuifikisha pale alipoikuta? Kwanini anaamini katika Nepotism rather than Expertism ili hali madhara yake ameyaona au ndio tuseme sikio la kufa halisikii dawa...? Matarajio yake ni yapi kwa watanzania pindi amalizapo mda wake? Anataka tumkumbuke kwa yapi ambayo ameyaanzisha yeye na kuyasimamia ki ukamilifu au barabara za Dar za mwendo kasi.... kama ndio zina mchango gani kwa taifa lote kwa ujumla wake?(kuhusu miradi ya umeme upembuzi yakinifu aliukuta swala ilikuwa niumaliziaji tu)....? naombeni msaada wa majibu jaman kwa yoyote mwenye jibu ama majibu NB: Nampa hongera kiasi kwa kujitaidi kwenye swala la uhuru wa viombo vya habari kwa kiasi flani kajitaidi kuliko waliomtangulia na ushirika na nchi za nje
 
Wakuu,

1. JK amekabidhiwa nchi ikiwa na amani kabisa, lakini Mheshimiwa huyu amekuwa ni mtu anayejificha kwenye matukio mbali mbali UDHAIFU wake usijulikane!

2. Alianza na Richmond ambayo ilitusumbua sana, hatimaye alivunja Baraza zima la Mawaziri, mambo yakatulia kidogo!

3. Hatujakaa vizuri tukasikia "Zanzibar sio nchi!" Hili nalo lilitusumbua sana hadi kupelekea Mabadiliko ya 10 ya Katiba ya Zanzibar, 1984 ili kuitambua Zanzibar kama "nchi!" Baadaye mambo yakatulia!

4. Tulishuhudia mgomo wa Madaktari na kuteswa kwa ULIMBOKA, lilisumbua sana akili za watu. Matukio mengine yaliyofanana na hayo: Kuuawa kwa wafuasi wa CHADEMA, waandishi wa Habari, Gesi ya Mtwara, nk. Yote hayo yalitufanya tu-concentrate na matukio menyewe zaidi kuliko ku-concentrate na mambo ya maendeleo!

5. Hili la ESCROW sihitaji hata kulielezea maana bado linaendelea kusumbuma akili za watu.

6. Hili la Katiba Mpya nalo limeleta kizaa zaa, ni kama vile limeletwa makusudi ili tugangamane nalo ili Mzee amalize ungwe yake ya Awamu ya Nne!

7. Hili la Mahakama ya Kadhi ndio funga kazi. JK anajua kabisa litatugawanya na litagawanya nchi vipande vipande! Kwa kuwa yeye ni mzee wa matukio yanayo-draw attention kwenye tukio lenyewe badala ya yeye mwenyewe basi tutakomaa nalo wakati yeye anaendelea kumalizia safari zake kwenye nchi ambazo alikuwa bado hajazitembelea! Hana shida na mshikamano na mustakabali wa nchi hii!

8. Bill Clinton alipoona issue yake na Monica Lewinsky imepamba moto, alihamisha attention kwa kuishambulia Iraq. JK naye akishaona kwamba kuna tukio ambalo linamlenga yeye na Serikali yake moja kwa moja analeta tukio jingine. Hili la Katiba lilifunikwa na ESCROW, hili tukio la ESCROW halijaisha tumeshaletewa mambo ya Mahakama za Kadhi.

Tunakorogwa sana kwa kweli! Nikimtafakari JK nashindwa kummaliza! Hapa sijagusia Mgogoro wa Malawi na Rwanda na baadaye na Kenya, Rwanda na Uganda kwa umoja wao! Yaani ni tatizo juu ya tatizo!

Karibuni kwa mjadala zaidi!!
 
Majungu haya. Unataka tujadili nini ilhali umeorodhesha matukio?
 
Ndugu yangu Buchanan, nchi yoyote inayoendelea kwa kasi lazima ikumbwe na misuko suko. Kwa haya yanayoendelea Tanzania ni athari mojawapo ya maendeleo chanya ya nchi yetu
 
Back
Top Bottom