Nyamayao
JF-Expert Member
- Jan 22, 2009
- 6,966
- 2,357
Duh Teamo!
Incident1: Tulitoka kwenye Harusi maeneo ya Golden Tulip - Harusi ilikuwa ya "Kilokole" - soda kwa sana! Nilikuwa na maraffiki zangu watatu - wote tumeoa na bahati mbaya wake zetu hawakuweza kuwa nasi kwenye hiyo harusi - Tumefika "Corner Baa" yapata saa sita Usiku tukaamua kuingia "Ambiance" kupata mbili tatu halafu kila mtu aondoke - Uwezi kuamini mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kutoka nje - ilikuwa tayari ni saa moja kasorobo asubuhi! Well - ndoa yangu ilisimama (nilisema ukweli) lakini ilichukua kama miaka mitatu kila mara wifu ananiuliza swali lile lile "in different ways" - rafiki zangu ndoa zao zilidondoka - sina uhakika walisema nini - lakini ni siku ambayo mpaka kesho ipo akilini mwangu!
Incident 2: Nimechukua "dada eliza" maeneo fulani ya Dar es Salaam, mara tupo kwenye anga za starehe kwa sana - home nilidanganya kuwa naenda kwenye msiba wa co-worker and will be late - Kosa yule co-worker nilimtaja kwa jina! Ghafla bin Vuu yule co-worker anapitia maeneo ya nyumbani - wifu anakuwa mdadisi anaamua kutomuuliza yule jamaa habari za msiba - lakini katika mazungumzo jamaa anaonyesha wazi kuwa hakuna msiba: Jamaa ananipigia simu na kunieleza kuwa amepitia nyumbani! "eliza" nilimuacha "gesti" na kuchomoka kama mshale - nili-make another story altogether: Msiba na mfiwa ilibidi wabadilishwe!
yaani jamani hawa mabinti humu ndani ndio wanakata tamaa kabisa, umenikumbusha moja ma colleague ambae kwa sasa kahamishiwa arusha kikazi....nae cku hiyo alinicngizia kwa wife wake kwamba tunaenda moshi kwenye sendoff ya mdogo wake nyamayao na cc kama unavyojua tupo kwenye kamati, katoka arusha bila kunitaarifu lolote anakujua alipokuwa anaenda, mie natokea nai naenda njoro nikasema nipitie shoprite then niunganishe, nakutana na wife, salamu salamu, mbona upo huku saa hizi? mie nipo eeeh na hapa napitia kwa sis tupate moja moto then ndio niunge kwa mama, naambiwa mr nae yupo njoro kwenye sendoff anakusubiri, mie nipo sendoff ya nani mbona cna taarifa?...akanikatiza juu juu tukaagana!...nilivuruga ile ndoa vibaya sana!