Matukio yanayoonesha uongo kwenye vitabu vya dini

Kweli unahoja ila unajua aliekuumba ndio ameweka ubongo wako kua kilaza hivo Hadi ukawaza hivo?
 
Kweli unahoja ila unajua aliekuumba ndio ameweka ubongo wako kua kilaza hivo Hadi ukawaza hivo?

Kilaza hanaga hoja....hii page ya kujadili nyie inawezakana ata Mungu mwenyewe anawashangaa hawa watu mbona wanaabudu tu kila kitu wakati mm kuna mambo Mengine ata sjasema wameletewa tu na wazungu na waarabu.
 
Huwezi nipangia jinsi ya kuishi dini umezaliwa umezikuta na utakufa utaziacha hiko kitabu biblia kinamiaka almost 7000 na bado wako wanaokiamin

Kama huamin biblia live your life huwez fanya watu wasiamin biblia kwa hoja zako dhaifu na za kiinga
Kwanini unaamini biblia na si msahafu?kwanini Mungu awe mmoja vitabu vyake viwe zaidi ya kimoja?
 
Hivi unapoenda kuomba ushauri kwa sheikh,wakili,padre,mchungaji,n.k. je huwa ni Mungu amekushauri au huyo uliyemuendea?
 
Mimi hili la bikira maria kubeba mimba bila kugongwa nalikataa kabisaaaa halipo na haitatokea,kwanini mtume muhamad naye hakuzaliwa kwa style hiyo?

Kiumbe gani kingine kimezaliwa kwa style hiyo?kwanini Mungu aliumba me na ke kwa wanyama wote?

Ujinga huu wa kuamini amini tu kila tualichoambukizwa na wazungu ufike mwisho bwana,je hao waislam wasioamini ukristo na yesu kuwa alizaliwa bila sex wanaadhibiwa kwa kutokuamini hivyo?

Bikra azae bado ni bikra huyo?
 
Huwezi kutoka kwenye mstari iwapo unania ya kupata ukweli na utapata ukweli kupitia wewe mwenyewe
 
Kwa uongo huu wewe ni mtumwa bado,wapo watu wanauwezo wa kutabiri na ikawa kweli bwana sema muafrika kama wewe huwezi kuamini hata kidogo utasema ni uchawi ila majibu ya vipimo vya ultrasound utakubali
 
Naomba uruhusiwe mjadala zisiwepo lugha za matusi huyu bwana kaleta hoja fikirishi kwa uelewa wake
Wewe ndiyo mjinga unaebadilishiwa eneo tu na mtu yuleyule bado ukaendelea kuamini ujinga.

Aliyekuletea biblia na dini anakwamjia umetokana na mavumbi ukiwa kanisani,huyohuyo shuleni anakwambia umetokana na mbegu za x na y pia manyani,yooote umeyashika na kuyaamini kabisaaa,sasa mjinga ni nani?
 
Ila ukweli ni kwamba shetani yupo pia mungu yupo .Sisi nikama bidhaa tu mwenye nayo anaweza kuitumia vyovyote anavyotaka
Kivipi?hakuna shetani kama yupo basi ni huyohuyo Mungu ndiyo maana binadamu akifariki kwa ajali,magonjwa,n.k mnasema ni mioango ya Mungu au Mungu ndiyo anamoangia kila mtu kifo chake!!
 
Sindio?
Na kulingana na biblia, wakristo wanaruhusiwa kunywa pombe ila waislamu hawaruhusiwi. Kwahio hio 'siku ya kihama' sjui itakuaje, kila mtu atahukumiwa kulingana na dini au itakuaje..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna hili la watu kunywa pombe/mvinyo eti ni damu ya yesu na itawatakasa na pia kula mkate eti ni mwili wa yesu utawaokoa,hivi hii ni laana na kurogwa unaona kabisa pombe na mkate halafu unaamini ni mwili na damu ya yesu/mtu.

Shitholes wote wasiotaka kudadisi ujinga kama huu sasa kunatofauti gani na sisi tunaoabudu miti na mawe na kufanikiwa ukilinganisha na wao masikini wengi waliojaa makanisani na misikitini?
 
Imani zote ni upuuzi tu. Hamna vitu kama ivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kulingana na concept ya Mungu nilivyoielewa katika imani ni kuwa Mungu ni kila kitu na kila kitu kimetokana na Mungu na kila kilichofanyika au kutendeka ni kwa mapenzi yake yeye aliyesema iwe na ikawa na hakuna anayempangia wala kumchagulia cha kufanya kilicho sahihi kwake kwa kuwa hakuna alichokiumba kilichokikamilifu isipokuwa ni yeye.

Mungu yu kila kitu tunachokifahamu kwa kuwa existance ya Mungu ndiyo uwepo wako, uwepo wa malaika,uwepo wa shetani, uwepo wa ulimwengu mzima, uwepo wa wema au uovu n.k kwa kuwa vyote vi ndani yake (kama parts za mwili wake) hivyo anaposema acheni dhambi watu wangu mtaangamia anajikosoa yeye binafsi na uumbaji wake kwa kuwa anaelewa mabaya yakizidi mizania ya wema na ubaya unaoleta balansi utapwaya na hatimaye atadhurika, na hii itamwondolea sifa ya ukamilifu ambayo ndiyo ukuu wake.

Kwani uovu ukiendelea atalazimika kuondoa kiungo kimoja kimoja kinachomkosesha hata kama ni mkono ataukata na kama ni jicho yuko radhi kuling'oa abakie na chongo "siyo maneno yangu bali ni Yesu mwenyewe katika mafundisho yake" ndiyo maana wapinzani wake umdhiaki kwa alama ya chongo katika ishara zao.

Naye anazidi kukuambieni ya kwamba je, hamjui ya kuwa ndinyi mu miungu? Na mimi ndani yake nanyi ndani yangu nasi pamoja naye tu wamoja.

Hivyo utaona kuwa kila part ya mungu aliyoiumba na kuipa uhai kama yeye ina utambuzi fulani wa kimungu ndani yake juu ya kuamua cha kufanya na kutokufanya bila kuingiliwa kama mungu mwenyewe, kikubwa Mungu utoa guidelines na counseling tu ila maamuzi ni yako, mwisho wa siku vyote ufanyika kwa ajili ya kukamilisha utukufu na mapenzi yake yeye aliyempaji.
 
Umeandika sana, lakini hujajibu hoja. Kulikuwa na ulazima gani amwumbe binadamu na adui yake awepo? Kama yeye ni pendo kweli, alimleta shetani ili iweje?

Hivi unayempenda unamwekea mitego badala ya ulinzi 100%?

Halafu hao waovu nao humwomba yeye na anawapa, tena anawapa sawa kabisa na watu wema, ili iweje? Huwezi kukataa. Waharibifu wa dunia kwa kufadhili uovu wanaishi kwa amani kuliko wanaodhurika na uovu huo. Kwanini?

Na kwanini dini imekuwa uchochoro wa upigaji tena kwa kutajwa yeye na wapigaji wananeemeka vilivyo huku yeye mwenyewe akiwanyima maskini na kuwapa wenye nacho?

Mimi ninafikiri dini na uwepo wa Mungu ni falsafa kama zilivyo falsafa nyingine ili to balance maisha ya watu na kuwezesha urahisi wa utawala wa watu.

Twende tubishane kwa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…