Unahisi umesoma insha na kuielewa kumbe bado; nimesema mungu ili akamilike kuitwa mungu lazima awe mbaya na mzuri at the same time kwa kuwa vyote uzuri na ubaya vipo ndani yake yeye lakini lazima viwe katika mizania sawa.
1Samweli 16:14-23 Basi, Roho ya BWANA ilikuwa imemwacha Sauli, na roho mbaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua.
Zaburi 106:40 Hasira ya BWANA ikawaka juu ya watu wake, Anauchukia urithi wake.
Kwa mfano huo wa mistari hiyo michache nadhani umenielewa sasa kuwa Mungu ndiye kila kitu ukijuacho ni binadamu, ni shetani,ni ulimwengu, ni vinavyoonekana na visivyoonekana vyote vinamkamilisha yeye vyote ni utukufu wake lakini vyote vinahitajika kwa mizania (mfano mema na mabaya) endapo kimoja kikitaka kuzidi dhidi ya kingine umdhuru yeye aliye mkamilifu hivyo hana budi kuchukua hatua.
Na viumbe vyote ukiwemo binadamu huko ulivyo kwa mapenzi na rehema zake yeye aliyetaka uishi hivyo, kwa kuwa mungu ndani yake ana upande wa WEMA/ UBAYA/WEMA NA UBAYA kwa pamoja/ISIYOELEZEKA.
(Ufafanuzi wa hiki kifungu huu hapa chini)
Kuna viumbe kaviumba kutenda mema (malaika), kuna viumbe kaviumba kutenda mema na mabaya(binadamu), kuna viumbe vimeumbwa kutenda mabaya tu(shetani) kuna viumbe au vitu atujui vyenyewe vina dhambi au havina (wanyama,ulimwengu kiujumla) na kuna hali au mambo hayaelezeki hata kwa fikra zetu au maneno n.k
Kama umenielewa sasa, zote hizi ni sifa za Mungu na ndiyo ukamilifu wake na hawezi kuviangamiza maana vina co-exist kwa kutegemeana na vyote kavipenda, kaviumba na kuvibariki.
Kama binadamu jukumu lako nikuhakikisha unabalance mizania ya wema na ubaya usiyumbe maana ukizidisha wema utaangukia kwa malaika na dunia itakutesa na ukizidisha ubaya utaangukia kwenye sifa isiyo yako pia ambayo ni ushetani hivyo kwa lugha nyepesi wapaswa kuishi katikati ndiyo maana bila kutenda dhambi na wema kwa pamoja binadamu hawezi ku-exist juu ya uso wa dunia kwa amani.